Serikali kukopa Fedha NMB kwaajili ya kununua Mabasi 100 ya Mwendokasi

Serikali ya mama Yao imekosa mwelekeo kabisa.kila kitu kinaenda hovyo hovyo tu.hadi unapata hasira kabisa unatamani huu mradi ufutwe tu.wataleta hayo magari baada ya miezi miwili yanakufa sijui Tena watakopa Hela zingine wakanunue mengine!hizo riba za mikopo tunakamuliwa sisi wananchi.
 
Nimepata hasiraa.. Kama walisema wametafuta mwekezaji, Serikali inanunua mabasi ili iweje?

Miaka yote ya kuendesha mradi umeshindwa kumaintain na kujinunulia mabasi mapya mpaka unakopa?

Ujenzi wa barabara mkopo na uendeshaji wake ni mkopo!

Kama wamezishindwa kwanini wanaingia madeni mapya kujenga barabara mpya tena nyembamba kuliko za awali ilhali ya ruti ya Kimara wamenyoosha mikono!

Na mbona kakimbia kutaja kiwango cha mkopo!
Hayo mabasi wanamnunulilia mwekezaji na ukute mwekezaji NI mapapa wa nchii hii yanatumia fedha zetu wenyewe halafu yanakuja kwa mgongo wa uwekezaji ! Serikali inanunua mabas baadae utasikia amepatikana mwekezaji
 
Kumbe unajua halafu unazunguka zunguka tu
 
Kwaiyo uyo Dubai anakuja na nini?
Hapo hakuna wa Dubai kuna kivuli cha wadubai Ila wazee wakucheza na system wapo bongo hapahapa tunadanganywa mwekezaji kumbe kuna mtu anatafuna fedha za umma kwa kivuli cha uwekezaji
 
Nitajibu swali la pili tu.
Waliosababisha Ni kina Mhede, yule aliyeshindwa TRA, akashindwa vibaya UDART, Sasa hivi Ni NAIBU KATIBU MKUU.
tilia mstari KATIBU MKUU wa wizara.
Unaweza kuta na huyu wa Sasa akifeli akapewa posti nyeti.
Na kuelewa ingawa sidhani kama Mhede ndio aliifikisha hapo..huyo aliikuta UDART ipo ICU, akaizika kabisa..shida yangu kuu ni akina nani waliipeleka ICU na wamechukuliwa hatua gani?
 
Kwa nini hayo mabasi wasiyabinafsishe tu kwa sekta binafsi, halafu hiyo serikali ikajikita kwenye ukusanyaji wa kodi na pia kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji!
Wazo zuri, watafute mwekezaji wa kuendesha huo mradi.
 
Mabasi ya mwendokasi wanakopa ila maV8 ya kutembelea wao hawakopi.. Shubastad..

Na je wana uhakika haya yaliyopo hayatoshi, kama mara 2 hivi nishakuwepo kituo cha mwendokasi pale feri, linakuja basi, linashusha watu linapaki, jingine linakuwa tupu, linaondoka likiwa tupu, jingine linashusha kisha linapaki, haji mpaka mjazane, yaani upite muda fulani ndio aje, haijalishi mko wengi kiasi gani.. Kabla ya mabasi mapya kwanza watizame waendeshaji wana akili humo vichwanj mwao!??
 
Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu, amesema katika jitihada za kuboresha uendeshaji wa mabasi ya mwendokasi benki ya NMB imekubali kutoa mkopo kwa Serikali ambayo inamiliki kampuni ya UDART kwa 85% ili kuongeza mabasi zaidi ya 100 ya mwendokasi.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo July 15,2024 katika Mkutano wa Msajili wa Hazina na Wahariri wa Vyombo vya habari, Mchechu amenukuliwa akisema “UDART sasa hivi ni kampuni inayomilikiwa 85% na Serikali, ilipoanza ilikuwa inaendeshwa na Sekta binafsi Serikali ilikuwa na mchango mdogo, tukajikuta ina madeni mengi, mabasi yake ndio hivyo, kwa miezi miwili nimekuwa nafanya vikao na DART kampuni inayosimamia miundombinu, na UDART inasimamia uendeshaji na mabasi”

“Tunaenda kuongeza idadi ya mabasi na kesho nina kikao na benki ya NMB ambayo ndio wanatukopesha, tutakuwa na kikao pale NMB na UDART, DART, LATRA kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa fedha wa kupata mabasi yasiyopungua mabasi 100 ambayo yataweza kutusaidia”

“La pili kwa hatua tuliyofikia tunahitaji kampuni zaidi ya tano au sita, sio kampuni moja tu ambayo siku wakigoma au kupata matatizo Mji wote umesimama, unapokuwa na Waendeshaji wengi pia ni rahisi kujua nani anatoa huduma nzuri”

“Tutahitaji miezi sita kuanzia tunapotoa oda mpaka mabasi yaje, tutafanya maongezi na NMB kesho tutajua lini mabasi yatakuwa yanafika, najua nitamuachia Mkurugenzi Mkuu wa UDART na Bodi yake kuisema kwa Umma lakini kazi yetu ni kuhakikisha wanapata pesa”

Millard Ayo

Serikali haijawahi kufanya biashara kwa ufanisi, Hayo mabasi hata yakiletwa elfu 10 yatafanyiwa ufisadi mpaka kampuni itakufa, rejea zilivyokufa kampuni za magari za mikoa kwa nini msiwaachie sekta binafsi? Kwa kweli viongozi wetu mnakera sana kwa sababu mwisho wa siku tutakaolipa haya madeni ni sisi wananchi kupitia kodi
 
Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu, amesema katika jitihada za kuboresha uendeshaji wa mabasi ya mwendokasi benki ya NMB imekubali kutoa mkopo kwa Serikali ambayo inamiliki kampuni ya UDART kwa 85% ili kuongeza mabasi zaidi ya 100 ya mwendokasi.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo July 15,2024 katika Mkutano wa Msajili wa Hazina na Wahariri wa Vyombo vya habari, Mchechu amenukuliwa akisema “UDART sasa hivi ni kampuni inayomilikiwa 85% na Serikali, ilipoanza ilikuwa inaendeshwa na Sekta binafsi Serikali ilikuwa na mchango mdogo, tukajikuta ina madeni mengi, mabasi yake ndio hivyo, kwa miezi miwili nimekuwa nafanya vikao na DART kampuni inayosimamia miundombinu, na UDART inasimamia uendeshaji na mabasi”

“Tunaenda kuongeza idadi ya mabasi na kesho nina kikao na benki ya NMB ambayo ndio wanatukopesha, tutakuwa na kikao pale NMB na UDART, DART, LATRA kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa fedha wa kupata mabasi yasiyopungua mabasi 100 ambayo yataweza kutusaidia”

“La pili kwa hatua tuliyofikia tunahitaji kampuni zaidi ya tano au sita, sio kampuni moja tu ambayo siku wakigoma au kupata matatizo Mji wote umesimama, unapokuwa na Waendeshaji wengi pia ni rahisi kujua nani anatoa huduma nzuri”

“Tutahitaji miezi sita kuanzia tunapotoa oda mpaka mabasi yaje, tutafanya maongezi na NMB kesho tutajua lini mabasi yatakuwa yanafika, najua nitamuachia Mkurugenzi Mkuu wa UDART na Bodi yake kuisema kwa Umma lakini kazi yetu ni kuhakikisha wanapata pesa”

Millard Ayo

Kule Kwa Wajomba hatukopesheki tena!??

NMB wajiandae kutukopesha na mishahara ya Watumishi wa Umma. Ndo anguko la NMB hilo
 
Mabasi ya mwendokasi wanakopa ila maV8 ya kutembelea wao hawakopi.. Shubastad..

Na je wana uhakika haya yaliyopo hayatoshi, kama mara 2 hivi nishakuwepo kituo cha mwendokasi pale feri, linakuja basi, linashusha watu linapaki, jingine linakuwa tupu, linaondoka likiwa tupu, jingine linashusha kisha linapaki, haji mpaka mjazane, yaani upite muda fulani ndio aje, haijalishi mko wengi kiasi gani.. Kabla ya mabasi mapya kwanza watizame waendeshaji wana akili humo vichwanj mwao!??
Sahihi broo Kwanza magari yaliyopo yanafanya kaz ipasavyo then waongeze, alafu kukopa pesa V8 zao mbona hazna production yyte na zina bajeti husika inamana swala la mabasi lenye kuleta faida ndo Hadi wakope?
 
Turudi kwenye hoja/mada husika

Sisi Bado Sana yaan ni lini tunaweza kujisimamia humu Jf naona Kuna watu wazuri humu wenye mawazo chanya mama Samia wa spot Hawa vijana wakabidhiwe mwendokasi tuondoke kwenye huu mkwamo..

TANZANIA 😊
 
Sahihi broo Kwanza magari yaliyopo yanafanya kaz ipasavyo then waongeze, alafu kukopa pesa V8 zao mbona hazna production yyte na zina bajeti husika inamana swala la mabasi lenye kuleta faida ndo Hadi wakope?
Hapo kwenye mkopo na kuagiza basi mpya tunaenda kupigwa na kitu kizito, gari ya milioni 100 mtumba, watatwambia ni milioni 500
 
Wananununua mabasi mengine ya nini wakati kampuni ameshapewa mwarabu?
Yale yale mambo ya bandari serikali imewekeza mtaji mkubwa hata kabla haijaanza kurudisha kapewa mwarabu.
 
Kwa nini hayo mabasi wasiyabinafsishe tu kwa sekta binafsi, halafu hiyo serikali ikajikita kwenye ukusanyaji wa kodi na pia kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji!
Halafu meneja atakula nini? Ila umeongea point ya maana basi tu ni tumbo kwanza.
 
Back
Top Bottom