cocochanel
Platinum Member
- Oct 6, 2007
- 27,885
- 76,043
Inaonyesha ni zaidi ya hilo bali wanawaondoa kijanja.. ujanja umefeli wamekasirika. Nafasi wana wakuwapatia wengine tayari
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Katiba Katiba Katiba....Watoto wanafeli mitihan Kwa kiwango kikubwa sana
Maajabu tuna Viongozi wanoumia, kisa Aloteuliwa, hataki uteuzi wenyewe !!.
Hivi wanaotaka UDC wameisha? Mbona Wana CCM ni wengi? Mtu kama hataki Ukuu wa Wilaya, siumuacheee, Kwan lazima? Kwann tuanze kutafutana?
Yaan Tuna Viongozi ambao bado Wana Ile mentality ya kikoloni.
Hii Nchi Sijui Imelaaniwa na nani.
View attachment 2502023
Tatizo lao waliwekeza kwenye mitandao wakaona deal. Wangeweka mikakati ya kukataa kimyakimya huenda yasingekuwa haya. Tatizo wakaanza kupayuka kwenye makundi yao ya whatsapp. Hivyo vyeo walivyonavyo kama ndio vinawapa ujeuri watavisikia tu kwenye bomba na ukaguzi dhidi yao utawafuata.Sio lazima kukubaki uteuzi/ cheo, ndio maana mhusika aliyeteuliwa huwa anatakiwa kukiri kukikubali cheo. Kwahiyo unaweza tu kumshukuru aliyekuteua kwa kuonesha imani kwako kisha ukasema haupo tayari kwa majukumu hayo mapya na kwamba hutoweza kuyatekeleza kwa ufasaha, hivyo usije ukamuangusha aliyekuteua.
Kwahiyo unatakiwa kutoa sababu tu za kukakataa uteuzi inaruhusiwa.
Ukweli ni kuwa tabia na mienendo ya CWT haina tofauti na Ile ya CCM.Rushwa ,wizi,upendeleo ubadhilifu ndio kwao.Waliomo CWT hawataki kutoka kwakuwa Kuna ulaji mkubwa.Nafurahi kuwa siyo mwanachama waoMh Rais imulikeni CWT!!! Kikichotokea nimrejesho kuwa ndani ya CWT Kuna ujujaji wa kutisha, pia napendekeza walimu wakatwe tsh 8000 kama CWT contribution!! Wasikatwe kulingana na ukubwa wa mshahara kama ilivyo sasa
bora ya hao waliokataa uteuzi huo kuliko kukubali hali yakuwa mtu uwezo huo hana mfano alikuwepo mkuu wa wilaya kilombero huyuWateule wa nafasi za Ukuu wa Wilaya ambao inasemekana wamekataa uteuzi huo watatakiwa kutoa maelezo ya kwa nini wameshindwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kwa ajili ya uapisho.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amesema wanasubiri taarifa kutoka kwa wizara zinazohusika ili waangalie taratibu na sheria zinasema nini juu ya viongozi wa Chama cha Walimu Nchini (CWT) kutotokea kula kiapo cha ukuu wa wilaya katika mikoa husika.
Viongozi walioshindwa kuapa ni Rais wa CWT, Leah Ulaya ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita na Katibu Mkuu wa chama hicho, Japheth Maganga aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Kagera
Katika kile kinachoonekana kutokuwepo kwa taarifa rasmi juu ya udhuru wao, Waziri Mhagama amesema yeye pia ameona kwenye vyombo vya habari kuwa wateule hao hawajaripoti katika viapo vyao kama walivyofanya wateule wengine katika maeneo yao ya kazi.
Amesema wateule hao walitakiwa kutii uteuzi huo kwa sababu katiba inamruhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Sululu Hassan kufanya hivyo.
Kumekuwa na mijadala katika mitandao ya kijamii kwa vigogo wa Chama cha Walimu Nchini (CWT) kutofika katika vituo vyao vya kazi kwa uapisho.
Amesema wanachosubiri ni taarifa rasmi kutoka wizara zinazohusika wao yaani Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Humu jukwaani naona watoto ni wengi sana; hawaijui kabisa Serikali namna ambavyo huwa inafanya kazi....wastage of time and resources, kwwani hii ni vita ya mtukula kwamba mtu asipokwenda anachukuliwa hatua? Au walitaka wakaripoti, wasitimize wajibu wafukuzwe kwa aibu?
Haya maoni based kwenye hasira fulani hivi!Yaani kama wewe ni mtumishi wa Serikali huwezi kugomea uteuzi wa Mh Rais kirahisi rahisi tu! Kumbuka hata hapo ulipo yeue ndio Mwajiri Mkuu! Kwahiyo hawa ndg zetu kifupi wameyakanyaga!
Kibaya zaidiwatu wanahusisha kukataa kwao uteuzi kunatokana na maslahi makubwa wanayoyapata kutoka kwenye pesa za walalahoi na watu wasiofaidika chochote na uwepo wa Chama hicho cha Waalimu!!!
Lichama lipolipo tu linakusanya pesa nyingi kutoma kwa Waalimu badala yawe na ubunifu wa kuwasaidia walimu hata kuwapa mikopo ya riba nafuu hawawezi! Ujinga mwingi sana na badala yale wahuni wanazipiga tu na kulipana mishahara ya kutisha huku wachangiaji wakizidi kuchoka tu!!
Hata Mwalimu akistaafu hapati chochote cha maana hata shukrani tu ya kuwachangia!
Maendeleo ya nchi yatapatikana kwa viongozi kupenda kuwa viongozi wa wananchi, mtu asilazimishwe kuwa kiongozi wa siasa wakati mwenyewe anayaona mapungufu yake. Cheo ni dhamana..........Ataharibu vipi?Hao watu wamejazwa viburi na fedha za WALIMU ambao wapo wapo tu
Huko mbele ya safari nadhani kuna haja angalau tukapitisha hataMh Rais imulikeni CWT!!! Kikichotokea nimrejesho kuwa ndani ya CWT Kuna ujujaji wa kutisha, pia napendekeza walimu wakatwe tsh 8000 kama CWT contribution!! Wasikatwe kulingana na ukubwa wa mshahara kama ilivyo sasa
Tunatakiwa tuigawane nchi kila mtu kwenye mji wake awe ni Nchi kamili inayojitegemea. Yaani hawa watu nawatamani wangekuwa kwenye anga zangu lakini ubaya meno sina. Hatuwezi kuwa tunaishi holela tu namna hii utafikiri ni wanyama poriniTukiruhusu kila mtu afanye analoona linafaa Nchi itaenda kweli?
Uteuzi wao umezingatia mambo kadhaa muhimu sana ikiwa ni pamoja na kuonekana kuwa wana rekodi ya kufanya vizuri sana au kutokuharibu kwenye sehemu walizopo sasa. Kwa nini itarajiwe kuwa watakwenda kuharibu walikoteuliwa ilhalii kwenye post ambazo si za uteuzi hawajawahi kuharibu?Kwa hiyo kwako ipi bora?
Aende aharibu au akatae kwenda kuharibu?
Uko sahihi kabisa. Ndiyo maana mamlaka za uteuzi zikawaona wao kuwa wanafaa kuwa ma-DC na siyo mimi au wewe. Vinginevyo kama mimi na wewe tungekuwa tunafaa na si wao, basi wao wasingeteuliwa ila mimi na wewe ndiyo tungekuwa kwenye list hiyoSiyo kila mtu anaweza kuwa DC
Ulikuwa ni mwalimu umeteuliwa kuwa DC. Ikitokea umetenguliwa u-DC, unarudi kuwa mwalimu; hufukuzwi kazi ya ualimu kisa ulikuwa DC halafu ukatenguliwa, hicho kitu hakipoSiasa ni kazi ya muda mfupi, heri ubaki kwenye ajira ya kudumu
Hili halipaswi kujadiliwa kuna watu wanaweza ku-cover hizo nafasi. Ila chawa hiyo ni wake up call kwao.
Sasa wao wameteuliwa na mpaka siku ya uapisho awajatoa sababu yoyote kama walikuwa awataki walitakiwa wamwambie aliewateuaSio lazima kukubaki uteuzi/ cheo, ndio maana mhusika aliyeteuliwa huwa anatakiwa kukiri kukikubali cheo. Kwahiyo unaweza tu kumshukuru aliyekuteua kwa kuonesha imani kwako kisha ukasema haupo tayari kwa majukumu hayo mapya na kwamba hutoweza kuyatekeleza kwa ufasaha, hivyo usije ukamuangusha aliyekuteua.
Kwahiyo unatakiwa kutoa sababu tu za kukakataa uteuzi inaruhusiwa.
Tatizo wahusika awajashukuru wala awajakataaNadhani Kwa nchi za kidemokrasia hili lisingebebe vichwa cha habari.
Hutaki uteuzi anapewa mwingine anayehitaji hakuna haja kuwekeana vinyongo.
Sana sana wahusika walitakiwa washukuru na kukataa kwa heshima
Naelewa unachoongea. Kile kimama huwa hakina vitisho ni kistaarabu sana, sijawahi kukiona kinatishia watu; watu ambao huwa hawatishi wanatisha!Kama hili Jambo limefika mezani kwa Jenista, CWT waandae uchaguzi na segerea wakae mkao wa kupokea wateja.