Serikali kuwajadili waliokataa Ukuu wa Wilaya

Serikali kuwajadili waliokataa Ukuu wa Wilaya

Siyo kila mtu anaweza kuwa DC
For this case, why only viongozi wa CWT leaders denied an appointment? Hupati maswali ya kujiuliza? Hujiulizi kuna nini CWT?

Kuna mahali nilisoma moja ya indications za fraud ni mtu kugomea kuhama ofc, teuzi, Likizo etc.... kuna namna ambayo mtu huyo anataka kuficha uchafu anaoufanya kupitia ofc ile!

That could be the case..... Serikali iwe upande wa Waalimu ifanyike special Auditing ya mfuko wa CWT....tutapata majibu ya kiburi cha hawa viongozi!!!
 
Unajua lazima tukae chini tufikiri zaidi.
Hebu waza, huyu mtu ni Rais wa cwt, mwingine ni katibu mkuu...ok forget baadhi ya hoja ambazo naziona kwa baadhi ya wajumbe, mmoja akidai wakaguliwe n.k. sasa mtu ana cheo kama hiki, unampa ukuu wa wilaya, ndio kusema nchi haina watu mbadala wa kuwapa hiyo nafasi mpaka umpe mtu mwenye cheo kingine? Maana yake, huyo aachie hiyo ngazi ufanyike uchaguzi mwingine wa kumpata rais na katibu...
Hili jambo lisiangaliwe kimhemuka bali twende na uhalisia. Kuna sabb gani ya kufanya hivyo kwa watu wa namna hiyo?
Listi wa wasomi imeisha?
Ule mgogoro uliotatuliwa hivi karibuni uliokuwepo kwenye hicho chama uliwahi kuusika? Na kama uliwahi kuusikia; unadhani kwa nini ulikuwepo?
 
Uko sahihi kabisa. Ndiyo maana mamlaka za uteuzi zikawaona wao kuwa wanafaa kuwa ma-DC na siyo mimi au wewe. Vinginevyo kama mimi na wewe tungekuwa tunafaa na si wao, basi wao wasingeteuliwa ila mimi na wewe ndiyo tungekuwa kwenye list hiyo
Aliyeteuliwa mwenyewe kaona hawezi
 
Nashangaa sana jambo moja. Mtu kabla hujampa uteuzi wowote busara ni kumpigia simu na kumtaarifu. Sasa hiina hili wala lile unapangiwa Geita. Ukumbuke

1. Unatoka Dar es salaam wewe mke wa mtu na una watoto na makazi Dar. Sasa unampa mtu week aache ndoa na vingine akatumikie serikali mbali huko ukute hajawahi kufika

2. Inamtoa mtu kwenye cheo kisicho na maehaka unampa uDC anajua mda wowote anatumbuliwa pia labda hana uwezo wa kuwa DC. Kipimo gani umempima kuonyesha kuwa Anaqualify?

3. Mtu Ana kazi yenye marupurup na mshahara mzuri. Unamuamisha kwenye kazi yenye mshahara mdogo. Hata kama ni mimi nisingeweza kukubali. Unajuaje kama Ana mikopo tele na mshahara anaoufata hauendani na kima cha chini cha marejesho ya mikopo. .
Uko sahihi. Kama ni kweli huku ni kupotezeana wakati. Labda kama wanataka kujadili imekuwaje mtu anateuliwa kabla ya kupata uhakika kuwa anautaka huo uteuzi? Hamna mahali penye Katiba au Sheria panaposema kuwa ni lazima mtu kukubali uteuzi.

Badala ya kulikuza na kuangalia namna ya kuwaadhibu wangependekeza watu mbadala lakini safari hii wawaulize kwanza. Na waangalie namna ya kurudisha heshima ya hivi vyeo maana wako watakaosita kukubali vyeo vilivyoshehena wasanii na wanasiasa walioshindwa sehemu zao.

Amandla...
 
...wastage of time and resources, kwwani hii ni vita ya mtukula kwamba mtu asipokwenda anachukuliwa hatua? Au walitaka wakaripoti, wasitimize wajibu wafukuzwe kwa aibu?
Mbona kwenye ajira zingine mtu usiporipoti unatemwa nafasi anapewa mtu mwingine fasta sasa hao cwt mnawang`ang`ania nini au mlikuwa na lenu jambo juu yao
 
Inaelekea due diligence kabla ya uteuzi hakuna kabisa.

Hilo ni tatizo kubwa kwa serikali kushindwa kuwatafuta wateuliwa kabla na kufanya vetting.

Hii kazi ya vetting miaka yote ndiyo kazi ya TISS.

Wizara husika ya yule mama Jenista Mhagama imeshindwa kazi.

Kuteuliwa si adhabu na kukubali uteuzi si lazima.
Labda kuna jambo CWT ambalo Rais alitaka kulifanikisha, yaani kuwaondoa CWT kisha baada ya siku chache kutengua uteuzi hivyo wabaki hawana mbele wala nyuma!
 
For this case, why only viongozi wa CWT leaders denied an appointment? Hupati maswali ya kujiuliza? Hujiulizi kuna nini CWT?

Kuna mahali nilisoma moja ya indications za fraud ni mtu kugomea kuhama ofc, teuzi, Likizo etc.... kuna namna ambayo mtu huyo anataka kuficha uchafu anaoufanya kupitia ofc ile!

That could be the case..... Serikali iwe upande wa Waalimu ifanyike special Auditing ya mfuko wa CWT....tutapata majibu ya kiburi cha hawa viongozi!!!
Yaani upigaji unataka kutufikisha kwenye level ambayo mpigaji ana mamlaka ya kuamua waziwazi kabisa kuwa anapendelea aendelee kupiga wapi
 
Sheria za kazi zinasemaje endapo mtu amekataa uteuzi? Mimi nafikiri mtu aandaliwe kwanza kisakolojia, kwanza kwa kumuhoji kuhusu utayari wake endapo atateuliwa kufanya kazi fulani kupitia teuzi zinazofanywa na taasisi nyeti ya urais.

Ili kuepuka suala kama hili lisijirudie, wateule watarajiwa wapimwe kwanza kuhusu utayari wao wa kuweza kutumikia majukumu mapya na kuyaacha yale ambayo wanayatumikia kwa wakati uliopo. Wengine hukwepa kufanya hivyo ili kukwepa mgongano wa maslahi.
Assuming amekataa uteuzi kwa sababu mahali alipo, alishaji-establish kiasi kwamba bado anadhani kuwa anaweza kuendelea kufanya fraud pasipo kujulikana, kama ataendelea kubaki pale?
 
Ni wakati sasa kama hatuna muongozo wa kuteua watu uandaliwe. Nafikiri ni busara kuwe na option ya mteuliwa kukubali kabla ya kuapishwa
 
Sio lazima kukubaki uteuzi/ cheo, ndio maana mhusika aliyeteuliwa huwa anatakiwa kukiri kukikubali cheo. Kwahiyo unaweza tu kumshukuru aliyekuteua kwa kuonesha imani kwako kisha ukasema haupo tayari kwa majukumu hayo mapya na kwamba hutoweza kuyatekeleza kwa ufasaha, hivyo usije ukamuangusha aliyekuteua.

Kwahiyo unatakiwa kutoa sababu tu za kukakataa uteuzi inaruhusiwa.
Mkuu uloyosema ni sahihi.

Lakini uelewe kwa maelezo yako, mwenye kufanya hivyo alitakiwa afanye wa sekta binafsi.

Ukitunishia misuli ajira ndani ya ajira huku umeajiriwa na serikali hiyo hiyo, haujijengei mazingira rafiki.

Halafu wote waliokataa teuzi wanatoka ofisi moja, huoni kunaleta sintofahamu, unawapa Serikali kuhoji kuna nini ama maslahi gani wanang'ang'ania hawa staff?

Mambo mengi sana yanaweza kuibuliwa hapo.

Embu tusihukumu kwanza tusubiri sakata hili tuone litaishia wapi.
 
Yaani kama wewe ni mtumishi wa Serikali huwezi kugomea uteuzi wa Mh Rais kirahisi rahisi tu! Kumbuka hata hapo ulipo yeue ndio Mwajiri Mkuu! Kwahiyo hawa ndg zetu kifupi wameyakanyaga!

Kibaya zaidiwatu wanahusisha kukataa kwao uteuzi kunatokana na maslahi makubwa wanayoyapata kutoka kwenye pesa za walalahoi na watu wasiofaidika chochote na uwepo wa Chama hicho cha Waalimu!!!

Lichama lipolipo tu linakusanya pesa nyingi kutoma kwa Waalimu badala yawe na ubunifu wa kuwasaidia walimu hata kuwapa mikopo ya riba nafuu hawawezi! Ujinga mwingi sana na badala yale wahuni wanazipiga tu na kulipana mishahara ya kutisha huku wachangiaji wakizidi kuchoka tu!!

Hata Mwalimu akistaafu hapati chochote cha maana hata shukrani tu ya kuwachangia!
Mkuu umeufunga mjadala kwa comment yako hii.
 
Wabongo vichwa vimejaa mende. Ni majuha na maiti mnaotembea.
Sio Kila mtu anaongozwa na mihemko na hisia.Tunaongea tunachojua administratively.Wewe unaleta porojo za mtaani.Do reaserch and attack
 
Wateule wa nafasi za Ukuu wa Wilaya ambao inasemekana wamekataa uteuzi huo watatakiwa kutoa maelezo ya kwa nini wameshindwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kwa ajili ya uapisho.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amesema wanasubiri taarifa kutoka kwa wizara zinazohusika ili waangalie taratibu na sheria zinasema nini juu ya viongozi wa Chama cha Walimu Nchini (CWT) kutotokea kula kiapo cha ukuu wa wilaya katika mikoa husika.

Viongozi walioshindwa kuapa ni Rais wa CWT, Leah Ulaya ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita na Katibu Mkuu wa chama hicho, Japheth Maganga aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Kagera

Katika kile kinachoonekana kutokuwepo kwa taarifa rasmi juu ya udhuru wao, Waziri Mhagama amesema yeye pia ameona kwenye vyombo vya habari kuwa wateule hao hawajaripoti katika viapo vyao kama walivyofanya wateule wengine katika maeneo yao ya kazi.

Amesema wateule hao walitakiwa kutii uteuzi huo kwa sababu katiba inamruhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Sululu Hassan kufanya hivyo.

Kumekuwa na mijadala katika mitandao ya kijamii kwa vigogo wa Chama cha Walimu Nchini (CWT) kutofika katika vituo vyao vya kazi kwa uapisho.

Amesema wanachosubiri ni taarifa rasmi kutoka wizara zinazohusika wao yaani Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Mimi kwa mfano, ni raia wa Tz, Ila sijui na sijaona ni wapi Katiba ya Tz inanilazimisha kwenda na kufanya kazi niliyoteuliwa na rais!
Na kama hivyo ndio utaratibu, Kati ya watu milioni 60, rais kashindwa kuokota yeyote mitaani, kama ni lazima, akaifanye hiyo kazi? Ung'ang'anie watu watatu, wenye shughuli zao muhimu za kutetea waalimu wenzao?! Kama si kusudi maalum la kuwaacha waalimu solemba, rais ana lengo gani zaidi? Ni Ile kamba ndefu ya ulaji, mtu analazimishwa aivae shingoni ili akale!
Rais acha rushwa!
 
Mbona kama sio wasomi waajiriwa? Muajiri wao ni serikali ambayo inawalipa mishahara na inaweza kuwapangia majukumu mengine kwa kuwa ni waajiri wake. Kwanza ni utovu wa nidhamu kugomea uteuzi huo
Matatizo ya kazi zisizo na usaili! Unajiokotea yeyote tu, kwa vigezo gani, halafu bila aibu unamshurutisha! Serikali uozo kabisa!
 
Watoto wanafeli mitihan Kwa kiwango kikubwa sana

Maajabu tuna Viongozi wanoumia, kisa Aloteuliwa, hataki uteuzi wenyewe !!.

Hivi wanaotaka UDC wameisha? Mbona Wana CCM ni wengi? Mtu kama hataki Ukuu wa Wilaya, siumuacheee, Kwan lazima? Kwann tuanze kutafutana?

Yaan Tuna Viongozi ambao bado Wana Ile mentality ya kikoloni.

Hii Nchi Sijui Imelaaniwa na nani.

View attachment 2502023
Hilo neno. Yaan inashangaza
 
Back
Top Bottom