Serikali kuweka siku ya jumamosi kuwa siku ya Usaili ni kuwakosea Haki Wahitimu waumini wa kisabato

Sidhani kama ni fahari kutamba kuwaumiza watu wa Imani nyingine kwa sababu tu wamesimamia misingi ya Imani yao,, na umewataja kabisa waliohusika kuwasitishia masomo. Huyo Padri alipata faida gani. Serikali inatakiwa kulizingatia hili.
Wakuu nchi haina dini hii, mimi mitihani yangu mingi sana nimefanya jumapili na wala sikulalamika kwakua nililijua hilo
 
Ingekuwa secular state ingepanga Jumapili pia. Lakini kama Jumapili shughuli za kiserilali zinasimama unasemaje ni secular state ?
 
Kama ungekuwa unatumia Logical ya kawaida ungeelewa kuwa kuweka Siku ya usaili katika siku ya ibada ungeona ni kumkataza mtu indirectly asiende kuabudu. Ni vile hujataka kuifikirisha akili yako.
Nakwambia hivi 👇

Serikali haiwezi kuacha kufanya kazi zake kwa kigezo cha dini za watu.

Kama ibada ni muhimu kwako nenda ibadani.

Kama usaili ni muhimu kwako nenda kwenye usaili.

Yani wewe huna tofauti na muislamu aje kulalamika hapa usaili kuwekwa Ijumaa.

Sasa kila mtu akitaka serikali ifanye vitu kwa kuangalia imani yake, shughuli zitaenda kweli?

Si kila mtu atataka upendeleo kwenye imani yake.

Wewe ndio hutumii logical ya kawaida.
Au mtu anaweza kujigawa mara mbili. Wakati huohuo awe Kanisani na wakati huohuo kwenye Usaili?
Kama kanisa ni muhimu kwako nenda kanisani.

Kama usaili ni muhimu kwako nenda kwenye usaili.

Serikali haiwezi kuvuruga ratiba yake kwa kigezo cha dini au imani yako.
Bado unasema serikali haijazuia mtu kuabudu? Unatumia akili yako sawasawa
Serikali imepanga siku ya usaili kuwa jumamosi.

Halafu wewe unaleta imani zako kwenye mambo ya kiserikali.

Una utimamu kweli wewe?

Au unafikiri serikali ni kanisa au msikiti?
Unajua maana ya Secular State?
Ambacho huelewi ni kipi hapo?

Kwamba Hujawahi kusikia neno secular state.

Au unataka ufafanuzi gani zaidi?
 
Lakini huo ni udini

Waislam nao vivyohivyo watasema hayo.
Walokole nao vivyohivyo!

Unajua matokeo yake?
Waislamu usiwaingize humu. Jiteteeni peke yenu. Waislamu Ijumaa wanaingia kazini kama kawaida. Saa sita na nusu wanaenda Masjid. Ukiwaambia baada ya Swala warudi kazini, hawana noma wala nini. Wanarudi na wanachapa kazi kama kawaida! Ninyi Wasabato ni kimeo!!!
 
Father Dk. Kitima sasa hivi Katibu wa TEC (sijui unaijua?)? Na Dk. Mfumbusa sasa hivi ni Askofu wa Jimbo la Kondoa. Wamepata zaidi ya kile walichokuwa nacho kipindi wanawashughulikia hao Wasabato.
Na ndicho anachosema Heriel. Kumbe kwa kuwashughulikia hao Wasabato kimkakati na kuwatesa kimasomo wakapanda vyeo.
 
Hawa wasabato ni kakundi kadogo sana ka watu wasiojielewa. Yesu alishaweka sabato mpya wao wapowapo tu kufata uongo wa Hellen G White.
 
Ingekuwa secular state ingepanga Jumapili pia. Lakini kama Jumapili shughuli za kiserilali zinasimama unasemaje ni secular state ?
Serikali ndio yenye maamuzi. Kulingana na ratiba zake.

Hata ikiamua kupanga jumapili, Ijumaa au jumamosi ni sawa.

Wewe raia ndio utaamua kipi kina umuhimu kwako, ibada au kazi.
 
🙋‍♂️✍️🎯👍🤝🙏💐🎁
 
Serikali ndio yenye maamuzi. Kulingana na ratiba zake.

Hata ikiamua kupanga jumapili, Ijumaa au jumamosi ni sawa.

Wewe raia ndio utaamua kipi kina umuhimu kwako, ibada au kazi.
Nakubaliana na wewe serikali ina maamuzi ,, Ipange hiyo Jumapili basi hata kwa bahati mbaya tuone. Kama sivyo inakuwa ni mkakati na makusudi.
 
Na ndicho anachosema Heriel. Kumbe kwa kuwashughulikia hao Wasabato kimkakati na kuwatesa kimasomo wakapanda vyeo.
Kipindi hicho nikisoma hapo kina "Mzee" mmoja Msabato akivaa mashati meupe pee na tai. Very smart. Yeye baada ya kuona hapo SAUT mambo ya Kisabato yamekuwa magumu, aliomba kuhamia Chuo Kikuu cha Wasabato kile Cha Arusha.

Sasa hivi amestaafu baada ya kuwa Mtumishi Mkubwa tu serikalini.
 
Nakwambia hivi 👇

Serikali haiwezi kuacha kufanya kazi zake kwa kigezo cha dini za watu.

Kama ibada ni muhimu kwako nenda ibadani.

Kama usaili ni muhimu kwako nenda kwenye usaili.
Ibada sio tuu muhimu kwa mtu binafsi Bali hata kwa Serikali yako hiyo ambayo wewe unasema ni Secular lakini hujui maana hata ya hiyo istihali.

Wewe unaposikia viongozi wa nchi wanaposimama jukwaani wanasema waombewe, watu wasali, shuleni pawepo na vipindi vya Dini unaelewa nini au akili yako huwezi kung'amua na kuchambua vitu?

Yani wewe huna tofauti na muislamu aje kulalamika hapa usaili kuwekwa Ijumaa.

Muislam yeye dini yake inasemaje kuhusu kuabudu ijumaa?

Sasa kila mtu akitaka serikali ifanye vitu kwa kuangalia imani yake, shughuli zitaenda kweli?

Vitu vinaenda pakiwa na utaratibu mzuri.
Wewe ndio huelewi.
Sijui kama uliwahi kuwa kiongozi hata wa Darasa.

Au siku ukipata Mke na watoto utaelewa uongozi ni kitu gani.
Nchi inaongozwa kwa kufuata taratibu, Kanuni na Sheria
Hizo Sheria ndio zinaweka utaratibu mzuri kutimiza mahitaji ya watu wote yawe kwa HAKI.

Wewe huelewi hilo
Si kila mtu atataka upendeleo kwenye imani yake.

Hatutaki upendeleo.
Tunataka HAKI

Hujui maana ya Secular na huenda umekariri ndio maana nikakuambia ueleze jinsi unavyoelewa na sio ui-copy huko kisha uiweke hapa.

Eleza unaeewaje ukisikia istihali Secular State
 
Hawa wasabato ni kakundi kadogo sana ka watu wasiojielewa. Yesu alishaweka sabato mpya wao wapowapo tu kufata uongo wa Hellen G White.

Huwezi kuta muislam anatoa maoni hivi.

Wakristo ndio hujitambulisha hivi.
Unajua maana yake?
 
Dr. Ulisubyisa Mpoki, Chief Executive Officer of the Muhimbili Orthopaedic and Neurosurgery Institute (MOI), aligoma kufanya mitihani siku ya sabato wakati anasoma chuo miaka hiyo. Igeni mfano wake.
 
Samahani,naomba ushahidi kuwa Jumamosi ni siku ya saba na ni siku ya sabato.Jibu ukitumia 'common sense' plus fikra tunduizi.Zingatia neno Jumamosi

Vipi wale wanaobadu Ijumaa, Jumapili,Jumatatu n.k?? Punguza ubinafsi na kujiona ninyi ni so special!
Unaijua katiba ya nchi? Unajua kama katiba inatambua na kuheshimu dini za raia wa Tz?
Lama hujui pita kule
 
Mwongozo wao unawataka wakaswali mida wa swala lakini wengine wanakua kwenye majukumu wanashindwa. Wasabato punguzeni kujidekeza utadhani mbingu mmeandikiwa nyie tu kumbe hellen na kikundi chake ndo watunga sheria zote hizo
Kama wewe ni Mkristo na unasoma Biblia utazikuta hizo sheria kwenye biblia. Hazikuanzishwa na Ellen.
 
Dr. Ulisubyisa Mpoki, Chief Executive Officer of the Muhimbili Orthopaedic and Neurosurgery Institute (MOI), aligoma kufanya mitihani siku ya sabato wakati anasoma chuo miaka hiyo. Igeni mfano wake.

Watagoma Mpaka Lini?
Unajua hiyo ni Haki ya Watanzania wote, kwa nini serikali isiangalie namna Bora ya kufanya ili kutoa Haki kwa wote?

Unataka kusema serikali inakosa Mbinu,maarifa ya kujua cha kufanya?
Au ni Tabia ileile ya kutokujali, kudharau, kudhulumu na kuona wengine hawana Haki ya Kupata Fursa Sawa na wengine kutokana na Itikadi Zao?

Huo ni UONEVU
Huo ni USHENZI
Huo ni ukandamizaji
 
Hujatumia common sense, kama ungetumia hizo siku plus kalenda ni utashi wa watu na siyo Mungu.Onyesha sehemu yoyote Mungu anataja majina ya siku.
Kwani mkuu wewe siku zako unazitofautishaje? Au zote ni Jumatatu? Na ni mfumo gani umeamua kufuata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…