Serikali: Makala ya BBC haina ushahidi. Tutachukua hatua kulinda uhuru, heshima na usalama wa nchi

Zamani ilikuwa congo sudan elitrea

Sasa hivi tanganyika aaah nyie **** mmetuharibia nchi sana. Demokrasia inazidi kuzorota na kuzoroteshwa. Viongozi wastafu wapo wanaangalia tu. TISS mpo kwa ajili ya maslahi gani?

it is what it is.....kuna wakati watu wanaangalia ili tu waje waseme tulijua
 

Hao watanzania ni watanzania gani?
 
Wale wa Commonwealth sijui EU msingewafukuza na kuwazuia kuingia nchin. Mliwazuia hao hao kuhoji pande zote mbili, wakarudi.

Leo mnabana pua hamjapewa nafasi,, Ipi ????

Miaka yote tangu uhuru 09/12/1961 kuacha 1964, ilikuwa ukimuona mwanajeshi au vifaru, na magari ya kijeshi jua wanaenda porini mazoezini au vifaa vinaenda mipakani au kuhamishiwa kambi ingine.

Leo hii wanajeshi na askari wametapakaa mitaani utafikiri tuko vitani rasmi. Hatukuyaona haya.

Waropokaji wakiwatisha kidogo mnajaa mitaani na mavifaa utafikiri mtu kavaa Maputo. Hatukuyaona haya.

Miaka ya nyuma ungeweza kumwona hata Waziri mkuu alfajiri na mlinzi mmoja anafanya mazoezi.

Leo hii ving'ora kila gari, kila Mtawala anajihami, ulinzi utadhani Zaire ya Mobutu. Askari haulizwi njia na mpitaji, tena. Hatukuyaona haya.

Chuki kwa vyombo vya dola vyote ni kubwa, japo tunajifariji na kucheka kwa maumivu. Hatukuyaona haya.

Tanganyika imeharibika kiasi ambacho ni damu za watu tu zinazoongea mengi vichwani mwa watu. Kuna watawala na mamluki wasio jali lolote,, kuna waliopoteza ndugu, kuna waliotumika kuuwa, kuna wanaoetea mauaji na kuna walioamua kukaa kimya na kumwachia MUNGU.

Maskini Nyerere angefufuka, aone. Tanganyika yangu kwa heri upendo, kwa heri furaha, kwa heri amani ya kweli, kwa heri uzalendo.
 
Zamani ilikuwa congo sudan elitrea

Sasa hivi tanganyika aaah nyie **** mmetuharibia nchi sana. Demokrasia inazidi kuzorota na kuzoroteshwa. Viongozi wastafu wapo wanaangalia tu. TISS mpo kwa ajili ya maslahi gani?
Siku nilipoona nchi imezama rasmi ni pale Samuya alipowaalika CNDD-FDD ya Burundi kwenye uapisho feki kule maporini kwenye kambi ya jeshi.

Ukisoma historia ya CNDD-FDD halafu mtu aseme atakua nao bega kwa bega unajua ni kwamba nchi imepiga hatua 10 nyuma.
 
Kila siku wanadi hivyo. Msigwa si awaombe kwenda kuongea mao na kueleza upande wa pili.

Hivi hata hiyo ya Lissu kupigwa risasi na serikali kudhindwa kufanya upelelezi mayo bado wanajitetea....!?
CNN ilivyotaka kupata CCM's side of the story immediately baada ya massacre 29th-Oct-2025 walikwepa lakini baada ya documentary kuwa released wakaanza kumshambulia Larry Madowo personally mpaka wakafikia kusema ni figisu za Wakenya ilhali yeye Larry pale CNN ni muajiriwa tu na ile ilikuwa ni habari ya CNN iliyohakikiwa na CNN kabla ya kurushwa hewani. CCM/Serikali/Grey Msigwa walilialia kuwahadaa wananchi wakati ni wao waliikwepa CNN wakiogopa maswali yasiyo ya Kichawa.
Haiwezekani BBC waharibu reputation yao kutoa habari ambazo hazijahakikiwa, CCM/Serikali/Msigwa/Samia wanajulikana kwa kubobea katika uongo, giliba na kukanusha ukweli kipumbavu hivyo hata hii habari kuikanusha Msigwa amelenga wapumbavu wenzake ambao anaamini watamuamini yeye zaidi ya wanavyoiamini BBC.
Msigwa hauna akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…