Kuna muandishi mmoja wa Kiingereza nilikuwa napenda sana kumsoma, alikuwa anaitwa Christopher Hitchens.
Hitchens alitoa hadithi ya jinsi alivyoanza uandishi.
Alisema, yeye alikuwa anapenda sana kusoma habati za kimataifa, hususan za vita.
Lakini, alikuwa anahuzunika sana, kwa sababu karibu kila habari aliyoisoma aliona ina mapungufu mengi sana. Akasema hivi hakuna muandishi wa habari mzuri anayeandika mambo kwa kina? Akaona uandishi mzuri anaoutaka kama haupo.
Akasema sawa, basi kama uandishi ninaoutaka siupati kwa watu wengine, nachukua jukumu hili mimi kuwa muandishi nankuandika habari kwa jinsi ninayoitaka mimi.
Hitchens alienda kuwa "war correspondence" muhimunsana wa magazeti mengi makubwa, watu walipenda sana jinsi alivyoandika, waliona tofauti kubwa sana jinsi alivyoandika.
Sasa, na wewe mwenzetu, inawezekana una kipaji kikubwa sana cha kuona kitu kinachokosekana ambacho labda wengi tunakihitaji, lakini hatujakijua tu kutokana nankuishi kwa mazoea.
Sasa, ninekuoa hiyo habari ya Christopjer Hitchens upate changamoto ya kuanza kuifanya hiyo kazi ambayo unaona haifanywi.
Kazitafute mwenyewe, anzisha biashara au organization ya kazi hizo, anzisha website, tafuta wafadhili wanaopenda mambo hayo. Ifanye hiyo kuwa ni passion yako.
Unaweza kuja kuwa Christopher Hitchens au Sir David Attenborough wetu.
Mara nyingine, if you see a gap in doing something, and you want that something to be done well, do it yourself.
Jielimishe, andika project plan, present kwa watu watakaokupa funding, mfano
www.kiva.org halafu piga kazi.
Tunalalamika ajira hakuna, kumbe ajira zenyewe ndiyo hizi hizi passions zetu.
Nakuona kama una passion sana na hizo picha.
Chukua changamoto hiyo na ifanyie kazi.