Serikali kutoa ruzuku ya bilioni 100 kunusuru bei ya mafuta. Yaomba mkopo IMF na Benki ya Dunia

Serikali kutoa ruzuku ya bilioni 100 kunusuru bei ya mafuta. Yaomba mkopo IMF na Benki ya Dunia

Kufikia hiyo June mosi tayari bei ya mafuta itakuwa kwenye 3800/l.

Wakisema waondoe kodi&tozo pekee ambayo ni kama 800/l tutakuwa tunanunua kwa 3000/l.

Hii 3000/l nayo haimalizi hata wiki ipande.

Sioni umuhimu wa vyama vya siasa kugawiana ruzuku kila mwezi na hiyo misamaha ya kodi kwa taasis za dini ifutwe.

Serikali ifute kodi yote kwenye mafuta na itie 1000/l ili tuyapate kwa 2000/l mikoa na 1700/l Kwa DSM.😁.
 
"Katika mazungumzo yake kwenye kikao chetu usiku, Rais Samia alionesha kusononeshwa na kusikitishwa kwake na hata kama bei za soko la dunia ziko juu, lakini tutangulize utu na huruma na kuwajali wananchi" - January Makamba,
IMG-20220510-WA0010.jpg
 
Kufikia hiyo June mosi tayari bei ya mafuta itakuwa kwenye 3800/l.

Wakisema waondoe kodi&tozo pekee ambayo ni kama 800/l tutakuwa tunanunua kwa 3000/l.

Hii 3000/l nayo haimalizi hata wiki ipande.

Sioni umuhimu wa vyama vya siasa kugawiana ruzuku kila mwezi na hiyo misamaha ya kodi kwa taasis za dini ifutwe.

Serikali ifute kodi yote kwenye mafuta na itie 1000/l ili tuyapate kwa 2000/l mikoa na 1700/l Kwa DSM.[emoji16].
Mkuu, Mwezi ujao inawezekana bei ikapanda zaidi.

Solutions ilikuwa ni kuondoa hizo tozo za ajabu, mwisho wa siku wanasema tozo zinaenda kwenye kujenga BARABARA alafu barabara zenyewe kwa sasaivi hatuzioni wakijenga

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Bunge litaendelea na vikao vyake leo na kubwa linalotarajiwa kutokea ni mrejesho wa hatua ambazo Serikali inatarajiwa kuchukua kukabiliana na kupanda kwa kasi bei za mafuta kunakotajwa kusababishwa na vita ya Urusi na Ukraine. Hali hiyo ilipelekea ongezeko la nauli kwenye daladala ambalo mara ya mwisho zilipanda Aprili 12, 2013.

May 5 mwaka spika wa Bunge, Tulia Ackson alimpa waziri Makamba siku tano kuja na ufafanuzi kutoka kwa Serikali juu ya hatua za dharura ambazo Serikali inatarajia kuchukua. Kwenye kikao hicho wabunge wengi walipendekeza baadhi ya tozo ziondoke kushusha bei ya mafuta au Serikali ikope ili kuipa ruzuku sekta ya mafuta.

Kujielimisha zaidi, soma:
=> Bungeni: Mjadala wa dharura kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta nchini. Mbunge asema tozo mbili zinaongeza 792 kwenye bei

=> Rais Samia atangaza neema punguzo ya bei za mafuta kuanzia Juni 1, 2022

Kaa nami

======

Makamba:- Rais Samia amesononeka na kupanda mafuta na bidhaa
Waziri Makamba: Rais Samia alituweka kitako usiku mkubwa akasema mengi kwa uchungu mkubwa, akaonesha masononeko. Alielezea kugusa kwake na kusononeka kwake juu ya kupanda kwa gharama za mafuta nchini na gharama za bidhaa mbalimbali.

Akasema hata kama bei ya mafuta duniani iko juu, hata kama takwimu na namba zinaleta mantiki lakini tutangulize utu na huruma kwanza katika kulishughulikia jambo hili.

Hatuzalishi hivyo wahanga wa bei
Nchi yetu haina visima vya mafuta wala mashine za kuchakata mafuta ghafi, sisi ni wapokeaji wa bei kwa maana wahanga wa bei.

Mwezi Oktoba 2021 Serikali ilichukua hatua ya kupunguza tozo zifuatazo
  1. Tozo ya miundombinu ya bandari iliyokuwa inalipwa kwa mamlaka ya bandari.
  2. Tozo ya kuchakata nyaraka za forodha(Customs processing fee) inayolipwa TRA
  3. Tozo ya kupima na kuthibitisha viwango vya mafuta nchini iliyokuwa inalipwa kwa wakala wa vipimo Tanzania(WMA)
  4. Serikali ilipunguza tozo ya kupima na kuthibitisha ubora wa mafuta iliyokuwa inalipwa kwa TBS
  5. Ilipunguza tozo ya wakala wa meli inayolipwa kwa shirika la wakala wa meli(TASAC)
  6. Ilipunguza tozo ya udhibiti ya biashara ya mafuta iliyokuwa inalipwa kwa Ewura.
Makamba: Katika mjadala wa mafuta kumekuwepo kulinganisha bei za mafuta za nchi yetu. Kulinganisha bei lazima kuendane na kulinganisha kila kitu kinachoingia katika bei ikiwemo viwango vya kodi na tozo.

Sisi kama nchi tumeweka kodi ya shilingi zaidi ya 900 kwenye kila lita ya petroli.

MKOPO
Makamba:
Serikali ilianza taratibu za kuchukua mkopo wenye masharti nafuu kutoka benki ya dunia na shirika la fedha duniani(IMF) kwa ajili ya kuweka ahueni kwenye bei za mafuta na bidhaa nyinginezo.

Mchakato wa kuchukua mkopo huu uko mbioni kukamilika na ahueni ya kupanda kwa bei ya mafuta na bidhaa mbalimbali itapatikana kutokana na mkopo huu katika mwaka ujao wa fedha.

RUZUKU
Makamba:
Hata hivyo kutokana na mahitaji ya wananchi na mapendekezo ya wabunge, mheshimiwa Rais alitoa maelekezo kwamba mwaka ujao wa fedha ni mbali kusubiri ahueni hiyo na akaelekeza kwamba ahueni itafutwe haraka zaidi.

Katika kipindi hiki kabla hatujafikia mwaka mpya wa fedha, Serikali ijibane, ijinyime na zitolewe Tshs bilioni 100 kwaajili ya kupunguza bei za mafuta hapa nchini.

Kwahiyo Serikali imeamua kutoa bilioni 100 sasa kwaajili ya kutoa ahueni kwaajili ya mafuta. Ruzuku hii inatolewa kwa kupunguza matumizi ya Serikali katika kipindi kilichobaki katika mwaka huu wa fedha.

Kutolewa kwa ruzuku hii hakutagusa miradi ya maendeleo ambayo inaendelea. Nafuu ya bilioni 100 ni nafuu ya kipindi cha mpito kuelekea kwenye mwaka mpya wa fedha ambapo nafuu nyingine inayotokana na mikopo niliyoelezea awali itakuja kwenye mwaka ujao wa fedha na itaelezwa kwa kina zaidi na waziri wa fedha katika bajeti ya Serikali ya mwezi ujao.

Ruzuku itatolewa kupunguza bei za mafuta kuanzia Juni 1. Hii inatokana na kuwa, wafanyabiashara kwa mfumo wa biashara ya mafuta, wafanyabiashara wa jumla wameshalipia ya mafuta ambayo imejumuishwa kwenye bei na wafanyabiashara wa mafuta kwenye vituo wameshanunua mafuta kwa bei inayotumika sasa.
Tatizo wanasiasa ni wanafiki sana. Mama mwenyewe kasema mafuta yatapanda bei. Kila kitu kitapanda Bei. Na yeye ndo aliondoa hiyo 100. Na huyu huyu hangaya kasema mafuta USA yako juu kuliko Tanzania. Leo anasikitika na kusononeka.

Yaan wanaccm wanatuona wananchi wote ni mazuzu. Hawa jamaa ni wanafik sana aisee

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
"Bei kubwa ya mafuta tuliyoishuhudia nchini sasa inatokana na bei kubwa ya mafuta duniani kuanzia mnamo mwezi Machi mwaka huu, ni bei ambayo haikuwahi kufikiwa katika kipindi cha miaka 14 sasa"
IMG-20220510-WA0011.jpg
 
Utu kutoka kwa nani? MSD wamepiga ela nyingi za UVICO yaani mamilioni ya pesa bila hata huruma!

kwa nini MSD wasionyeshe utu kwa watu maskini?

Tuanzie hapo!
 
[emoji3][emoji3][emoji3] wamenishangaza sana kukopa Ili kuleta unafuu wa mafuta.
.
Siyo Wana cut expenditure na wanaendelea na expenditure zile zile ila wanaenda kukopa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
1.* IMETOA RUZUKU YA SHILINGI BILIONI 100, ILI KUTOA AHUENI YA BEI YA MAFUTA KWA WANANCHI KUANZIA 1, JUNE 2022.

2. KURUHUSU WATU WA KUINGIZA MAFUTA KWA BEI NAFUU KUANZA MAFUTA NA GHARAMA ITAPUNGUA TENA AGOSTI 2022

3. KUANZISHWA KWA MFUKO WA KUKABILIANA NA MFUMUKO WA BEI YA MAFUTA (FUEL PRICES STABILIZATION FUND)

4. KUANZISHA UTARATIBU WA KUHIFADHI MAFUTA YA KIMKAKATI.

5. KUJENGA MAGHALA MAKUBWA YA KUHIFADHI MAFUTA KWA AJILI YA KUUZA NDANI NA NJE YA NCHI.

6. KUANZA UPOKEAJI WA MAFUTA KATIKA GHALA MOJA (SINGE RECEIVING TERMINAL), ILI KUPUNGUZA MUDA WA MELI KUSUBIRI PINDI INAPOLETA MAFUTA AMBAPO NAYO ILIKUA SABABU YA KUPANDA KWA GHARAMA ZA BEI YA MAFUTA.

7. KUONGEZEWA UWEZO WA TAASISI YA TPDC ILI KUFANYA BIASHARA YA MAFUTA.

8. KUBORESHA UTENDAJI KAZI WA TAASISI ZINAZOJIHUSISHA NA MASUALA YA MAFUTA IKIWEMO EWURA.

#KaziIendelee
#TanzaniaSalamaNaSamia
#SisiTumekubali
IMG-20220510-WA0012.jpg
 
Back
Top Bottom