Serikali kutoa ruzuku ya bilioni 100 kunusuru bei ya mafuta. Yaomba mkopo IMF na Benki ya Dunia

Serikali kutoa ruzuku ya bilioni 100 kunusuru bei ya mafuta. Yaomba mkopo IMF na Benki ya Dunia

Watakaokuelewa ni wachache sana, tena ambao ndiyo walewale mlikokotoa hizo bil 100 mkaona zinatufaa watu 60m kwa siku 30.

Utaniambia kama impact ya Bil 100 kwa watu mil 60 kwa wezi itaonekana....huu ni UTANI, ni bora mngeacha kabisa ili lijulikane moja.
Hatukurupuki,hata hiyo impacts hatuiangalii kwenye maumivu yenu bali tunaangalia kama consumption ya mafuta imepungua ndio tunafanya uamzi..

Wewe unaeweka Lita 10 kwa wiki hakuna kitu utaona ila anaetumia mitambo na kuweka mafuta mengi ataona ahueni.
 
Bunge litaendelea na vikao vyake leo na kubwa linalotarajiwa kutokea ni mrejesho wa hatua ambazo Serikali inatarajiwa kuchukua kukabiliana na kupanda kwa kasi bei za mafuta kunakotajwa kusababishwa na vita ya Urusi na Ukraine...
Muvi mpya hiyo.

Tunaenda kuomba mkopo wakati tuna madini na Almasi mlima hazieleweki zinakouzwa.

Wanapiga tu. Tunawezaje kujiendesha. Yale aliyosema Jobo Ndugai yanaendelea kujirudia hadi tuuze nchi.

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Kazi iendelee

Billioni 100 si haba

👊Tuna Imani na Rais Samia... kipenzi cha watanzania
 
Makamba anaweza kuwa kiongozi/ waziri mzuri sana, japo siyo kwa wizara aliyopo. Nashauri apewe Prof. Muhongo. Anayo mapungufu lakini ni bora zaidi. Magufuli alimuonea kumtoa kisa hajajenga smelter za makinikia, kwani mpaka leo makinikia yanasafirishwa nje kama kawa.,,
 
Mtanikumbuka tu nasema mtanikumbuka .nchi yeyote duniani ili kufika mbali inahitaji dikteta awapeleke mpaka mambo yakae saw Kwa command ila ukiwa mnajifanya watu demokrasia mtajuta bado sana nchi za Africa kuwa na demokrasia
Unafikiri Magu angefanya nini kwa kipindi Kama hiki? Unafikiri hii ni korona? Vita vya wakubwa historically wanaoumia ni wadogo,refer 1st and 2nd world wars.
 
Kwa siku nchi inatumia mafuta lita 1.7m Petrol, 3.54M diesel na lita 200k za mafuta taa.... Ukitoa billion 100 kama ruzuku ina maana kwa bei ya 3,000 per lita unalipia lita 34m.

Ambapo kwa siku serikali itakua inatoa lita 1.1m kama ruzuku kupunguza makali. Kwa matumizi ya hizo lita (3.54+1.7+0.2)m ambayo ni jumla ya lita 5.44m lita per day ina maana mafuta yatashuka kwa kiasi kati ya 500 mpaka 612.

So punguzo hili kama litaanza mwezi ujao na kama soko la dunia hawatapandisha bei mafuta yatauzwa 2,500-2,700/=. Na kama soko la dunia mafuta yatapanda basi bei ya mafuta itakua ni kati ya 2,800 - 3,100/= Kwa lita.

Tuishi humu kwa sasa.
 
Bunge litaendelea na vikao vyake leo na kubwa linalotarajiwa kutokea ni mrejesho wa hatua ambazo Serikali inatarajiwa kuchukua kukabiliana na kupanda kwa kasi bei za mafuta kunakotajwa kusababishwa na vita ya Urusi na Ukraine...
yaani tunaongozwa kimafumbo mafumbo tu,mara ooh jambo lenu lipo, mara bei ya pipa duniani, tozo za kitaasisi...takwimu nyingiii, TUAMBIENI MAFUTA BEI ELEKEZI SHILINGI NGAPI. heh?
 
IMG-20220510-WA0002.jpg
 
Hizo ngonjera wangebandika kwenye Ofisi zao, sisi tuambiwe Lita moja ya mafuta imepungua kwa kiasi gani?
 
Maneno meengiii.... tolewe bei tujue tumepunguziwa ngapi.Kila kitu kukopa duuuh!
 
Si mpunguze mi tozo hao mambugila wa EWURA sjui TBS na vitaasisi uchwara walazimike kupunguza matumizi ya lazima baada ya fedha zao kupungua?? Mkopo wa nini?
 
China mbali, Marekani hapo, aliyewatoa kwenye great depression na kuifanya liwe taifa lenye nguvu duniani 1933 - 1945 alikaa madarakani awamu 4 na akafia madarakani. Tokea 1945 Marekani ndio ikawa nchi yenye nguvu duniani kuliko zote. Sisi hapa bila vita nchi hii haiendi.
Anaitwa Nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom