Serikali kuondoa udhibiti wa sukari kutoka nje kisheria. Bashe adai anaenda kuwatikisa 'Big Boys'

Asitafutwe mchawi, ni sera mbovu za serikali ya CCM katika masuala ya kiuchumi na kibiashara. Asitishie kivuli cha ruhani asiyekuwepo ambaye amebatizwa jina la kiruhani Big Boys, CCM itazidi kuaibika
Kunaweza kuwa na ka ukweli hapa, kwamba Big Boys asiyekuwepo anatwishwa gunia la misumari kumbe mchawi dola, hakuna dolare za kuagiza sukari nje!
 

Magafuli anaingi madarakani situation kama hii ilitokea, hatua aliyochukua ni pamoja na msako kwa wanaoficha sukari. Yeye anashindwa nn kuchukua hio hatua wakt akisubir hilo la bunge
 
Magafuli anaingi madarakani situation kama hii ilitokea, hatua aliyochukua ni pamoja na msako kwa wanaoficha sukari. Yeye anashindwa nn kuchukua hio hatua wakt akisubir hilo la bunge
Magufuli alikuwa mshamba asiyeelewa uchumi na hiyo solution yake ilikuwa ya kishamba. Huyu ndiye aliyeingusha biashara ya korosho akaiharibu, alitaka wanajeshi wabangue korosho hata kwa meno. Ujinga mtupu.

Magufuli alikuwa kama mtu mwenye nyundo ambaye tatizo lolote anaona kulitatua ni kulipiga nyundo.

Nakwambia hivi, serikali haiwezi kutatua suala la bei kwa kutumia nguvu, serikali inatakiwa kutumia akili zaidi ya nguvu.

Magufuli alikuwa anatumia nguvu zaidi ya akili.

Kutumia nguvu zaidi ya akili ndiyo hizo habari za msako wa walanguzi. Hizo habari tumezifanya tangu enzi za Sokoine na hazijawahi kufanikiwa. Ni maigizo ya kuchota akili watu wajinga wasioelewa uchumi tu.

Kutumia akili zaidi ya nguvu ni kuziachia nguvu za supply and demand zipange bei zenyewe, kwa fair competition.

Hiki ndicho Bashe anasema anaenda kufanya.
 
Wakafie mbele huko. Kama ni syndicate ya kututesa wananchi kwa kulangua sukari acha ife tu. Tunduma sukari ni 2500/- lakini ukifika Mbeya mjini ni 4800. Kwa nini watu wateseke? Wafungue mipaka sukari ya Zambia na Malawi ije kwa wingi bei zishuke.
Kabisa kama taifa limeshindwa kufanya biashara fulani waachie wengine wafanye kwa manufaa ya wananchi. Wao wanachojua ni kuvizia tu pale festoni na TRA wao na kukamata watu na bidhaa za nchi jirani hawajiulizi ni kwa nini wananchi wananunua hizo bidhaa ilihali na sisi tunazo.
 
Kwahiyo anasema hadharani hayo ili kuwatisha wenye viwanda ili wamwone au waongeze dau, kwa maana ya kwann asichukue hatua at first place ili wakilalamika yy ndiyo aje na haya majibu?
Na kwa kuwa ameshasema hadharani ni lazima aliyoyasema yaonekane yametendeka !
Short of that watu hawataacha speculations za kwamba money speaks every language !!
🙏🙏
 
Blah blah za Bashe hizo. Mnatengeneza tatizo ili mpate pa kupigia kwa kuanzisha kiwanda na shamba la Miwa kule Kilolo Iringa. Mlifanya hivyo kwenye mbolea mkaanzisha ITRACOM na Bi. Tozo sasa mnapambama ili muanzishe mashamba na kiwanda chenu cha sukari.

Wacha janja Janja, Iwezeshe kwanza TFC ili yule Mshote aache kuwadanganya wakulima.
 
makampuni mengi nchi hii ni makanjanja, hawana hata aibu. Wanaihujumu serikali, hawabebeki. Acha soko huria ifanye kazi. Ndio maana matajiri wa nchi hii wanachukiwa sana na wananchi na walifurahia kipindi MAgu anawashughulikia. Hawana utu wala ubinadamu. Sijui ni kwa kuwa utajiri wao mwingi ni wa shirki? Wana roho mbaya kuliko shetani, ndio maana Magu aliwaambia wataishi km mashetani. Wanajilimbikizia mali ya dhuluma wakati wanaziacha hapa duniani. Washenzi kabisa, wafungiwe hizo biashara zao nao waje kuishi km mashetani
 
Kwa umeme huu watashindana vipi bila kuwabeba labda waambiwe wafunge viwanda! Au serikali ipunguze makodi tuu!
 
Ame admit kuna 'monopoly'.

Ni hatari.

Kweli usalama wa nchi unaweza kua vibindoni mwa watu wachache. Duh
Ame admit kuna 'monopoly'.

Ni hatari.

Kweli usalama wa nchi unaweza kua vibindoni mwa watu wachache. Duh
Well iko hivi kwa muda mrefu, just tu imefumbiwa macho, ila wafanya biashara wanalifahamu hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…