Tetesi: Serikali kupeleka bungeni muswada wa Sheria juu ya chama cha siasa kujitoa kwenye uchaguzi

Hukumuelewa,Yaani ukitopiga kura unapigwa fain.Kwa kuwa kupiga kura ni jambo la lazima kwa raia mfano huko Australia. Lakini tanzania si lazima kwa raia kupiga kura,bado ni hiari tuu.
We wailete huku waone tutakavyochinja, YAANI unilazimishe nije kupiga kula, well nitakuja lakini nakupigia NO. NACHAGUE MWINGINE. hiyo sidhani kama wataleta.
 
Hiyo sheria ikipita ningefurahi maanake tungebaki na CCM tu .Raha raha kwenda mbele stress hakuna.Mkuu anakaa ikulu anachagua anavyotaka.Tena waweke na mtu akijitoa ashtakiwe tu kwani kuna shida tuna ishi kisoviety
 
Hii ni dhahiri kuwa hichi kikundi cha majambazi hakishindwi kubadili katiba, Jiwe atawale mpaka achoke mwenyewe.
Hatutaki kuona nchi yetu ikiingizwa kwenye machafuko au rais wetu kipenzi kuondolewa madarakali kwa aibu na kwa njia zisizo za kidemokrasia kama ilivyotokea kuwa
Jacob Zuma na Robert Gabriel Mugabe.
Yaliyotokea Zimbabwe na Afrika Kusini ni historia. Historia inafunza kwa kurejerea yaliyomfika binadamu huyu siku za nyuma.
Watu wajinga wanadhani vurugu huletwa na vyama vya upinzani. CCM na serikali yake wakidhoofisha na wakifuta upinzani nchini wapambana wenyewe kwa wenyewe. Rejereeni hiyo mifano niliyotoa. Pale wapinzani wanapoamua liwe na liwalo, kinachotokea ni mapambano ya silaha kati ya pande mbili kinzani. Hapa tena wajinga watabisha kuwa hilo haliwezekani kwa sababu kuna vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Hakuna demokrasia ya kulazimishana, linapokuja suala la kulazimisha kushiriki uchaguzi maana ya demokrasia itakuwa haipo tena. Ni heri walete muswada wa kufuta demokrasia ya vyama vingi.

Vv
 
Hukumuelewa,Yaani ukitopiga kura unapigwa fain.Kwa kuwa kupiga kura ni jambo la lazima kwa raia mfano huko Australia. Lakini tanzania si lazima kwa raia kupiga kura,bado ni hiari tuu.

Nadhani wewe ndiye ambaye hujaelewa zaidi!
Hoja ni kwamba je huko wanakolazimishwa kupiga kura je wanafanya mambo ya kipuuzi kama huku kwetu?
... je hufanya visa vya kuuzima upinzani kwa kuwafanyia fitina na figisu za namna ya huku kwetu?
...je hufanya njama za kuwaengua wapinzani, eti jimbo zima wakosee fomu,au watendaji wa huko huzikimbia ofisi??
 
Waendelee kupanda upepo tu ipo siku watavuna tufani au kimbunga kisichozuilika.
 
sawa wapeleki ila kibaki chama chao tawala ndo lengo lao .vifuteni tu
 
Hata Ulaya ukibainika haujapiga kura faini ni pesa kubwa mno

Zunguka kidogo ujionee (exposure)...Kwa nchi kama Marekani, UK, Nordic countries etc. Kila mwananchi analipwa substance allowance kila Mwezi kutoka Serikalini. Wazee na Walemavu wana maeneo tengefu ambayo hujudumiwa na Serikali mpaka umauti!

Hata hivyo swala la kupiga kura ni Uhuru wa mpiga kura mwenyewe kama ulivyo uhuru wa kwenye mambo ya Ushoga na Usagaji! Sidhani kama mtu anaweza kupigwa fine kwa kutokupiga kura! Na kama hivyo ndivyo basi lazima wawajibike kwa serikali ambayo itawapatia huduma hizo nilizozitaja hapo juu! Huku kwetu utamlazimisha mtu akapige kura kwa sababu zipi za msingi?!
 
Asee... Upinzani huu huu, Ususie uchaguzi wa serikali kuu? 😂😂 Ngoja tuone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…