Serikali kutoa ruzuku ya bilioni 100 kunusuru bei ya mafuta. Yaomba mkopo IMF na Benki ya Dunia

Serikali kutoa ruzuku ya bilioni 100 kunusuru bei ya mafuta. Yaomba mkopo IMF na Benki ya Dunia

Rais anasikitishwa vipi wakati yeye ndio alikuja na kauli za kusema sisi mafuta yetu yako bei chini kuliko kwa mabeberu na lazima yapande. Yeye ndiye alikuja na kauli lazima vitu zipande bei. Wanatoa viziwi eh
Waziri anasoma hisia za bosi wake kwamba amesononeka.
Huku huwa wanasema tumesikia kelele za wananchi, huo msononeko huwa una wakati gani?
 
Na hii exchange rate ya us dola inayoendelea kuwa 2,287 ni realistic? Je inamnufaisha nani?

Kwa mfano mwaka jana exchange rate ilikuwa 2310 na bei ya mafuta ya kula (Alizeti Singida) ilikuwa shs 4,400 (lita 5 shs 22,000).

Leo mafuta hayo hayo yamekuwa shs 7,000 kwa lita. Je kuendelea kuiweka dola kwenye 2,287 kunamsaidia nani? Je mtu anayefikiria kuja kutalii inamsaidia? (Yaani all local cost in Tshs zimepanda lakini exchange rate imeshuka)
 
Mkuu wewe ni diaspora?
Gesi ya Tanzania iko kwa mume, subiri mume afe ufikiriwe ktk mirathi, Gesi si Mali yenu/ yako.

Kwa msononeko nasema,
Yule mstaafu atakufa kifo cha tabu sana na ahera atakutana na hukumu kali sana.
Acheni kelele, tunamalizia kujadiliana mkataba wa bandari ya Bagamoyo, hili la mafuta nalo litapita.
 
Tunavyohangaika utadhani sio nchi yenye utajiri wa Tanzanite, Almasi na Dhahabu...
 
Kwa mara ya kwanza namuona January Makamba akiongea huku body language ikiongea mengine tofauti kabisa!

Hivi wanamdanganya nani?
Serikali itaomba mkopo kupunguza makali alafu inatoa 100 bilioni alafu inatoza 900 kwa kila lita ya mafuta.
Screenshot_20220510-123438.png

Screenshot_20220510-123032.png
 
Rais anasikitishwa vipi wakati yeye ndio alikuja na kauli za kusema sisi mafuta yetu yako bei chini kuliko kwa mabeberu na lazima yapande. Yeye ndiye alikuja na kauli lazima vitu zipande bei. Wanatoa viziwi eh
Ila nyiee watu mtafanya watu wafanye kazi masaa 24. Hahahah
 
Huyu jamaa ni majanga kwa serikali ya Samia ni majanga makubwa sana, kweli ukipunguza bei kesho shida iko wapi? hoja yake yameshalipiwa kwa hiyo?


Kashakula pesa za stock iliopo…unataka apunguze aikose?!
 
Rais anasikitishwa vipi wakati yeye ndio alikuja na kauli za kusema sisi mafuta yetu yako bei chini kuliko kwa mabeberu na lazima yapande. Yeye ndiye alikuja na kauli lazima vitu zipande bei. Wanatoa viziwi eh
Jamani,hata Mimi alinishangazaa kwa Kauli zake.maana alihalalisha.
 
Tunahangaikia chanzo cha nishati wakati nchi ina utajiri wa gesi..........kinachompa kiburi Urusi ni nini zaidi ya gesi, akili za mtu mweusi anazijua mwenyewe......
 
"Katika mazungumzo yake kwenye kikao chetu usiku, Rais Samia alionesha kusononeshwa na kusikitishwa kwake na hata kama bei za soko la dunia ziko juu, lakini tutangulize utu na huruma na kuwajali wananchi" - January Makamba,View attachment 2218889


Leo ndio anajua kuhusu utu….

Huyu February ni kichefuchefu kwanza ni nuksi akitolewa hapo utashangaa mambo yatakuwa shwari
 
Ondoeni tozo wakati huu ambao mambo ni serious kupunguza mzigo kwa raia, na baadala yake punguzeni matumizi ya serikali kadili muwezavyo na wakati huu kuna miradi mnaweza kuacha kupump hela ikasubiri mpaka mambo yastabilize, Semina zote zifanyike online, ziara zote zikome, Wabunge posho zipunguzwe kwa muda mpaka pale mambo yatakapostabilize..
 
Kashakula pesa za stock iliopo…unataka apunguze aikose?!
Ila kuna kitu kwa hawa wabunge na wana siasa unafiki ndio sipendi, mimi ukisoma sijatetea upande mmoja kizuri nasifia kibaya kwa maoni yangu nasema. Makamba na Mwigulu ni majanga ila sijasikia hata mbunge mmoja kupendekeza kama wao watachangia nini? bunge ni gharama kubwa sana lingine jambo la muhimu kila mtu kwanini asikate gharama zisizo kuwa za lazima kama kupunguza trips kwa maana stay katika budget yako kila mtu kuwa na gari hata kwenye trip labda mnaweza kushare wewe na mwenzako kuna mambo mengi kama mtu unaweza kufanya uka balance ila hiyo haina maana serikali isifanye wajibu wake. Nimependekeza acha petrol juu punguza Diesel.
 
Back
Top Bottom