Serikali kukopa Fedha NMB kwaajili ya kununua Mabasi 100 ya Mwendokasi

Serikali kukopa Fedha NMB kwaajili ya kununua Mabasi 100 ya Mwendokasi

Naanza kushtuka taaratibu inawezekana hata bandari mwarabu pale katumiwa tu ila mabos wako hapa hapa tu maana tukiuliza huyo mwarabu bandarini amekuja na nn kuwekkeza maana serikali ilishawekeza .jibu ni hola kaja tu na mfumo anakula hela za majinga.Sasa hata mwendo kasi naona ni haya haya tunakopa sisi wao wabakuja na mfumo wanakula hela 🤣🤣🤣ila kuna siku haina jina hii nchi patanuka na haiko mbali hiyo siku.
 
Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu, amesema katika jitihada za kuboresha uendeshaji wa mabasi ya mwendokasi benki ya NMB imekubali kutoa mkopo kwa Serikali ambayo inamiliki kampuni ya UDART kwa 85% ili kuongeza mabasi zaidi ya 100 ya mwendokasi.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo July 15,2024 katika Mkutano wa Msajili wa Hazina na Wahariri wa Vyombo vya habari, Mchechu amenukuliwa akisema “UDART sasa hivi ni kampuni inayomilikiwa 85% na Serikali, ilipoanza ilikuwa inaendeshwa na Sekta binafsi Serikali ilikuwa na mchango mdogo, tukajikuta ina madeni mengi, mabasi yake ndio hivyo, kwa miezi miwili nimekuwa nafanya vikao na DART kampuni inayosimamia miundombinu, na UDART inasimamia uendeshaji na mabasi”

“Tunaenda kuongeza idadi ya mabasi na kesho nina kikao na benki ya NMB ambayo ndio wanatukopesha, tutakuwa na kikao pale NMB na UDART, DART, LATRA kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa fedha wa kupata mabasi yasiyopungua mabasi 100 ambayo yataweza kutusaidia”

“La pili kwa hatua tuliyofikia tunahitaji kampuni zaidi ya tano au sita, sio kampuni moja tu ambayo siku wakigoma au kupata matatizo Mji wote umesimama, unapokuwa na Waendeshaji wengi pia ni rahisi kujua nani anatoa huduma nzuri”

“Tutahitaji miezi sita kuanzia tunapotoa oda mpaka mabasi yaje, tutafanya maongezi na NMB kesho tutajua lini mabasi yatakuwa yanafika, najua nitamuachia Mkurugenzi Mkuu wa UDART na Bodi yake kuisema kwa Umma lakini kazi yetu ni kuhakikisha wanapata pesa”

Millard Ayo

Mwekezaji muarabu tunamkopea mabasi ila deni ni letu ....hawa ndiyo wawekezaji ambao SAMIA ANATULETEA NI WAHUNI TU NA MAFISADI WAJOMBA ZAKE ...SAMIA KAIVUA NGUO NCHI IPO UCHI WA MNYAMA KILA MUHUNI ANAJIPIGIA.
 
NMB Hakikisheni hizo audited accounts wanazowaletea zimekua audited na kampuni ya nje inayojiheshimu.
Kama zimekua audited na Patel, Bashe ,Gekul & company or any other questionable company achaneni nao.
 
Hasara ya mwaka hii: yaani mwarabu aje na kanzu tuu hela atazikuta hapa hapa.
Hii dunia ina mambo kweli na DP World napo waarabu wamekuja kukuta kila kitu na pesa za kuendesha bandari wamepewa.
 
Nimepata hasiraa.. Kama walisema wametafuta mwekezaji, Serikali inanunua mabasi ili iweje?

Miaka yote ya kuendesha mradi umeshindwa kumaintain na kujinunulia mabasi mapya mpaka unakopa?

Ujenzi wa barabara mkopo na uendeshaji wake ni mkopo!

Kama wamezishindwa kwanini wanaingia madeni mapya kujenga barabara mpya tena nyembamba kuliko za awali ilhali ya ruti ya Kimara wamenyoosha mikono!

Na mbona kakimbia kutaja kiwango cha mkopo!
Ccm no maongoo.Huyo Dubai yuki wapiii?
 
Mwekezaji muarabu tunamkopea mabasi ila deni ni letu ....hawa ndiyo wawekezaji ambao SAMIA ANATULETEA NI WAHUNI TU NA MAFISADI WAJOMBA ZAKE ...SAMIA KAIVUA NGUO NCHI IPO UCHI WA MNYAMA KILA MUHUNI ANAJIPIGIA.
Hao wahuni walikua wamejazana kwenye mahoteli huko wanatafuta madili watupige Magu alikua anawakataa ila kwa sasa ndio wamepata nafasi.

Kila kitu sasa hivi ni dili.
 
Very idiotic idea. Zaidi ya Kisenya Nani mwingine kafungwa?
Kwa miaka mingapi mradi huu utakuwa white elephant?
Miradi hii isiyolipa ndiyo mojawapo imepelekea Wastaafu kulipwa Mafao ya Kikokotoo. Ipo siku Nmb watapandisha Riba Kwa Wateja kufidia Madeni Kwa Serikali. Siku zote Hizo Udart haijazalisha Fedha ya kununua Mabasi mapya? Kama Serikali hatuwezi biashara mnajiingiza huko kwa nini?
 
Back
Top Bottom