Sasa mbona bashungwa alitumia chopa kuchungulia maafa, Lakin hakuonyesha maafa, akajionyesha yeye mwenyewe akiwa ndani ya chopa,Mawqziri ni wanasiasa, si wanajiografia, wapigapicha wala walimu.
Hawawezi kuacha nafasi ya kujipiga picha wao wapige picha ya mlima kukufundisha wewe.
Uchumi ukichanganya, kina Millard Ayo na wenzake watapata chopa nankwenda kupiga picha.
Vilevike, kwa sasa inawezekana ni mapema sana kupata picha za juu kwa sababu watu wanatafiti kilichotokea ni nini, wasije kwenda kupiga picha huko wakakutana na ajali nyingine.
Jibu la swali lako lipo katika post uliyoinukuu.Sasa mbona bashungwa alitumia chopa kuchungulia maafa, Lakin hakuonyesha maafa, akajionyesha yeye mwenyewe akiwa ndani ya chopa,
Kwa hiyo wewe Una msaada Gani , ili nizipate hizo pichaJibu la swali lako lipo katika post uliyoinukuu.
Umeisoma na kuielewa au umeinukuu tu?
Waziri ni mwanasiasa, interest yake ni kukuonesha wewe mwananchi kuwa yupo katika eneo la maafa.
Interest yake si kukufundisha wewe jiografia.
Huelewi nini hapo?
😂😂😂😂😔 nashukuruni
😂😂😂asante sana mkuu💆Jf kuna wathengerema,sikutegemea kama to yeye nae ni miongoni mwao
Wala,mi nimetulia tu hapa mkuuNever mind
Kiranga tunza heshima Yako bana! Kwani lazima watu wapande kwa miguu kwa Dunia ya leo iliyojaa Kila aina ya teknolojia?Mlima ndiyo kwanza umetupa mudslide, watu wanasafisha miundombinu chini bado, wewe unataka watu wapande juu wakapige picha za kukuonesha wewe?
Alafu ni member ninaemkubali hapa jf sasa nashangaa leo sijui amekuaje!Kiranga atakuwa ni muha huyu
Kuna muandishi mmoja wa Kiingereza nilikuwa napenda sana kumsoma, alikuwa anaitwa Christopher Hitchens.Kwa hiyo wewe Una msaada Gani , ili nizipate hizo picha
Asante sanaKuna muandishi mmoja wa Kiingereza nilikuwa napenda sana kumsoma, alikuwa anaitwa Christopher Hitchens.
Hitchens alitoa hadithi ya jinsi alivyoanza uandishi.
Alisema, yeye alikuwa anapenda sana kusoma habati za kimataifa, hususan za vita.
Lakini, alikuwa anahuzunika sana, kwa sababu karibu kila habari aliyoisoma aliona ina mapungufu mengi sana. Akasema hivi hakuna muandishi wa habari mzuri anayeandika mambo kwa kina? Akaona uandishi mzuri anaoutaka kama haupo.
Akasema sawa, basi kama uandishi ninaoutaka siupati kwa watu wengine, nachukua jukumu hili mimi kuwa muandishi nankuandika habari kwa jinsi ninayoitaka mimi.
Hitchens alienda kuwa "war correspondence" muhimunsana wa magazeti mengi makubwa, watu walipenda sana jinsi alivyoandika, waliona tofauti kubwa sana jinsi alivyoandika.
Sasa, na wewe mwenzetu, inawezekana una kipaji kikubwa sana cha kuona kitu kinachokosekana ambacho labda wengi tunakihitaji, lakini hatujakijua tu kutokana nankuishi kwa mazoea.
Sasa, ninekuoa hiyo habari ya Christopjer Hitchens upate changamoto ya kuanza kuifanya hiyo kazi ambayo unaona haifanywi.
Kazitafute mwenyewe, anzisha biashara au organization ya kazi hizo, anzisha website, tafuta wafadhili wanaopenda mambo hayo. Ifanye hiyo kuwa ni passion yako.
Unaweza kuja kuwa Christopher Hitchens au Sir David Attenborough wetu.
Mara nyingine, if you see a gap in doing something, and you want that something to be done well, do it yourself.
Jielimishe, andika project plan, present kwa watu watakaokupa funding, mfano www.kiva.org halafu piga kazi.
Tunalalamika ajira hakuna, kumbe ajira zenyewe ndiyo hizi hizi passions zetu.
Nakuona kama una passion sana na hizo picha.
Chukua changamoto hiyo na ifanyie kazi.
Mkuu,Kiranga tunza heshima Yako bana! Kwani lazima watu wapande kwa miguu kwa Dunia ya leo iliyojaa Kila aina ya teknolojia?
Mkuu ndo maelezo yote hayoMkuu,
Kama unaniheshimu sana, na hiyo heshima inaelekea kuninyima uhuru wangu wa kujieleza, naomba uiondoe hiyo heshima kwangu, unibakishie uhuru wangu wa kujieleza.
Nikiambiwa nichague kati ya upande mmoja kuheshimiwa sana na watu hapa JF, au upande wa pili kuwa na uhuru wa kujieleza ninavyotaka, nitaamua kuwa na uhuru wa kujieleza ninavyotaka.
Kwa hivyo, usifanye heshima iwe mnyororo wa kuninyima uhuru wa kujieleza.
Kwenye post yako.
Kwani wapi nimesema wapande kwa miguu?
Watanzania wengi wanaodai dai vitu kwa mtindo wa thread hii, wana tatizo la kutaka kufanyiwa kazi. Yani wanataka wengine wafanye kazi, wao wapate faida tu.
Muimbaji wa muziki wa reggae Anthony B aliimba.
"Nobody wants to plant the corn
Everybody want to raid the barn
Who are you going to blame it on
When it is a next man you are depending on?"
Yani.
"Hakuna mtu anayetaka kupanda mahindi
Kila mtu anataka kuvamia ghala na kuchukua mahindi
Utamlaumu nani ikiwa unategemea mambo yafanywe na mtu mwingine tu?"
Hii inaweza kuwa fursa yako kuanzisha kitu muhimu ambacho hakipo, watu wanakihitaji na ni cha manufaa kwa jamii.
Lakini, na wewe usichangamkie hiyo fursa, unategemea watu wengine wakufanyie kazi.
Matokeo yake nchi nzima mnalaumiana, kila mtu anategemea mwingine afanye kazi, lakini yeye hataki kuifanya hiyo kazi.
View: https://youtu.be/k-hCpJ2e30k?si=QLBCYySIKN7My91p
View: https://youtu.be/1S8Ha__cJgY?si=X9GfvMO0QlR4XPnw
Hapana. Hayo si yote. Hiyo dibaji tu.Mkuu ndo maelezo yote hayo