Serikali kujenga madarasa mapya manne katika kila shule ya Sekondari ya Serikali. Watoto wote 1M kuanza shule Januari 2022

Kumbe pesa zinatoka kwa wananchi? Halafu nyie wenye akili ndefu ndiyo sasa mnaimilikisha kwa vigogo wasiochangia lolote? Kwa hivyo tuwashukuru mno kwa lolote watakalo fanya na sehemu yoyote ya pesa hizo kwa vile sasa ni zao?

Hiiiiii bagosha!
Sasa hao wananchi hawana kiongozi wao? Ulitaka tuseme wananchi wamejenga madarasa 15,000? Unateseka Sana jamaa kwa kijiba cha roho 😁😁
 
Kwanini kila mtu asilipe kodi sote tuisikie chungu yake?

Kwanini matumizi ya kodi zetu yahodhiwe na awaye yote? Eti Samia kajenga hali uhalisia ni walipa kodi na yeye si mmoja wao?

Mengine haya waambieni Chatto na Makunduchi. Huku mtaumbuka tu.

Kama ni mwanamke wa 2025, tafuteni mengine kwani hata akisuluhisha haya:

IMG_20210930_170832_807.jpg

wa kumpa kura tutakuwapo!
 
View attachment 1962445

wa kumpa kura tutakuwapo!
Una matatizo na msingi wa mawazo Sana wewe ndugu..Samia tunae Hadi 2030 mimi Niko bara siko makunduchi tambua hilo.
 
Wewe umefanya lipi Kati ya ha hayo unayosema? Au unabwabwaja bila kuonesha mfano? Unataka nani akufanyie?
Nimelipa Kodi na Tozo ndio kazi yangu kama raia..., Hao tuliopwa kazi ya kutunga Sera na kuweka mambo sawa wanapwaya ndio maana kwenye nchi yenye vyanzo lukuki bado tunakamuana..., ingia mtaani uliza watu au bila kuuliza ukiona maisha yao ndio utajua mambo hayapo sawa (Na kama unadhani hii hali ni nzuri) nina wasiwasi na standard yako ya uzuri
 
Una matatizo na msingi wa mawazo Sana wewe ndugu..Samia tunae Hadi 2030 mimi Niko bara siko makunduchi tambua hilo.

Hata akikaa hadi 3000, wewe unaongelea 2030?

Kwani jiwe tulikuwa tunae hadi lini vile?

"Kweli wewe huna matatizo na msingi wa mawazo Sana wewe ndugu.."

Hiiiiii bagosha!
 
They better start ASAP just in-case there's a will to do so.
 
Safi Sana hili la wanafunzi kuanza shule kwa pamoja lina manufaa sana kwa walimu na wanafunzi kitaaluma.

Kwa walimu linapunguza mzigo wa kazi ya kuanza kufundisha mada upya kwa wale wa chaguo la pili. Hivyo inampasa aidha atumie muda wa ziada (remedial time) ikiwemo zile siku zinazompasa kupumzika kisheria siku za wikiendi au aongeze masaa/muda wa kukaa kazini tena mara nyingi maofisa elimu hulazimisha bila malipo ya overtime.

Kwa wanafunzi wanaochelewa kuanza (second selection) mara nyingi huanza mwishoni mwa mwezi wa tatu au wa nne kabisa. Wao mara nyingi wanaathirika kitaaluma na kisaikolojia. Kitaaluma walimu wengi huwaharakisha au huwarukisha baadhi ya mada ndogo au mada kuu. Mara nyingi pia hukosa kozi ya Kiingereza (English Orientation Course) Kama wenzao wanaoanza kuripoti shuleni. Na hata kama wakipewa huwa si vile inavyotakiwa. Kisaikolojia wengi wanakuwa mitaani kwa muda mrefu kuanzia pale walipomaliza mitihani yao ya darsa la Saba mpaka kujiunga, hivyo morali ya kusoma hupungua. Wengi ndio wanaongoza kuacha shule (School drop out),kuwa na kesi za utoro,kupata mimba,mapenzi,nidhamu n.k

Kiuhalisia chaguo la pili huwa hawafanyi vizuri kitaaluma na ndio waachaji shule wazuri. Naipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuliona Hilo. Lisimamiwe vizuri kwa manufaa ya vijana wetu.
Kwa hiyo hakutakuwa na "second selection"!???
Hiyo chaguo la pili ni kwa sababu ya upungufu wa madarasa/majengo/maboma!!??
 
Wajenge basi kwa mpangilio mzuri Yaan mpangilio mbovu ili mradi madarasa yamejengwa tu hakuna bustani
 
Elimu ya sekondari ni ya kuwafanya watoto wasitusumbue nyumbani waende shuleni wakakue na watoto wenzao.
Ulimwengu wa Sasa elimu ya sekondari sio tija labda iwe hiari kwa anaehiitaji.
Serikali ijenge vyuo vya ujuzi kila kata mtu akimaliza la saba akasomee ujuzi autakao Ili umfae maishani.
Huu mfumo wa sekondari tu chuo kikuu then akimaliza chuo kikuu anarudi mtaani kuendesha bodaboda,kuwa machinga,kuwa mamalishe sio afya ni kuongeza idadi ya masikini nchini,maana mtu akipata cheti uona aibu kujichanganya.
 
Hakuna second selection ndio
Wewe ni "kihiyo" na "kilaza" mkubwa.
"Second selection" ilianzishwa kwa sababu mbili.
Mosi, ni upungufu wa vyumba vya madarasa.
Pili, ni kutokana na wanafunzi wengi wanaochaguliwa kwenda shule za umma kutokwenda kunakotoka na kwenda shule binafsi hivyo kuacha nafasi nyingi za wazi kwenye shule za umma.

Daaah
 
#2025Fever itawapotezea muda wenu bure,hakuna wakumuangusha Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi hizi kubwa na nzuri anazozifanya,

#KAZIIENDELEE NA MAMA
 
Hakika kama mambo yataendelea kuwa hivi Rais Samia Suluhu Hassan atashinda Uchaguzi Huru na Haki wa 2025 kwa zaidi ya 76%
 
Tanzania tuko katika uelekeo sahihi sana tuendelee kumwombea rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan,

Tunakila sababu ya kujivuna,
 
Rais Samia kujenga madarasa mapya manne ( 4 ) katika kila ilipo shule ya Sekondari ya Serikali nchi nzima | Watoto wote 1M wa kidato cha kwanza nchi nzima kuanza shule Siku moja ambayo ni tarehe 06|01|2021

====================================
Tanzania inajumla ya shule za sekondari 5,143 hii ni kwamujibu wa Shirika la Taifa la takwimu yaani NBS huku kati yake shule 3,863 ni shule za Serikali |Umma huku shule 1,280 zikiwa ni shule binafsi|Private schools,

Rais Samia Suluhu baada ya kupata anachokiita "Kijipesa " mahali sasa ameamua kuwatua mzigo wazazi kwa kujenga jumla ya madarasa mapya elfu 15,"Hii haijawahi kutokea " alisikika Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya TAMISEMI akisisitiza chanzo ni " UTV Habari" jana trh 01|10|2020 Saa 2 Usiku,

Sasa ukichukua haya madarasa yote 15,000 ukayagawanya kwa shule zote za sekondari za Serikali 3,863 kila shule itapata wastani wa madarasa mapya manne ( 4 ) kwa lugha rahisi Rais Samia Suluhu Hassan ataongeza wastani wa madarasa manne katika kila shule ya serikali Tanzania nzima hakika Rais Samia Suluhu ni masikini anayekumbuka masikini wenzake,

Mtakumbuka pia ni jumla ya watahiniwa elfu 460 ndio wanatarajiwa kumaliza kidato cha nne mwezi ujao huku matarajio ya Wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza ni jumla ya wanafunzi milioni moja sawa na ongezeko la zaidi ya wanafunzi elfu 500,Hawa ndio walimnyima Mama Samia Suluhu Hassan usingizi na tayari amelimaliza hili, nakufanya kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania watoto wote waliofaulu kwenda kidato cha kwanza kuripoti kwa tarehe moja nchi nzima ambayo ni tarehe 06|01|2022

Hata hivyo watoto hawa hawatalipa ada hata mia kwani tayari Rais Samia ameshapeleka jumla ya Tshs 62.4bl kwa halmashauri zote 184 yaani mambo ni bam bam,

.........Kazi iendelee .........

==================================

Kidato cha kwanza 2022 wote kuanza shule siku moja
MONDAY SEPTEMBER 27 2021

Summary

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu amesema wanafunzi watakaochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwakani wote wataanza shule siku moja tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu amemuhakikishia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wanafunzi watakaofaulu na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwakani wote wataanza shule siku moja.

Ummy amesema hayo leo Jumatatu Septemba 27, 2021 katika mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ngazi ya Taifa unaofanyika mkoani Dodoma.

Amesema amepata maagizo kutoka kwa kiongozi huyo kupitia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwa asingependa kuona mwakani wanafunzi wanapishana kuanza shule kwa kisingizio cha uhaba wa madarasa.

“Ujumbe wako Rais nimeupata, hakuna cha kusubiri, madarasa lazima tuyajenge na nikuhakikishie tayari tumeshaanza kuyafanyia kazi, na wanafunzi wote itakapofika siku ya kufungua shule Januari 6, wote wataanza kwa pamoja, hakuna cha wa kwenda baada ya kusubiri miezi miwili au mitatu ili tumalize madarasa,” amesema Waziri huyo.

Alimshukuru Rais Samia kwa kuendeleza sera ya elimu bila ada, kwani katika miezi yake miwili ya bajeti yake ya kwanza ya mwaka 2021/22 wameshapeleka kwenye halmashauri zote 184 Sh62.4 bilioni.

“Tunakushukuru Rais, kwani kulikuwa na uzushi kwamba elimu bila malipo itafutwa chini ya uongozi wako lakini wote ni mashahidi fedha zimeshakwenda katika halamshauri zetu katika shule zetu za msingi na sekondari.

“Katika hili tunakushukurum, umesaidia watoto wa maskini kupata elimu,”amesema Ummy.

Kutokana na sera hiyo ya elimu bila malipo, Waziri huyo amesema wanafunzi wanaotarajiwa kuanza kidato cha kwanza ni takribani milioni moja wakati wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne ni 460 elfu kwa hiyo kuna ongezeko la wanafunzi wa kidato cha kwanza zaidi ya 500 elfu

VIVA SAMIA VIVA || VIVA TANZANIA VIVA

View attachment 1960234
Kaziiendelee Tanzania, Hongera Mama Samia
 
Kaziindelee Tanzania na Samia
 
Back
Top Bottom