Serikali kuweka siku ya jumamosi kuwa siku ya Usaili ni kuwakosea Haki Wahitimu waumini wa kisabato

Ni Dk. Bernadine (siyo Bernidine) Mfumbusa Mhadhiri wangu aliyepika vyema katika Somo lake nililolipenda la Critical Thinking / Logical Reasoning mwaka 2009 pale SAUT Mwanza na namkubali hakuna Mfano kwani ana Akili (ni Genius) hadi anakera.
Ahsante kwa masahihisho. Ila wanafunzi wake wa Masters in Mass Communication wanakumbuka alivyotolewa "knockout" siku moja na mwanafunzi wake genius kuliko yeye akiitwa Lubango! Aliichambua "Thesis ya Doctorate" ya Dk. Mfumbusa na mapungufu yake ikaonekana kama gazeti la Kitu tu! Ahahahahaha!!!
 
Huelewi unachokizungumza.

Unajua Moja ya chanzo cha baadhi ya Makundi dini kutaka kuanzisha nchi Zao ni pamoja na Hoja uliyoieleza?
Unafikiri serikali inapotoa Uhuru wa kuabudu ni wajinga?

Waliotunga hayo mambo walikuwa mbele yako maili elfu
Kwani kuna sehemu serikali imekukataza kuabudu siku yako ya sala?

Serikali imeweka siku ya usaili ni jumamosi, Kama mtu ataona ibada ni muhimu kuliko usaili. Aende ibadani.

Serikali haiwezi kuacha kufanya mambo yake kwa kigezo cha dini za watu.

Tanzania ni secular state.
 
Dini Zao zinasemaje. Hiyo ndio Hoja ya MSINGI

Na kwa nini serikali inapewa taarifa wewe ikuume kana kwamba kuna hasara utapata kwa Wasabato kusikilizwa?

Ajabu ni kuwa Waislam wao hutowaona humu wakiandika vitu vya kipuuzi na chuki kama Wakristo.
Hii inashangaza Sana
 
ndiyo maana hii nchi bado ni maskini
 
Kwani kuna sehemu serikali imekukataza kuabudu siku yako ya sala?
Kama ungekuwa unatumia Logical ya kawaida ungeelewa kuwa kuweka Siku ya usaili katika siku ya ibada ungeona ni kumkataza mtu indirectly asiende kuabudu. Ni vile hujataka kuifikirisha akili yako.

Au mtu anaweza kujigawa mara mbili. Wakati huohuo awe Kanisani na wakati huohuo kwenye Usaili?

Serikali imeweka siku ya usaili ni jumamosi, Kama mtu ataona ibada ni muhimu kuliko usaili. Aende ibadani.
Bado unasema serikali haijazuia mtu kuabudu? Unatumia akili yako sawasawa
Serikali haiwezi kuacha kufanya mambo yake kwa kigezo cha dini za watu.

Tanzania ni secular state.

Unajua maana ya Secular State?
 
Tulikuwa na mwenzenu kwenye kazi moja hivi....siku ya Jumamosi halikiwa hataki kufanya kazi lakini ikitangazwa Jumamosi ni siku ya malipo...saa Tatu alikuwa maeishafika kwenye kituo cha malipo....!!!

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Huyo mhuni
 
Acha kuisumbua serikali, serikali haina dini.

Jumapili ndio inatakiwa kuwa siku ya mapumziko na kutumia muda huo wa Jumapili kuyatafakari matendo ya Mungu.

Ijumaa na Jumamosi ni siku za kazi kama ilivyo Jumatatu au Jumanne.
 
Sidhani kama ni fahari kutamba kuwaumiza watu wa Imani nyingine kwa sababu tu wamesimamia misingi ya Imani yao,, na umewataja kabisa waliohusika kuwasitishia masomo. Huyo Padri alipata faida gani. Serikali inatakiwa kulizingatia hili.
Father Dk. Kitima sasa hivi Katibu wa TEC (sijui unaijua?)? Na Dk. Mfumbusa sasa hivi ni Askofu wa Jimbo la Kondoa. Wamepata zaidi ya kile walichokuwa nacho kipindi wanawashughulikia hao Wasabato.
 
Acha kuisumbua serikali, serikali haina dini.

Jumapili ndio inatakiwa kuwa siku ya mapumziko na kutumia muda huo wa Jumapili kuyatafakari matendo ya Mungu.

Ijumaa na Jumamosi ni siku za kazi kama ilivyo Jumatatu au Jumanne.

Unacheo chochote serikalini?
Au umestaafu?
Au unatazamia?
 
[emoji57][emoji57][emoji57][emoji57]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…