Serikali kuweni makini; inakuaje mtoto ana A ya math, B ya Chemistry, B ya biology na B ya Physics halafu mnampangia combination ya Art?

Mbaya zaidi dogo hakuomba combination yoyote ya arts katika maombi yake ya uchaguzi (selform)..... machaguo yOte matano ye ni PCM, PCB AU CBG.

Kijana amepambana kwenye shule yake ya kata hadi amefikia hapo ili ndoto zitimie halafu mnataka kumsumbua na kumuathiri kisaikolojia kama hivyo.

Najua kuna kubadilisha, lakini hilo ni mchakato na kwakuwa amepelekwa shule isiyo na hizo combinations maana yake itamlazimu kugharamika huyo katika kutafuta shule nyingine, kuna wakuu miungu watu; maringo, rushwa n.k.

Halafu kama machaguo ya mtoto, ambayo hufanyika kwa kuwahusisha walimu pamoja wazazi/walezi, hayazingatiwi kuna haja gani ya kujazishwa?

Inakera sana!
Tupe matokeo ya Arts subjects na combination yake.
Huenda huko ana A zote.
Arts subjects ni masomo mazuri sanaaa
 
Hayo Mambo yalisha pitwa na wakati bro siku hizi hata ukiwa na zero zote Bado unaweza kusomea urubani au udokta unatakiwa tuu kuwa na hela zama zinabafikika
 
Anamaanisha labda ufaulu ni mkubwa AAA zipo nyingi zimejaza nafasi. Hapo ni kupeleka private tu ili mtoto apate kitu anachoatahili, kitu kizuri.
Siamini kwa masomo ya sayansi nafasi zimejaa kwa mtu mwenye ufaulu huo.
Akienda private mnamkosesha mkopo ukizingatia katoka shule za kata huko huyo ni akili kubwa.
 
Hayo Mambo yalisha pitwa na wakati bro siku hizi hata ukiwa na zero zote Bado unaweza kusomea urubani au udokta unatakiwa tuu kuwa na hela zama zinabafikika
Si kweli kama umefeli masomo ya sayansi yote Kuna kuwa na ugumu kidogo kupata admission kozi za urubani au udaktari.
Tuwekee hapa ushahidi chuo kinachopokea mtu mwenye sifa hizo kwenye udaktari au urubani.
 
Aliyefaeli hivyo ataweza kufanya hesabu module ya Aerodynamics?
Atawe kukokotoa Mass and balance kutafuta center of gravity ya aircraft?
Ataweza kukokotoa hesabu za wind speed na indicated speed?
Au umeongea kishabiki tu?
Nilidhani upo field ya Aviation kutokana na ID yako hapa JF.
 
Mbaya zaidi dogo hakuomba combination yoyote ya arts katika maombi yake ya uchaguzi (selform)..... machaguo yOte matano ye ni PCM, PCB AU CBG.

Kijana amepambana kwenye shule yake ya kata hadi amefikia hapo ili ndoto zitimie halafu mnataka kumsumbua na kumuathiri kisaikolojia kama hivyo.

Najua kuna kubadilisha, lakini hilo ni mchakato na kwakuwa amepelekwa shule isiyo na hizo combinations maana yake itamlazimu kugharamika huyo katika kutafuta shule nyingine, kuna wakuu miungu watu; maringo, rushwa n.k.

Halafu kama machaguo ya mtoto, ambayo hufanyika kwa kuwahusisha walimu pamoja wazazi/walezi, hayazingatiwi kuna haja gani ya kujazishwa?

Inakera sana!
Serikali sio wajinga kiasi hicho.

Kama watoto walipewa mpaka muda wa ziada wa kubadilisha tahasusi wajaze wanazozitaka iweje huyo kijana apangiwe tahasusi sio wakati hata alama zake ziko vizuri?

CHAI.
 
Hiyo ni mbaya sana na haikubaliki. very unfair, very unethical!!!!!
 
Najiuliza kuna haja gani ya kujaza selform,kimbembe sasa hivi kila mtu anataka kuwa daktari
 
Serikali sio wajinga kiasi hicho.

Kama watoto walipewa mpaka muda wa ziada wa kubadilisha tahasusi wajaze wanazozitaka iweje huyo kijana apangiwe tahasusi sio wakati hata alama zake ziko vizuri?

CHAI.
Dah, we jamaa nilikufikiria kuwa ni mtu mmoja very smart upstairs. Hivi nije hapa jidanganye jambo kama hili ili iweje?!!!!!!!! Mbona mnakera sana nyie wakati mwingine?!!!!! Au ndo wachaguzi wenyewe nyie?!!
 
Mwingine aliomba kwenda chuo kama option yake ya kwanza, serikali imempeleka advance, yaani tafrani
 
Siamini kwa masomo ya sayansi nafasi zimejaa kwa mtu mwenye ufaulu huo.
Akienda private mnamkosesha mkopo ukizingatia katoka shule za kata huko huyo ni akili kubwa.
Sasa mtoto anataka sayansi na anaiweza atasoma arts? Hapo ni kufanya kazi tu kwa bidii mtoto umuwezeshe.
 
Si kweli kama umefeli masomo ya sayansi yote Kuna kuwa na ugumu kidogo kupata admission kozi za urubani au udaktari.
Tuwekee hapa ushahidi chuo kinachopokea mtu mwenye sifa hizo kwenye udaktari au urubani.
Utamsikia. Atasema ni Polisi😀😀
 
Inaumiza na kupoteza matumaini Kwa Kiasi kikubwa
Aende shule aliyopangiwa, aombe uhamisho kwenda kwenye shule yenye masomo anayotaka kusoma
Tofauti na hapo, sishauri sana kumpeleka private. Ni Bora tu kumpeleka college Moja kwa Moja akasoma kile anachopenda
 
Back
Top Bottom