Serikali kukopa Fedha NMB kwaajili ya kununua Mabasi 100 ya Mwendokasi

Serikali kukopa Fedha NMB kwaajili ya kununua Mabasi 100 ya Mwendokasi

Mwendokasi ni mpango wa kuifilisi nchi. Kwa nini wasingejenga city tram zikatumia umeme?
 
Mchechu ni husiness minded bravo, hawa wanatakiwa wapewe mabasi ya mkopo ili wawe na ari ya kutoa huduma nzuri na efficient kwani kuna machungu ya marejesho,hii mambo serikali inafanya uwekezaji mkubwa wa miundombinu bado iwape mtaji,bado vitendea kazi , ndio inaleta inefficiency na taasisi kufanya kazi buziness as usual, na ndio maana mashirika mengi yana kila kitu ila yanatengeneza hasara kwakuwa hakuna anayeumiza kichwa, ruzuku itakuja 😡😡
Hee huu ndo ujinga, kama hawana hali ya kutoa huduma nzuri si wawatoe?
Wasipokua na hio ari baada ya mkopo nani atalipa?

Au na wewe ni mnufaika ndo mana?
 
Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu, amesema katika jitihada za kuboresha uendeshaji wa mabasi ya mwendokasi benki ya NMB imekubali kutoa mkopo kwa Serikali ambayo inamiliki kampuni ya UDART kwa 85% ili kuongeza mabasi zaidi ya 100 ya mwendokasi.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo July 15,2024 katika Mkutano wa Msajili wa Hazina na Wahariri wa Vyombo vya habari, Mchechu amenukuliwa akisema “UDART sasa hivi ni kampuni inayomilikiwa 85% na Serikali, ilipoanza ilikuwa inaendeshwa na Sekta binafsi Serikali ilikuwa na mchango mdogo, tukajikuta ina madeni mengi, mabasi yake ndio hivyo, kwa miezi miwili nimekuwa nafanya vikao na DART kampuni inayosimamia miundombinu, na UDART inasimamia uendeshaji na mabasi”

“Tunaenda kuongeza idadi ya mabasi na kesho nina kikao na benki ya NMB ambayo ndio wanatukopesha, tutakuwa na kikao pale NMB na UDART, DART, LATRA kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa fedha wa kupata mabasi yasiyopungua mabasi 100 ambayo yataweza kutusaidia”

“La pili kwa hatua tuliyofikia tunahitaji kampuni zaidi ya tano au sita, sio kampuni moja tu ambayo siku wakigoma au kupata matatizo Mji wote umesimama, unapokuwa na Waendeshaji wengi pia ni rahisi kujua nani anatoa huduma nzuri”

“Tutahitaji miezi sita kuanzia tunapotoa oda mpaka mabasi yaje, tutafanya maongezi na NMB kesho tutajua lini mabasi yatakuwa yanafika, najua nitamuachia Mkurugenzi Mkuu wa UDART na Bodi yake kuisema kwa Umma lakini kazi yetu ni kuhakikisha wanapata pesa”

Millard Ayo

Huyu jamaa anapenda kukopa balaa
 
Serikali imejenge miundombinu, ikope hela kununulia mabasi kisha imkabidhi mwarabu kuyaendesha, akili matope hizi zinapatikana Tanganyika tu.
 
Tanzania wakubali tu mfumo wa SOEs (State Owned Enterprises) hawauwezi ni hasara tupu kila mahali

Serikali ya Tanzania haina ubunifu kwenye biashara ina speed ya trekta

Nikiangalia jinsi akina Abood, Shabiby, B.M n.k wanavyoweza kumanage biashara ya usafiri huwa nashindwa kuelewa kwa nini serikali huwa haitaki kuwashirikisha hawa wadau kwenye kutoa huduma

DART na UDART ni vitengo vya upigaji tu
 
kwenye kukopa tuko vizuri

kuendesha na kusimamia mradi
Ndiyo sifuri.....

Ova
 
Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu, amesema katika jitihada za kuboresha uendeshaji wa mabasi ya mwendokasi benki ya NMB imekubali kutoa mkopo kwa Serikali ambayo inamiliki kampuni ya UDART kwa 85% ili kuongeza mabasi zaidi ya 100 ya mwendokasi.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo July 15,2024 katika Mkutano wa Msajili wa Hazina na Wahariri wa Vyombo vya habari, Mchechu amenukuliwa akisema “UDART sasa hivi ni kampuni inayomilikiwa 85% na Serikali, ilipoanza ilikuwa inaendeshwa na Sekta binafsi Serikali ilikuwa na mchango mdogo, tukajikuta ina madeni mengi, mabasi yake ndio hivyo, kwa miezi miwili nimekuwa nafanya vikao na DART kampuni inayosimamia miundombinu, na UDART inasimamia uendeshaji na mabasi”

“Tunaenda kuongeza idadi ya mabasi na kesho nina kikao na benki ya NMB ambayo ndio wanatukopesha, tutakuwa na kikao pale NMB na UDART, DART, LATRA kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa fedha wa kupata mabasi yasiyopungua mabasi 100 ambayo yataweza kutusaidia”

“La pili kwa hatua tuliyofikia tunahitaji kampuni zaidi ya tano au sita, sio kampuni moja tu ambayo siku wakigoma au kupata matatizo Mji wote umesimama, unapokuwa na Waendeshaji wengi pia ni rahisi kujua nani anatoa huduma nzuri”

“Tutahitaji miezi sita kuanzia tunapotoa oda mpaka mabasi yaje, tutafanya maongezi na NMB kesho tutajua lini mabasi yatakuwa yanafika, najua nitamuachia Mkurugenzi Mkuu wa UDART na Bodi yake kuisema kwa Umma lakini kazi yetu ni kuhakikisha wanapata pesa”

Millard Ayo

Tuseme tu ukweli mali za serikali hamtunzi kabisa mnaingiza walipa kodi hasara kama nimadaladala yenu yanafanya kazi hata miaka 10 barabarani na hela manaingiza lakinj inakua vipi likija mali ya umma linahujumiwa na hakuna anaechukuliwa hatua wala kuwajibishwa hata mkikopa kwa utaratibu huu wakutotunza ni hasara kwa walipa kodi maskini
 
Serikali iache kufanya biashara, serikali ijenge miundombinu iwaite private sector tendering operators hata wa tatu na serikali irudishe gharama kwa kucharge hizi kampuni huku ikiboresha na ku maintain miundombinu. Hata SGR nilitoa ushauri serikali ikusanye tu fees isiingie kwenye issue ya kuendesha haya mashirika yalishakufa unawapa tena mtaji watauwa tena. Itafute njia ya kurudisha gharama sio tena kutoa mitaji na gharama za uendeshaji.

TRC na SGR mpaka leo sijui nini kipya wanacho ili isitokee yaliyotokea kwa Railway ya kati ya zamani. Ila nimesikia kuwa watakaribisha serikali hata private sector kutumia SGR kwa malipo na hili ni sawa na huduma za usafiri waachie private.
 
Mmmmmmmmmh 🤔 mabasi 100 wanataka mkopo sasa fedha zote zinazo kusanywa kwenye mradi tangu umeanzishwa zinakwenda wapi 🤔 wana gawana zote hakuna za kuendeshea mradi zinazobaki🤔 sasa ni kipi hii serikali inafanya kwa fedha zake unazo kusanya 🤔
 
Halafu baadaye kidogo watauziwa Waarab!
Tuliambiwa Kuna mwarabu mdubai amepatikana kuwa mbia.
Tukaambiwa Kuna mabasi yanashuka bandarini Mara gear imebadilishwa angani, tunakopa NMB.
Uganda wanatengeneza mabasi yasiyo tumia dizeli. Kwanini tusiagize kwa jirani? Au m7 amegoma kutoa Cha juu ?
Mimi naona atafutwe MTU mwenye daladala zaidi ya kumi apewe aendeshe huu mradi. Mtakuja kunishukuru.
Lakini kwa hizi PhD za kina Mhede & co. Hatufiki mbali.
 
Tungekuwa na mkuu wa isanga mwenye uchungu na nchi yake asingekubali huu upumbavu, bahati mbaya ni mwendelezo wa "mkayatizame"
 
Tuliambiwa Kuna mwarabu mdubai amepatikana kuwa mbia.
Tukaambiwa Kuna mabasi yanashuka bandarini Mara gear imebadilishwa angani, tunakopa NMB.
Uganda wanatengeneza mabasi yasiyo tumia dizeli. Kwanini tusiagize kwa jirani? Au m7 amegoma kutoa Cha juu ?
Mimi naona atafutwe MTU mwenye daladala zaidi ya kumi apewe aendeshe huu mradi. Mtakuja kunishukuru.
Lakini kwa hizi PhD za kina Mhede & co. Hatufiki mbali.
Tukishanunua ndio tutamkodisha
 
hizo kampuni zaidi ya tano/sita anazosema huyu fisadi mchechu kuwa zinahitajika kuendesha mradi zenyewe zinakuja na kitu gani? kwanini zisinunue hayo mabasi 100? Yani miundombinu na mabasi inanunua serikali tena kwa pesa ya kukopa itakayolipwa na walipa kodi masikini halafu hao wanaoitwa wawekezaji ambao ni hawahawa mafisadi watajipa hilo shavu kwa mgongo wa kampuni hewa au majina feki waje tu kukusanya pesa?
Huyu ameiba sana pesa za umma na kuanzisha kampuni yake inajenga nyumba binafsi kama NHC inaitwa Venny company, huyu ni FISADI
 
Back
Top Bottom