Serikali kurudisha tena Mswada wa Bima ya Afya kwa Wote tena bungeni kesho 01/11/2023

Serikali kurudisha tena Mswada wa Bima ya Afya kwa Wote tena bungeni kesho 01/11/2023

Hongera Rais Samia kwa kazi hii adilifu na dhamira ya dhati ya kuboresha sekta ya afya Tanzania.

Leo nitaongelea suala la bima ya Afya kwa wote.

Ikumbukwe niliwahi kuhoji swali katika mdahalo wa Urais 2015 kupitia JF na swali langu lilihoji juu ya namna viongozi tarajali wangeweza kufanyia kazi hoja ya bima ya afya ya jamii..

Hakuna mgombea yoyote au mwakilishi wake aliyeweza kujibu kwa ufasaha au aliyeenokana kuelewa.

Mhe.Rais Samia amejipambanua clearly kwamba anataka kuona suala la bima ya afya kwa wote linafikia katika suluhisho. Aliwataka wataalamu,wanasiasa na jamii kwa ujumla kuhitimisha wazo hili la mudamrefu.

Mwaka jana(kama kumbukumbu zangu zipo sawa) serikali kupitia wizara ya Afya iliwasilisha muswada bungeni ambao kwa bahati mbaya, au kutokana na poor coordination ya kisekta ama vurugu za mawazo kinzani kati ya wadau ikapelekea muswada huo kukwama.

Sasa kesho yaani tarehe 1 Novemba tunaelekea kupata fursa mpya na adhimu ambayo itaweka historia katika mfumo wa utoaji huduma za afya nchini lakini pia utaweka historia ya namna bora ya kufinance sekta adhimu ya huduma za afya nchini.

Kupitia muswada wa bima ya afya kwa wote TANZANIA itaenda kuanza kujitegemea katika sekta ya afya na hatimaye kuondokana na lile neno la KWA MSAADA WA WATU WA MAREKANI.

Chonde chonde Wabunge wetu na wataalamu msituangushe .

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Serikali kupitia Wizara ya Afya inatarajia kurejea Bungeni tena hapo kesho Novemba 1 2023 na Muswada wa Bima ya Afya kwa wote ambao ulikwama mnamo Mwezi Februari 2023 kwa hoja iliyotolewa na Bunge ya kutokuwepo kwa chanzo endelevu cha fedha kutekeleza Mpango huo.

Muswada huu ni ndoto ya Serikali ya miaka mingi ambapo Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeboresha huduma bora za afya kuanzia ngazi ya Taifa hadi ya msingi kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya karibu zaidi na maeneo yao.

"Serikali kupitia Wizara ya Afya, Wadau wa Sekta na Wataalam wengine tayari wamefanyia kazi hoja zote zilizoibuliwa na Bunge pamoja na Wadau, hata hivyo semina zimefanyika kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii kuhusu umuhimu wa Bima ya Afya kwa wote na tulipokea maoni yao na kuyafanyia kazi wananchi kesho watege macho na masikio yao Bungeni kujua nini ambacho Waziri wa Afya Mheshiwa Ummy Mwalimu atawasilisha Bungeni"
Amesema Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Afya Bw. Englibert Kayombo

Amesema kuwa kupitishwa kwa muswada huu kutawezesha kila mtanzania kuwa ndani ya Mfumo wa Bima ya Afya hatua itakayoboresha zaidi upatikanaji wa huduma za matibabu bila kuwa na kiwazo cha fedha.

"Serikali yetu ni sikivu sana na imefanyia kazi hoja zote zilizoibuliwa na Waheshimiwa Wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi hivyo yaliyomo ndani ya muswada huo yamelenga kuwasaidia wananchi kupata huduma bora za afya bila ya kikwazo cha fedha" alisema Bw. Kayombo.

Kuhusu gharama za vifurushi, Kayombo amesema kuwa mara baada ya Muswada huo kupita na kuwa Sheria, kanuni zitatungwa ili kuratibu suala la gharama za vifurushi na kusema kuwa uchambuzi utafanyika ili vifurushi viwe vya gharama nafuu na kila mwananchi aweze kuwa na bima ya afya.

Ameongeza kuwa kwa upande wa Serikali Imeshakamilisha maandalizi ya kutoa huduma kwa wananchi kupitia mfumo wa bima ya afya kwa wote ambapo imeboresha ubora wa huduma katika vituo vyake vya kutolea huduma ikiwemo upatikanaji wa Dawa, ununuzi na usimikaji wa vifaa na vifaa tiba, ajira za watumishi.

"Kwa sasa nchi yetu iko mbali sana katika utoaji wa huduma, tuna vifaa vya kisasa vya uchunguzi wa magonjwa, huduma nyingi za kibingwa zinapatikana hapa hapa nchini lakini pia huduma za afya zimesogezwa sana kwa wananchi hivyo kama nchi tupo tayari kutekeleza hili, nia na uwezo wa kufanya hivyo tunao" amesema Bw. Kayombo.

View attachment 2798960
Ni mbwembwe tu, hakuna kipya wala cha maana sana.
Kama NHIF yenyewe imekaa kimchongo, CHIF ni kama imekufa inangoja kuzikwa kibudu, hiyo bima ya afya kwa wote ina kitu gani kipya?
 
Ni mbwembwe tu, hakuna kipya wala cha maana sana.
Kama NHIF yenyewe imekaa kimchongo, CHIF ni kama imekufa inangoja kuzikwa kibudu, hiyo bima ya afya kwa wote ina kitu gani kipya?
Ulifanikiwa kusoma mswaada wa zamani kabla haujarudiswa kwa serkali kufanyiwa marekebisho?

iCHF na NHIF ni vitu viwili tofauti japo kwa mwaka 2020 na kuendelea NHIF iliamua kuibeba CHF kwa baadhi ya majukumu
 
Serikali kupitia Wizara ya Afya inatarajia kurejea Bungeni tena leo Novemba 1, 2023 na Muswada wa Bima ya Afya kwa wote ambao ulikwama mnamo Mwezi Februari 2023 kwa hoja iliyotolewa na Bunge ya kutokuwepo kwa chanzo endelevu cha fedha kutekeleza Mpango huo.

Muswada huu ni ndoto ya Serikali ya miaka mingi ambapo Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeboresha huduma bora za afya kuanzia ngazi ya Taifa hadi ya msingi kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya karibu zaidi na maeneo yao.

“Serikali kupitia Wizara ya Afya, Wadau wa Sekta na Wataalam wengine tayari wamefanyia kazi hoja zote zilizoibuliwa na Bunge pamoja na Wadau, hata hivyo semina zimefanyika kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii kuhusu umuhimu wa Bima ya Afya kwa wote na tulipokea maoni yao na kuyafanyia kazi wananchi kesho watege macho na masikio yao Bungeni kujua nini ambacho Waziri wa Afya Mheshiwa Ummy Mwalimu atawasilisha Bungeni” Amesema Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Afya Bw. Englibert Kayombo

Amesema kuwa kupitishwa kwa muswada huu kutawezesha kila mtanzania kuwa ndani ya Mfumo wa Bima ya Afya hatua itakayoboresha zaidi upatikanaji wa huduma za matibabu bila kuwa na kiwazo cha fedha.

Serikali yetu ni sikivu sana na imefanyia kazi hoja zote zilizoibuliwa na Waheshimiwa Wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi hivyo yaliyomo ndani ya muswada huo yamelenga kuwasaidia wananchi kupata huduma bora za afya bila ya kikwazo cha fedha” alisema Bw. Kayombo.

Kuhusu gharama za vifurushi, Kayombo amesema kuwa mara baada ya Muswada huo kupita na kuwa Sheria, kanuni zitatungwa ili kuratibu suala ya gharama za vifurushi na kusema kuwa uchambuzi utafanyika ili vifurushi viwe vya gharama nafuu na kila mwananchi aweze kuwa na bima ya afya.

Ameongeza kuwa kwa upande wa Serikali imeshakamilisha maandalizi ya kutoa huduma kwa wananchi kupitia mfumo wa bima ya afya kwa wote ambapo imeboresha ubora wa huduma katika vituo vyake vya kutolea huduma ikiwemo upatikanaji wa Dawa, ununuzi na usimikaji wa vifaa na vifaa tiba, ajira za watumishi.

“Kwa sasa nchi yetu iko mbali sana katika utoaji wa huduma, tuna vifaa vya kisasa vya uchunguzi wa magonjwa, huduma nyingi za kibingwa zinapatikana hapa hapa nchini lakini pia huduma za afya zimesogezwa sana kwa wananchi hivyo kama nchi tupo tayari kutekeleza hili, nia na uwezo wa kufanya hivyo tunao” amesema Bw. Kayombo.View attachment 2799737View attachment 2799738
IMG-20231031-WA0015.jpg
 
Tatizo sio muswada bali ni huduma bora.

NHIF waweke madaraja mazuri ili wenye uwezo walipe zaidi ili wapate huduma bora, vinginevyo mfuko utaendelea kufa
 
Wananchi wameshindwa kuchangia elfu 30 kwa mwaka kupitia bima ya CHF na wanatibiwa wanafamilia 6. Hyo inayo kuja kwa wote itakuwa chini ya 30k?
 
E72F3A04-5BBC-4BAD-9364-2CD00471F16E.jpeg

Nimekula ban la mwezi mzima kwa sababu ya kuomba hiki kitabu ‘jukwaa la habari tena kwa lengo la kukinunua kwa tsh 50,000.

Kitabu kinachoweza kukupa uelewa wa kuchangia mada kama hizi kuelewa hao NHIF wamejipanga vipi kuzuia mirija au serikali itasimamia vipi sheria zake kuhakikisha kuna compliance kwenye aspects zake muhimu👇 kama hizo chini when it comes to auditing.

15CB51DB-F656-429D-B2F9-02374DE0ED54.jpeg

Usimamizi wa hayo mambo ni very complicated na yanayoweza kufanya insurer kupanga viwango vya juu pengine kutokana na uzembe wa kutoweza zuia upotefu mkubwa wa hela.

Je, hawa wahusika insurers wana mbinu gani kwanza za kuzuia leakage za hovyo because in enterprise risk management for lises those someone as to cover for that cost.

Ni hivi kuchangia mada kama hizi kunataka technical knowledge.

Mie nimeomba kitabu tena kwa kumlipa mtu elfu 50 vilikuwa viwili nilipe laki, tumegombana na moderator mpaka kanipiga ban ya mwezi mzima.

Halafu inakuja mada kama hii yenye Issue za msingi nilizotaka kuzijua, wachangiaji wanakwambia tatizo bunge and other nonsense; nothing to do with the risk management ya shirika na kuelewa losses zinazosababisha wapoteze hela kwa udanganyifu uliopo na mbinu wanazotumia na nitty gritty issues za insurance business.

Ignorance is a bliss

Kwa michango hii you think you gonna offer a meaning perspective to what is wrong and how best to approach the problem, without proper knowledge.

Tanzania kila kitu rahisi, just copy and paste; without the need to understand the principles.

Shida inaanzia kwenye uongozi wa NHIF if you ask me to how they control their payments (and that’s the risk which costs other contributors to pay more).

Shitty country

Halafu Mohammed Said anaachwa atangaze kitabu chake cha sijui cha Sheikh nani wala mods hawana.
 
View attachment 2799773

Nimekula ban la mwezi mzima kwa sababu ya kuomba hiki kitabu ‘jukwaa la habari tena kwa lengo la kukinunua kwa tsh 50,000.

Kitabu kinachoweza kukupa uelewa wa kuchangia mada kama hizi kuelewa hao NHIF wamejipanga kuzuia mirija au serikali itasimamia vipi sheria zake kuhakikisha kuna compliance ya sehemu za sheria zake 👇 kama hizo chini

View attachment 2799784

Usimamizi wa hayo ni very complicated kujua badala ya kupanga viwango vya juu pengine kuna upotefu mkubwa wa hela.

Je, hawa wahusika insurers wana mbinu gani kwanza za kuzuia leakage za hivyo because in enterprise risk management those someone as to cover for that cost.

Ni hivi kuchangia mada kama hizi kunataka technical knowledge.

Mie naomba kitabu tena kumlipa mtu elfu 50 vilikuwa viwili nilipe laki, tumegombana na moderator mpaka kanipiga ban ya mwezi mzima.

Halafu inakuja mada kama hii yenye Issue za msingi nilizotaka kuzijua, wachangiaji wanakwambia tatizo bunge; nothing to do with the risk management ya shirika na kuelewa losses zinazosababisha wapoteze hela kwa udanganyifu uliopo na mbinu wanazotumia kama na nitty gritty zingins za insurance kukaguliwa.

Ignorance is a bliss

Kwa michango hii you think you gonna offer a meaning perspective to what is wrong and how best to approach the problem, without proper knowledge.

Tanzania kila kitu rahisi, just copy and paste; without the need to understand the principles.

Shida inaanzia kwenye uongozi wa NHIF if you ask me to how they control their payments (and that’s the risk which costs other contributors to pay more).

Shitty country

Halafu Mohammed Said anaachwa atangaze kitabu chake sijui cha Sheikh nani wala mods hawana.
Kama ni hivyo wamefanya vibaya..
Sijui why mods nowdays wako hivyo wanaharibu jamiiforum tukiyokuwa tunaijua Ya miaka hiyo ya 2009 ,2010 ilotufanya tujiunga humu miaka hiyo
 
Yeah mkuu itasaidia angalau kila mtanzania kumudu Huduma za Afya
Huwa hii wizara inachekesha sana, wanasema kila mTanzania awe na bima ya afya lakini mtumishi wa Umma ambae wategemezi wake wanne wapo wawili akileta mtoto mtu mwingine wanamkataa kuwa siyo mnufaika wakati huohuo anakatwa pesa kwa idadi ya wategemezi wote hadi ambao hajawasilisha taarifa zao.

Shangazi hana uwezo wa kupata matibabu kutokana na kipata lakini nikipeleka taarifa zake ili awe mtegemezi wangu anakataliwa lakini kwa mlango wa nyuma wizara inapiga domo kuwa kila Mtanzania awe na bima ya afya, ujinga mtupu.
 
Kama ni hivyo wamefanya vibaya..
Sijui why mods nowdays wako hivyo wanaharibu jamiiforum tukiyokuwa tunaijua Ya miaka hiyo ya 2009 ,2010 ilotufanya tujiunga humu miaka hiyo
Sometimes unakubali tu yaishe na kuelewa, haikudhuru wewe; ni akili tu za mtu mwingine you can’t change.

That’s life
 
Huwa hii wizara inachekesha sana, wanasema kila mTanzania awe na bima ya afya lakini mtumishi wa Umma ambae wategemezi wake wanne wapo wawili akileta mtoto mtu mwingine wanamkataa kuwa siyo mnufaika wakati huohuo anakatwa pesa kwa idadi ya wategemezi wote hadi ambao hajawasilisha taarifa zao.

Shangazi hana uwezo wa kupata matibabu kutokana na kipata lakini nikipeleka taarifa zake ili awe mtegemezi wangu anakataliwa lakini kwa mlango wa nyuma wizara inapiga domo kuwa kila Mtanzania awe na bima ya afya, ujinga mtupu.
Hebu fuatilia I think kuna waraka umetoka wategemezi wameongezeka mpaka 9 so jumla Wanufaika wa bima Ya afya kwa Mtumishi wa Umma ni 10 kwa sasa..

Wahusika (Wategemezi)
  • Mke/Mume (Kisheria Awe na cheti cha ndoa)
  • Watoto wako au wa Kuasili
  • Wazazi wako (Hili la Wakwe naona limeondolewa)

Na kuhusu kuingiza mtu ambaye sio Mwanao I think kuna taratibu zake, kama Ni mtoto, Muasili (Adopt) ili Apate kigezo cha kupata huduma hiyo.

Kuhusu Shangazi I think haiwezekani sio Tanzania hata NHIF-Kenya Pia na nchi zote..
Beneficiary Wa Huduma zote za Bima wanafahamika
 
Kama haya uliyoyasema ni kweli basi nadiriki kusema ni wauaji waliouandaa hiyo waraka...Sasa kuwaondoa wakwe maana yake nini? Ni sababu gani kuongeza wategemezi hadi 9 wakati practically watumishi wenye idadi hiyo kubwa ya watoto hawapo kwa hizi siku.

Yaani Baba na Mama wote watumishi au wastaafu, mimi na mke wangu wote watumishi wa Umma...kwa maana hiyo tuna wategemezi 18.
Sasa swali ni kuwa kama ninakatwa gharama ya wategemezi 9 na tayari nimewasilisha taarifa ya wategemezi 2 inashindikana nini mimi kumleta mtegemezi yeyote kama mjomba au shangazi? Kwasababu Sera ya Wizara ya Afya ni kila mtanzania awe na bima..

Naona hawana Logic hao watunga Sera.
 
Logic Ipo mkuu,
Kulitokea malalamiko mengi Kuhusu wake, kwa wale polygmous (Ikumbukwe sheria Inaruhusu wake Wanne kwa waislamu)..
Polygamous wengi walibanwa kuhusu wake naona kwa sasa wameruhusu idadi ya wake kuongezeka..
Kwa swala la wakwe nafikiri leo litajadiliwa kama litapita basi itakuwa ndo sheria hiyo..

Mkuu hao mashangazi na wajomba kuwathibitisha kisheria ni vigumu sana hivyo kama wataruhusu bhasi watu wataingiza mamluki wengi...

Ni rahisi kuthibitisha mke (Kupitia cheti cha ndoa)
Mtoto (Kupitia vyeti vya kuzaliwa)
Mkwe (Pia nae ilikuwa Rahisi kupitia cheti cha ndoa na cheti cha kuzaliwa cha mke)
Mzazi wako (kupitia vyeti vya kuzaliwa)

Ila ni vigumu kuthibitisha mjomba,shangazi kisheria kutumia nyaraka
 
Kwani shida ni mamluki au shida ni kufikisha ile idadi ya wategemezi wako uliopewa kisheria?
 
Kwani shida ni mamluki au shida ni kufikisha ile idadi ya wategemezi wako uliopewa kisheria?
Umenena Vizuri na Lengo hasa la Bima ya Afya ni kuhakikisha wale wote (Wategemezi Wote) ambao wameainishwa kisheria wanapata Huduma kwa idadi iliyotajwa na kwa sifa zao bila kuingiza watu wasiohitajika au kutambuliwa kisheria..

Kufanya hivyo (Kuingiza watu wasiotambulika Kisheria) huhesabiwa kama kuhujumu Taasisi na ni kosa la jinai mkuu...
Sio tu kuingiza watu wafike idadi bali watu sahihi kwa idadi sahihi..
 
Back
Top Bottom