Serikali kuwajadili waliokataa Ukuu wa Wilaya

Serikali kuwajadili waliokataa Ukuu wa Wilaya

KWANI N MJINGA HATAKI ULAJI
HAO WASHANUSA WASHDADISI
WAKAONA POSHO ZAHUKU ZINAWATOSHA KABISAA WAACHENI WAMALIZE MBIO ZAO SALAMA WAKOWAO TU?
 
Watoto wanafeli mitihan Kwa kiwango kikubwa sana

Maajabu tuna Viongozi wanoumia, kisa Aloteuliwa, hataki uteuzi wenyewe !!.

Hivi wanaotaka UDC wameisha? Mbona Wana CCM ni wengi? Mtu kama hataki Ukuu wa Wilaya, siumuacheee, Kwan lazima? Kwann tuanze kutafutana?

Yaan Tuna Viongozi ambao bado Wana Ile mentality ya kikoloni.

Hii Nchi Sijui Imelaaniwa na nani.

 
Unajua lazima tukae chini tufikiri zaidi.
Hebu waza, huyu mtu ni Rais wa cwt, mwingine ni katibu mkuu...ok forget baadhi ya hoja ambazo naziona kwa baadhi ya wajumbe, mmoja akidai wakaguliwe n.k. sasa mtu ana cheo kama hiki, unampa ukuu wa wilaya, ndio kusema nchi haina watu mbadala wa kuwapa hiyo nafasi mpaka umpe mtu mwenye cheo kingine? Maana yake, huyo aachie hiyo ngazi ufanyike uchaguzi mwingine wa kumpata rais na katibu...
Hili jambo lisiangaliwe kimhemuka bali twende na uhalisia. Kuna sabb gani ya kufanya hivyo kwa watu wa namna hiyo?
Listi wa wasomi imeisha?
 
Wateule wa nafasi za Ukuu wa Wilaya ambao inasemekana wamekataa uteuzi huo watatakiwa kutoa maelezo ya kwa nini wameshindwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kwa ajili ya uapisho.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amesema wanasubiri taarifa kutoka kwa wizara zinazohusika ili waangalie taratibu na sheria zinasema nini juu ya viongozi wa Chama cha Walimu Nchini (CWT) kutotokea kula kiapo cha ukuu wa wilaya katika mikoa husika.

Viongozi walioshindwa kuapa ni Rais wa CWT, Leah Ulaya ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita na Katibu Mkuu wa chama hicho, Japheth Maganga aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Kagera

Katika kile kinachoonekana kutokuwepo kwa taarifa rasmi juu ya udhuru wao, Waziri Mhagama amesema yeye pia ameona kwenye vyombo vya habari kuwa wateule hao hawajaripoti katika viapo vyao kama walivyofanya wateule wengine katika maeneo yao ya kazi.

Amesema wateule hao walitakiwa kutii uteuzi huo kwa sababu katiba inamruhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Sululu Hassan kufanya hivyo.

Kumekuwa na mijadala katika mitandao ya kijamii kwa vigogo wa Chama cha Walimu Nchini (CWT) kutofika katika vituo vyao vya kazi kwa uapisho.

Amesema wanachosubiri ni taarifa rasmi kutoka wizara zinazohusika wao yaani Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Ipo siku tutakuja gundua shetani ajapokuwa amefungwa bado anamizizi ktk mioyo ya wanadam. Kwani ni lazima kuwa DC? Chuki, wivu, husuda na michongo inalitesa Taifa. Hakuna upendo roho za kwanini zinalitesa Taifa mtu waziri ila bado anamuonea wivu masikini alie jikwamua nakuwa Tajiri, mtu ananafasi na mshahara mzuri ila anaona wivu kwenye mshara wakijana analipwa laki Tano kisa yule kijana anamaendeleo na pesa yake Boss anaonga nakula Raha... Masikini anapambana na hali yake mtaani Mungu anamuona Anatoka mtoza ushuru anakuja nakumwambia unadaiwa kodi 500m kiasi ambacho hata Mali yake haikifikii... Unashamba kubwa ila bado hata shamba la masikini unadhulumu.
Ndugu zangu msione haya ni yakawaida ipo siku tutaulizana tumefikaje hapa chuki mtaani chuki makanisani chuki misikitini chuki kwa wapagani chuki kila mahali Mungu liponye Taifa. Watu wangapi hawana kazi na wana akili msiwape hizo nafasi muanze tafutana kisa teuzi? Mungu hawezi dhihakiwa chochote apandacho mtu ndicho anachovuna. Mungu niwetu sote. Amen
 
Watoto wanafeli mitihan Kwa kiwango kikubwa sana

Maajabu tuna Viongozi wanoumia, kisa Aloteuliwa, hataki uteuzi wenyewe !!.

Hivi wanaotaka UDC wameisha? Mbona Wana CCM ni wengi? Mtu kama hataki Ukuu wa Wilaya, siumuacheee, Kwan lazima? Kwann tuanze kutafutana?

Yaan Tuna Viongozi ambao bado Wana Ile mentality ya kikoloni.

Hii Nchi Sijui Imelaaniwa na nani.

Kuna aliye kuwa na mentality ya kikoroni kama jiwe na bado ukawa chawa wake.

Acha unafiki.
 
Kuna protocol mkuu athari kwa mtumishi wa umma kukata alikotumwa na bosi wake ni kubwa.Sahau nchi nyingine wanafanyake deal mifumo ya utawala wetu na sheria za utumishi zekoje kwetu.
DC sio kaz ya utumishi, ni nafasi za kisiasa... acha kuish kwa woga mkuu, na ndio maana muda wowote unaweza tenguliwa bila notice... acheni siasa nyepesi
 
Tayari ameapishwa, asingeapishwa ingebidi achukuliwe hatua za kinidhamu. Mtumishi yeyote wa umma hapaswi kukataa uteuzi kwa maslahi yake binafsi
 
Mbona kama sio wasomi waajiriwa? Muajiri wao ni serikali ambayo inawalipa mishahara na inaweza kuwapangia majukumu mengine kwa kuwa ni waajiri wake. Kwanza ni utovu wa nidhamu kugomea uteuzi huo
Uteuzi wa rais ni wa kisiasa, ajira nyingine za serikali zinategemea taaluma ya mtu. Mfano huwezi kumteua mwalimu kuwa mkuu wa majeshi
 
Unajua lazima tukae chini tufikiri zaidi.
Hebu waza, huyu mtu ni Rais wa cwt, mwingine ni katibu mkuu...ok forget baadhi ya hoja ambazo naziona kwa baadhi ya wajumbe, mmoja akidai wakaguliwe n.k. sasa mtu ana cheo kama hiki, unampa ukuu wa wilaya, ndio kusema nchi haina watu mbadala wa kuwapa hiyo nafasi mpaka umpe mtu mwenye cheo kingine? Maana yake, huyo aachie hiyo ngazi ufanyike uchaguzi mwingine wa kumpata rais na katibu...
Hili jambo lisiangaliwe kimhemuka bali twende na uhalisia. Kuna sabb gani ya kufanya hivyo kwa watu wa namna hiyo?
Listi wa wasomi imeisha?
kuna msemo unasema mwenye nacho huongezewa, hao viongozi wamechomoza na wameonwa na mamlaka za uteuzi za nchi. Nafasi walizonazo waachie wengine nao wachomoze. Ni wakati wa walimu nao kuula serikalini, sio kustaafia kwenye ualimu tu. Walimu wakae mkao wa kula kuna teuzi zingine kama ukurugenzi wa halmashauri na promosheni zingine zitakazowatoa kwenye ualimu.
 
Mh Rais imulikeni CWT!!! Kikichotokea nimrejesho kuwa ndani ya CWT Kuna ujujaji wa kutisha, pia napendekeza walimu wakatwe tsh 8000 kama CWT contribution!! Wasikatwe kulingana na ukubwa wa mshahara kama ilivyo sasa
Unayemwambia aimulike CWT ndiye anayekata hizo pesa kutoka kwa watumishi na kuwapa.

Nani aliyetunga Sheria ya Ajira na mahusiano kazini ya 2004 = Mwajiri.

Nani anayekata pesa na kuwapa CWT = Mwajiri.

Sasa wao wamepewa pesa kutoka kwa watawala MAJUHA unataka wasile
 
Hapa naona issue ni kwamba hawakutoa maelezo au sababu za kwanini wameshindwa kufika kwenye maeneo yao ya kazi ili kuapishwa,ukisoma thd inaonekana kabisa kua tatizo sio kugomea uteuzi bali ni kutokutoa maelezo ya wao kutokufika kwenye kuapishwa BUT kukataa teuzi pia inaweza kua ni issue nyingine au wameshindwa kuitaja direct.
 
Back
Top Bottom