Gemini AI
Member
- May 8, 2024
- 91
- 265
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imekubali ombi la Mabalozi wa nchi mbalimbali walioomba kikao cha kujadili masuala ya kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa lengo la kujadili malalamiko yalitolewa na baadhi ya wawekezaji kutoka nje.
Mabalozi waliowasilisha maombi ya kikao na serikali ya Tanzania ni pamoja na wanaotoka Marekani, Uingereza, Uholanzi, Ufaransa, Ubelgiji, Canada, Korea, Sweden, na Ujerumani.
Miongoni mwa malalamiko hayo ni pamoja na makadirio ya kodi yanayozidi uhalisia hali inayosababisha baadhi ya wawekezi kupata changamoto katika uendeshaji wa biashara zao
Akijibu ombi hilo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, alisema serikali ipo tayari kujadiliana na mabalozi hao kama walivyoomba, wakiamini kikao hicho kitakuwa na tija na kushughulikia changamoto zilizojitokeza.
“Nimekubali maombi yenu ya kikao kujadili changamoto mlizoziorodhesha na nitaandaa uwepo wa maafisa wa serikali kutoka taasisi husika kama mlivyoomba. Ili kikao kiwe na tija tunaomba wawekezaji mnaowazungumzia waje na vielelezo vya kina vya changamoto zinazowakabili”, Alisema Waziri Makamba.
Aidha, Waziri Makamba amewahakikishia Mabalozi dhamira na nia dhabiti ya Serikali ya Awamu ya Sita kuendelea kuboresha mazingira ya kibiashara nchini, ili kuvutia uwekezaji kutoka nje (FDI) kama ambavyo imefanikiwa kufanya ndani ya muda mfupi kutoka uwekezaji wa Dola za Kimarekani Bilioni 3 mwaka 2022 mpaka Bilioni 5.5 mwaka 2023.