Yaani kama wewe ni mtumishi wa Serikali huwezi kugomea uteuzi wa Mh Rais kirahisi rahisi tu! Kumbuka hata hapo ulipo yeue ndio Mwajiri Mkuu! Kwahiyo hawa ndg zetu kifupi wameyakanyaga!
Kibaya zaidiwatu wanahusisha kukataa kwao uteuzi kunatokana na maslahi makubwa wanayoyapata kutoka kwenye pesa za walalahoi na watu wasiofaidika chochote na uwepo wa Chama hicho cha Waalimu!!!
Lichama lipolipo tu linakusanya pesa nyingi kutoma kwa Waalimu badala yawe na ubunifu wa kuwasaidia walimu hata kuwapa mikopo ya riba nafuu hawawezi! Ujinga mwingi sana na badala yale wahuni wanazipiga tu na kulipana mishahara ya kutisha huku wachangiaji wakizidi kuchoka tu!!
Hata Mwalimu akistaafu hapati chochote cha maana hata shukrani tu ya kuwachangia!
Mkuu Carlos The Jackal , kwanza post za ma DC ni muendelezo tuu wa the colonial legacy, kwa mfumo wetu, they are redundant post just a wasted of money, time and resources. Hivyo hao viongozi wetu kuwa na colonial mentality kwenye colonial legacy, they are very right.
Kwenye presidential appointments kuna wateuliwa wa aina mbili, 1. Wateuliwa kutoka public service, hawa ni watumishi wa umma, mtu kutoka public service akiteuliwa nafasi yoyote, hawezi kukataa uteuzi. Rais wa JMT ndie mwajiri wa public service yote, ukiteuliwa na rais na kukataa uteuzi, ni kosa kubwa linaloitwa insubordination, adhabu yake ni summary dismissals with no right to appeal!.
Hivyo mtumishi wa umma anapoteuliwa na rais kushika wadhifa wowote, ni lazima atekeleze au a hand over resignation letter yake na kupisha kuendelea na mambo yake. Hivyo hao waalimu wawili waliokataa uteuzi wa rais, kama nafasi zao kwenye chama cha waalimu ni ajira rasmi, na baada ya kupata nafasi hizo, walijiuzulu ualimu, then they are safe kukataa uteuzi wa something less than what they are, lakini kama nafasi zao sio ajira rasmi ni vyao tuu, lakini bado ni waajiriwa wa utumishi wa umma, kukataa uteuzi wa Mkuu wa nchi ni insubordination of the highest nature and they are finished!.
Kuna uteuzi wa rais kwa watu kutoka private sector, na independent organisations vikiwemo trade unions na professional associations, to avoid unnecessary embarrassment kumu embarrass the appointing authority, mtu kabla hujateuliwa unaulizwa kama uko tayari ndipo jina linapelekwa, unateuliwa.
Wako watu wengi tuu huwa wanaulizwa na wana kataa. Na kwa wasiojua, hii sio mara ya kwanza kwa watu kukataa uteuzi wa u DC, General Ulimwengu aliwahi kuteuliwa DC, sikumbuki vizuri kama ni aliripoti akaona kuko hovyo, akaandika barua kujiuzulu na kuwaachia u DC wao!.
Jielimishe zaidi kuhusu presidential appointment powers, rais ni dual personality rais ni mtu hivyo mambo mengine rais anakataliwa tuu kama mtu mwingine yeyote anavyo kataliwa, ila rais kama presidential institution, hawezi kukataliwa kitu, ukimkatalia, unakataliwa!.
Nakikumbuka kisa kimoja cha rais fulani mpenda mambo fulani, akamuita mteuliwa fulani akambomu jambo fulani la binafsi, mteuliwa huyo alikuwa very bold!, alimkatalia rais wa nchi hilo jambo!, na akaondoka, hivyo rais huyo alikasirika sana, akatumia rungu lake ya presidential institution, akanyanyua simu kutoa maelekezo fulani mahali, yule mtumishi akashughulikiwa!.
Wanabodi, Bandiko hili ni kufuatia watu fulani humu wenye viherehere na vimbelembele kutaka kuhoji kila kitu sasa wameingilia kuhoji uwezo wa serikali ya JPM kufanya vetting kabla ya teuzi fulani fulani, kumbe hawajui kuwa now days vetting is nothing!. Kinachoangaliwa sasa ni uwezo wa utendaji...
chama cha walimu kina mihela ya bure ya kula ndiomaana wamekataa ila ingekuwa enzi za jiwe anavunja chama anaamuru waingie tughe ama talgwu mchezo umeisha ukienda kushitaki kesi inatupwa ndio unajua hujui, jamaa alijikuta mungu sana yule, ila hata hawa watashughulikiwa tu ni suala la muda tu believe me
wale walimu hawana jeuri ya kugomea teuzi za muajiri wao. Haingii akilini kugomea promosheni kwa mwalimu. Watakubali tu la sivyo waache kazi kitu ambacho ni ujuha kuacha kazi kwa kugomea uteuzi wa mkuu wa nchi aliyekutunuku heshima
hata mm nimemsikia Jenista mhagama akiliongelea jambo hilo na nimeshindwa kuelewa.kwani ni lazima ukiteuliwa na rais nafasi fulani ukubali hata kama unaona huwezi kuimudu nafasi hiyo?si wawateue wengine kwani wenye sifa hizo ndani ya ccm wameisha mpaka wawang'ang'anie hao hao tu?hawataki kwani ni lazima.
Kuna protocol mkuu athari kwa mtumishi wa umma kukata alikotumwa na bosi wake ni kubwa.Sahau nchi nyingine wanafanyake deal mifumo ya utawala wetu na sheria za utumishi zekoje kwetu.
mbona wakati wa Magu kuna mtu alikataa uteuzi wake na akaachwa kwa nn huyu jenister analeta kiherehere.elimu yake yenyewe ni kidato cha nne na nusu kombi ya HL lkn ujuaji mwingiiii.
Huo ni mtego,unaweza ukateuliwa huo ukuu wa wilaya na ukatenguliwa na huko ushaaga kwa mbwembwe.Watu wanaogopa kuumbuka mjini.Kila mwezi ni kuteua na kutumbua
Wateule wa nafasi za Ukuu wa Wilaya ambao inasemekana wamekataa uteuzi huo watatakiwa kutoa maelezo ya kwa nini wameshindwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kwa ajili ya uapisho.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amesema wanasubiri taarifa kutoka kwa wizara zinazohusika ili waangalie taratibu na sheria zinasema nini juu ya viongozi wa Chama cha Walimu Nchini (CWT) kutotokea kula kiapo cha ukuu wa wilaya katika mikoa husika.
Viongozi walioshindwa kuapa ni Rais wa CWT, Leah Ulaya ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita na Katibu Mkuu wa chama hicho, Japheth Maganga aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Kagera
Katika kile kinachoonekana kutokuwepo kwa taarifa rasmi juu ya udhuru wao, Waziri Mhagama amesema yeye pia ameona kwenye vyombo vya habari kuwa wateule hao hawajaripoti katika viapo vyao kama walivyofanya wateule wengine katika maeneo yao ya kazi.
Amesema wateule hao walitakiwa kutii uteuzi huo kwa sababu katiba inamruhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Sululu Hassan kufanya hivyo.
Kumekuwa na mijadala katika mitandao ya kijamii kwa vigogo wa Chama cha Walimu Nchini (CWT) kutofika katika vituo vyao vya kazi kwa uapisho.
Amesema wanachosubiri ni taarifa rasmi kutoka wizara zinazohusika wao yaani Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu.

Sheria za kazi zinasemaje endapo mtu amekataa uteuzi? Mimi nafikiri mtu aandaliwe kwanza kisakolojia, kwanza kwa kumuhoji kuhusu utayari wake endapo atateuliwa kufanya kazi fulani kupitia teuzi zinazofanywa na taasisi nyeti ya urais.
Ili kuepuka suala kama hili lisijirudie, wateule watarajiwa wapimwe kwanza kuhusu utayari wao wa kuweza kutumikia majukumu mapya na kuyaacha yale ambayo wanayatumikia kwa wakati uliopo. Wengine hukwepa kufanya hivyo ili kukwepa mgongano wa maslahi.
hata mm nimemsikia Jenista mhagama akiliongelea jambo hilo na nimeshindwa kuelewa.kwani ni lazima ukiteuliwa na rais nafasi fulani ukubali hata kama unaona huwezi kuimudu nafasi hiyo?si wawateue wengine kwani wenye sifa hizo ndani ya ccm wameisha mpaka wawang'ang'anie hao hao tu?hawataki kwani ni lazima.
Wanaona Raisi wao kazarauliwa , ifikie hatua wajue tuu kuwa Raisi ni binadamu Tu na yeye , madaraka hayo amepewa Tu na Mungu kwa Mda , na hawezi nyenyekewa na kila mtu , watu sio waoga wa maisha Yao , wengine wanajitambua bhana ..... Kama vip waueni sasa si mamlaka mnayo , sio kila sku kubwabwaja tuu na kulazimisha kitu ambacho wenyewe hawataki hyo kazi
Amesema wateule hao walitakiwa kutii uteuzi huo kwa sababu katiba inamruhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Sululu Hassan kufanya hivyo.
Kwanini hajataja kipengele!!!
Kumtoa mtu kwenye kazi yake je, hakuna utaratibu? Wanapewa siku ngapi wakipokea ofa na kutakiwa kujibu? Kazi za CWT hazina utaratibu wake wa mtu anatokaje na inakuwaje? Na contract zao walipo zinasemaje?
Imekaa kama kuwaondoa watu waweka wanaowataka.. michezo hii ya kufukuza mtu kazi alipo? Je, akimaliza kuwa DC wanaweza kurudi?
Why ni lazima mtu akubali uteuzi kama anajijua hataki kazi hiyo?
Serikali na Rais kweli wanataka watumishi ambao wanajiona kazi hawawezi au kuzitaka?
ni bora nikaachishwa kazi kuliko kuingia kwenye mifumo ya hovyo ya nchi hii.kama rais analalamika kuhusu pesa za plea bargaining wakati yeye alikuwa makamu wa rais na makamu wake wa sasa alikuwa waziri wa fedha sasa hayo si maajabu ya dunia?kama watashughurikiwa itakuwa ni uonevu wa hali juu na tutakuwa tunarudi kwenye mambo ya hovyo ya awamu ya tano.
Mkuu Carlos The Jackal , kwanza post za ma DC ni muendelezo tuu wa the colonial legacy, kwa mfumo wetu, they are redundant post just a wasted of money, time and resources. Hivyo hao viongozi wetu kuwa na colonial mentality kwenye colonial legacy, they are very right.
Kwenye presidential appointments kuna wateuliwa wa aina mbili, 1. Wateuliwa kutoka public service, hawa ni watumishi wa umma, mtu kutoka public service akiteuliwa nafasi yoyote, hawezi kukataa uteuzi. Rais wa JMT ndie mwajiri wa public service yote, ukiteuliwa na rais na kukataa uteuzi, ni kosa kubwa linaloitwa insubordination, adhabu yake ni summary dismissals with no right to appeal!.
Hivyo mtumishi wa umma anapoteuliwa na rais kushika wadhifa wowote, ni lazima atekeleze au a hand over resignation letter yake na kupisha kuendelea na mambo yake. Hivyo hao waalimu wawili waliokataa uteuzi wa rais, kama nafasi zao kwenye chama cha waalimu ni ajira rasmi, na baada ya kupata nafasi hizo, walijiuzulu ualimu, then they are safe kukataa uteuzi wa something less than what they are, lakini kama nafasi zao sio ajira rasmi ni vyao tuu, lakini bado ni waajiriwa wa utumishi wa umma, kukataa uteuzi wa Mkuu wa nchi ni insubordination of the highest nature and they are finished!.
Kuna uteuzi wa rais kwa watu kutoka private sector, na independent organisations vikiwemo trade unions na professional associations, to avoid unnecessary embarrassment kumu embarrass the appointing authority, mtu kabla hujateuliwa unaulizwa kama uko tayari ndipo jina linapelekwa, unateuliwa.
Wako watu wengi tuu huwa wanaulizwa na wana kataa. Na kwa wasiojua, hii sio mara ya kwanza kwa watu kukataa uteuzi wa u DC, General Ulimwengu aliwahi kuteuliwa DC, sikumbuki vizuri kama ni aliripoti akaona kuko hovyo, akaandika barua kujiuzulu na kuwaachia u DC wao!.
Jielimishe zaidi kuhusu presidential appointment powers, rais ni dual personality rais ni mtu hivyo mambo mengine rais anakataliwa tuu kama mtu mwingine yeyote anavyo kataliwa, ila rais kama presidential institution, hawezi kukataliwa kitu, ukimkatalia, unakataliwa!.
Nakikumbuka kisa kimoja cha rais fulani mpenda mambo fulani, akamuita mteuliwa fulani akambomu jambo fulani la binafsi, mteuliwa huyo alikuwa very bold!, alimkatalia rais wa nchi hilo jambo!, na akaondoka, hivyo rais huyo alikasirika sana, akatumia rungu lake ya presidential institution, akanyanyua simu kutoa maelekezo fulani mahali, yule mtumishi akashughulikiwa!.
Wanabodi, Bandiko hili ni kufuatia watu fulani humu wenye viherehere na vimbelembele kutaka kuhoji kila kitu sasa wameingilia kuhoji uwezo wa serikali ya JPM kufanya vetting kabla ya teuzi fulani fulani, kumbe hawajui kuwa now days vetting is nothing!. Kinachoangaliwa sasa ni uwezo wa utendaji...
Hzi ni taratibu za hovyo , na matokeo Yake ni kutengeneza Taifa la hovyo tuu, hakuna umhimu wwte wa kuwa na taratibu mbovu kama Hz , ndo mana tunasema Raisi apunguziwe mamlaka ya kuteua badala yake watu waombe kazi , Ila awe na mamlaka ya kutengua , kung'ang'ania taratibu kama hzi matokeo Yake ndo haya kulazimisha watu wa kutii , na wakizingua unaona kama umedharauliwa , majamaa wamekataa hyo kazi hawataki , ya nini kuanza kuwatisha tisha, chawa wote sa hv fyoko fyoko , kila Kona utasikia mama mama .....
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.