Serikali kutoa ruzuku ya bilioni 100 kunusuru bei ya mafuta. Yaomba mkopo IMF na Benki ya Dunia

Serikali kutoa ruzuku ya bilioni 100 kunusuru bei ya mafuta. Yaomba mkopo IMF na Benki ya Dunia

Kila kitu tunakopa sasa, mpaka hela ya sensa tunakopa, baadae itakuwaje.

Mungu tupo mikononi mwako naomba utunusuru.
 
Mtumishi afanye Kazi ya umma afu alipie 30% ya pesa zake kufanya Kazi ya umma? Kuwa serious basi hata kama ni mjinga.
Mtumishi anapewa gari, nyumba na dereva; Muda mwingi gari la umma linafanya kazi zake, haya magari ndiyo tunayokutana nayo maada ya masaa ya kazi - NDIYO wachangie 30% ya mafuta - kama uchungu wote tuuone - na hii ni kuzazia Rais mwenyewe hadi Mtendaji wa kitongoji.

Ni lazima tuugawane pamoja umaskini wetu - hamna namna nyingine ndugu, usihamaki tunakwenda taratibu kutatua hili tatizo la mfumko wa bei - ni lazima tubane matumizi.
 
wauze mavi-8 yote ya wakurugenzi na madc pesa zielekezwe kwenye kupunguza gharama ya mafuta pia mikutano mingi ifanywe online na sio kwenye mihotel ya nyota 5
Ukitaka kuwaudhi wewe gusia hayo ma V8 yao, yaani unakuta wameweka vichoka full AC, kuwaambia wachangie walau 30% ya mafuta ya gari kwa mwezi - wanan'gaka hao balaaaa.
 
Bunge litaendelea na vikao vyake leo na kubwa linalotarajiwa kutokea ni mrejesho wa hatua ambazo Serikali inatarajiwa kuchukua kukabiliana na kupanda kwa kasi bei za mafuta kunakotajwa kusababishwa na vita ya Urusi na Ukraine. Hali hiyo ilipelekea ongezeko la nauli kwenye daladala ambalo mara ya mwisho zilipanda Aprili 12, 2013.

May 5 mwaka huu spika wa Bunge, Tulia Ackson alimpa waziri Makamba siku tano kuja na ufafanuzi kutoka kwa Serikali juu ya hatua za dharura ambazo Serikali inatarajia kuchukua. Kwenye kikao hicho wabunge wengi walipendekeza baadhi ya tozo ziondoke kushusha bei ya mafuta au Serikali ikope ili kuipa ruzuku sekta ya mafuta.

Kujielimisha zaidi, soma:
=> Bungeni: Mjadala wa dharura kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta nchini. Mbunge asema tozo mbili zinaongeza 792 kwenye bei

=> Rais Samia atangaza neema punguzo ya bei za mafuta kuanzia Juni 1, 2022

Kaa nami

======

Makamba:- Rais Samia amesononeka na kupanda mafuta na bidhaa
Waziri Makamba: Rais Samia alituweka kitako usiku mkubwa akasema mengi kwa uchungu mkubwa, akaonesha masononeko. Alielezea kugusa kwake na kusononeka kwake juu ya kupanda kwa gharama za mafuta nchini na gharama za bidhaa mbalimbali.

Akasema hata kama bei ya mafuta duniani iko juu, hata kama takwimu na namba zinaleta mantiki lakini tutangulize utu na huruma kwanza katika kulishughulikia jambo hili.

Hatuzalishi hivyo wahanga wa bei
Nchi yetu haina visima vya mafuta wala mashine za kuchakata mafuta ghafi, sisi ni wapokeaji wa bei kwa maana wahanga wa bei.

Mwezi Oktoba 2021 Serikali ilichukua hatua ya kupunguza tozo zifuatazo
  1. Tozo ya miundombinu ya bandari iliyokuwa inalipwa kwa mamlaka ya bandari.
  2. Tozo ya kuchakata nyaraka za forodha(Customs processing fee) inayolipwa TRA
  3. Tozo ya kupima na kuthibitisha viwango vya mafuta nchini iliyokuwa inalipwa kwa wakala wa vipimo Tanzania(WMA)
  4. Serikali ilipunguza tozo ya kupima na kuthibitisha ubora wa mafuta iliyokuwa inalipwa kwa TBS
  5. Ilipunguza tozo ya wakala wa meli inayolipwa kwa shirika la wakala wa meli(TASAC)
  6. Ilipunguza tozo ya udhibiti ya biashara ya mafuta iliyokuwa inalipwa kwa Ewura.
Makamba: Katika mjadala wa mafuta kumekuwepo kulinganisha bei za mafuta za nchi yetu. Kulinganisha bei lazima kuendane na kulinganisha kila kitu kinachoingia katika bei ikiwemo viwango vya kodi na tozo.

Sisi kama nchi tumeweka kodi ya zaidi ya shilingi 900 kwenye kila lita ya petroli.

MKOPO KUTOKA IMF NA WB
Makamba:
Serikali ilianza taratibu za kuchukua mkopo wenye masharti nafuu kutoka benki ya dunia na shirika la fedha duniani(IMF) kwa ajili ya kuweka ahueni kwenye bei za mafuta na bidhaa nyinginezo.

Mchakato wa kuchukua mkopo huu uko mbioni kukamilika na ahueni ya kupanda kwa bei ya mafuta na bidhaa mbalimbali itapatikana kutokana na mkopo huu katika mwaka ujao wa fedha.

RUZUKU
Makamba:
Hata hivyo kutokana na mahitaji ya wananchi na mapendekezo ya wabunge, mheshimiwa Rais alitoa maelekezo kwamba mwaka ujao wa fedha ni mbali kusubiri ahueni hiyo na akaelekeza kwamba ahueni itafutwe haraka zaidi.

Katika kipindi hiki kabla hatujafikia mwaka mpya wa fedha, Serikali ijibane, ijinyime na zitolewe Tshs bilioni 100 kwaajili ya kupunguza bei za mafuta hapa nchini.

Kwahiyo Serikali imeamua kutoa bilioni 100 sasa kwaajili ya kutoa ahueni kwaajili ya mafuta. Ruzuku hii inatolewa kwa kupunguza matumizi ya Serikali katika kipindi kilichobaki katika mwaka huu wa fedha.

Kutolewa kwa ruzuku hii hakutagusa miradi ya maendeleo ambayo inaendelea. Nafuu ya bilioni 100 ni nafuu ya kipindi cha mpito kuelekea kwenye mwaka mpya wa fedha ambapo nafuu nyingine inayotokana na mikopo niliyoelezea awali itakuja kwenye mwaka ujao wa fedha na itaelezwa kwa kina zaidi na waziri wa fedha katika bajeti ya Serikali ya mwezi ujao.

Ruzuku itatolewa kupunguza bei za mafuta kuanzia Juni 1. Hii inatokana na kuwa, wafanyabiashara kwa mfumo wa biashara ya mafuta, wafanyabiashara wa jumla wameshalipia ya mafuta ambayo imejumuishwa kwenye bei na wafanyabiashara wa mafuta kwenye vituo wameshanunua mafuta kwa bei inayotumika sasa.

KWA UFUPI HATUA ZILIZOCHUKULIWA
1. Serikali imetoa ruzuku ya shilingi bilioni 100, ili kutoa ahueni ya bei ya mafuta kwa wananchi kuanzia 1, June 2022.

2. Kuruhusu watu wa kuingiza mafuta kwa bei nafuu kuanza mafuta na gharama itapungua Agosti 2022

3. Kuanzishwa kwa mfuko wa kukabiliana na mfumuko wa bei ya mafuta (Fuel prices stabilization fund)

4. Kuanzisha utaratibu wa kuhifadhi mafuta ya kimkakati.

5. Kujenga maghala makubwa ya kuhifadhi mafuta kwa ajili ya kuuza ndani na nje ya nchi.

6. Kuanza upokeaji wa mafuta katika ghala moja (single receiving terminal), ili kupunguza muda wa meli kusubiri pindi inapoleta mafuta ambapo nayo ilikuwa sababu ya kupanda kwa gharama za bei ya mafuta.

7. Kuongezewa uwezo wa taasisi ya TPDC ili kufanya biashara ya mafuta.

8. Kuboresha utendaji kazi wa taasisi zinazojihusisha na masuala ya mafuta ikiwemo Ewura.
Serikali yote imeshindwa kazi IJIUZULU tuanze upya
 
Mtumishi anapewa gari, nyumba na dereva; Muda mwingi gari la umma linafanya kazi zake, haya magari ndiyo tunayokutana nayo maada ya masaa ya kazi - NDIYO wachangie 30% ya mafuta - kama uchungu wote tuuone - na hii ni kuzazia Rais mwenyewe hadi Mtendaji wa kitongoji.

Ni lazima tuugawane pamoja umaskini wetu - hamna namna nyingine ndugu, usihamaki tunakwenda taratibu kutatua hili tatizo la mfumko wa bei - ni lazima tubane matumizi.
Wapi uliwahi ona kwamba muda mwingi gari ya ofisi inafanya Kazi binafsi?
 
Kuhamishia tozo kwenye bidhaa nyingine ndio hakuleti inflation? Je kutatuhakikishia pesa ya barabara?
Kwahiyo Bei za vifurushi zikipanda itapelekea bei zingine kupaa?? Au Kodi ikiongezwa kwenye export levy ya korosho bidhaa zingine zitapanda bei?? Huwezi linganisha spillover effect ya Nishati yoyote kwa service zingine kma mawasiliano au utali n.k

umekariri tozo,tozo wakati pale kuna excise duty kubwa kuliko hizo zingine zote.
Nmeongelea sababu umegusia Miradi na wote tunafahamu hizo tozo nilizotaja zipo specific zinaenda wapi sio kama hizo excise duty ambazo mwisho wa siku zinaenda hazina kupangiwa matumizi!!!

Wewe uko nje wenzio tuko ndani,kufanya hayo unavyosema itategemeana na mwenendo wa Uchumi na yanafanyika hatua kwa hatua..
Ndio muwe wabunifu sasa, hatua kwa hatua wakati ni crisis hamsaidii kitu. Tatizo hapa currency yetu itashuka thamani maana purchasing power ya shillingi moja inaporomoka relative to dollar. Exports zitakua gharama tutacompete wapi? Imports nazo zitakua bei juu maana you'll get less products with a shilling today than last year!! Hayo yakitokea hata mkikusanya Bado say trillion 1 kutoka kwenye mafuta tu mtakuta karibu 200Bn imekufa thamani which in turn mngeweza ihamisha mapema kuokoa dhahama huko mbele ya kushuka kwa thamani ya shillingi na Mfumuko wa bei, interest rates zitapaa pia sababu wakopaji watakua wengi kukidhi liquidity n.k.
 
Bil 100 nimeichukua kama ilivyo nimeingawanya kwa kila mtanzania kwa kuchukulia kwamba tupo 60m.

JIBU kila mtanzania amepata ahueni ya bei kupanda kwa Tshs. 1,666.

Huu ni utani.
 
Kwahiyo Bei za vifurushi zikipanda itapelekea bei zingine kupaa?? Au Kodi ikiongezwa kwenye export levy ya korosho bidhaa zingine zitapanda bei?? Huwezi linganisha spillover effect ya Nishati yoyote kwa service zingine kma mawasiliano au utali n.k

Nmeongelea sababu umegusia Miradi na wote tunafahamu hizo tozo nilizotaja zipo specific zinaenda wapi sio kama hizo excise duty ambazo mwisho wa siku zinaenda hazina kupangiwa matumizi!!!

Ndio muwe wabunifu sasa, hatua kwa hatua wakati ni crisis hamsaidii kitu. Tatizo hapa currency yetu itashuka thamani maana purchasing power ya shillingi moja inaporomoka relative to dollar. Exports zitakua gharama tutacompete wapi? Imports nazo zitakua bei juu maana you'll get less products with a shilling today than last year!! Hayo yakitokea hata mkikusanya Bado say trillion 1 kutoka kwenye mafuta tu mtakuta karibu 200Bn imekufa thamani which in turn mngeweza ihamisha mapema kuokoa dhahama huko mbele ya kushuka kwa thamani ya shillingi na Mfumuko wa bei, interest rates zitapaa pia sababu wakopaji watakua wengi kukidhi liquidity n.k.
Kwenye vifurushi tayari kuna tozo ya maji na Tarura ,huwezi ongeza tena na ni huduma yenye substitute nyinginna very elastic so haitaleta uhakika wa mapato
 
Bil 100 nimeichukua kama ilivyo nimeingawanya kwa kila mtanzania kwa kuchukulia kwamba tupo 60m.

JIBU kila mtanzania amepata ahueni ya bei kupanda kwa Tshs. 1,666.

Huu ni utani.
Will never happen..Tafuta consumption rate ya mafuta Kwa siku ndio utapata jibu..hiyo ni less by far kwa sh.200
 
Will never happen..Tafuta consumption rate ya mafuta Kwa siku ndio utapata jibu..hiyo ni less by far kwa sh.200
Ongezeko la bei ya mafuta limeiathiri kila kaya hapa Tanzania, kwa hiyo ni lazima tupige hesabu kwa kila mtanzania amepata ahueni gani kwa ruzuku hii ya bil 100.

Ni utani.
 
Ongezeko la bei ya mafuta limeiathiri kila kaya hapa Tanzania, kwa hiyo ni lazima tupige hesabu kwa kila mtanzania amepata ahueni gani kwa ruzuku hii ya bil 100.

Ni utani.
Unatumia mechanical methodszfine Hiyo 1650 yako ni ruzuku ya muda Gani? Igawe Kwa mwezi na siku 😜😜
 
Unatumia mechanical methodszfine Hiyo 1650 yako ni ruzuku ya muda Gani? Igawe Kwa mwezi na siku 😜😜
Bil 100 imetolewa kwa mwezi June ambao una siku 30.

Sasa simple nimeigawanya kwa watu 60m nchi nzima - Jibu kila mtanzania kwa hizo siku 30 yaani 1st June hadi 30th June atapata ahueni ya Tshs 1,650.

Sasa ukitaka kupata jibu zuri zaidi chukua hiyo 1,650 gawanya kwa siku 30 ili upate ahueni ya kila mtanzania kwa siku... 1650 / 30 = centi 55 tu.

Ni utani sana huu.
 
Hata kama Rais alikosea mwanzo aliposema bei ya mafuta itapanda tujiandae, lakini kwa hii hatua aliyochukua namuunga mkono hasa ya kutoa ruzuku ya bilioni 100, we all learn from mistakes.
Kutoa hiyo fedha sioni kama kuna nia ya dhati naamini kushusha. Haya yanaigwa ila hela hii itapigwa tu. Kwa kiongozi smart tulitarajia aseme hiyo 100B itafanya nini, itapunguza nini. Zaidi hii itakuwa sehemu ya upigaji tu na maisha yataendelea. Sijaona mipango hapa zaidi ni kuongeza upigaji. Tuamke
 
Bil 100 imetolewa kwa mwezi June ambao una siku 30.

Sasa simple nimeigawanya kwa watu 60m nchi nzima - Jibu kila mtanzania kwa hizo siku 30 yaani 1st June hadi 30th June atapata ahueni ya Tshs 1,650.

Sasa ukitaka kupata jibu zuri zaidi chukua hiyo 1,650 gawanya kwa siku 30 ili upate ahueni ya kila mtanzania kwa siku... 1650 / 30 = centi 55 tu.

Ni utani sana huu.
Ndio maana nikakwambia uko too mechanical, serikali haifanyi hesabu zake kienyeji hivyo..

Iko hivi,,matumizi ya mafuta Kwa mwezi kwa Nchi Kwa bei za kabla ya kupanda ni Lita mil.400..

So 100bln/400mln Unapata sh .250/ litre kwa hiyo chukua bei ya Dar au average price less hiyo 250 .
 
Hivi kwenye gesi ya kusini hatuna chetu!? maana sioni hii serikali ikiongelea kuhusu kufanya exploitation ya gesi kama chanzo muhimu cha nishati na chanzo cha mapato ya nchi hasa tukiuza nje.....
Naona kiiiiiimya
 
Ndio maana nikakwambia uko too mechanical, serikali haifanyi hesabu zake kienyeji hivyo..

Iko hivi,,matumizi ya mafuta Kwa mwezi kwa Nchi Kwa bei za kabla ya kupanda ni Lita mil.400..

So 100bln/400mln Unapata sh .250/ litre kwa hiyo chukua bei ya Dar au average price less hiyo 250 .
Watakaokuelewa ni wachache sana, tena ambao ndiyo walewale mlikokotoa hizo bil 100 mkaona zinatufaa watu 60m kwa siku 30.

Utaniambia kama impact ya Bil 100 kwa watu mil 60 kwa wezi itaonekana....huu ni UTANI, ni bora mngeacha kabisa ili lijulikane moja.
 
Dawa hapa ni kupunguza matumizi ya kawaida ya Serikali
kwa mfano misafara yote ipunguze watu toka mia 200 na magari zaidi ya 50 wabakie watu 20 na magari chini ya 8.
Safari za nje na posho posho marufuku.

Watumishi wate wanaotumia Magari ya Umma walipie mafuta 30%.
Tulipie mafuta kufanya kazi za umma?
 
Back
Top Bottom