Serikali: Mikoa ya Tanga, Arusha, Mwanza, Pwani na Geita ina viashiria vya Ugaidi

Serikali: Mikoa ya Tanga, Arusha, Mwanza, Pwani na Geita ina viashiria vya Ugaidi

Hii sheria kikwete aliishtukia, akakataa kuikubali na kuisaini, magu nae aligoma kuisaini, le munakubali kirahisi hivi?
Unajua waislamu wanaenda kunyanyasika sana na hii sheria?
Na matokeo yake ndio mutazalisha sasa magaidi sio kwa ajili ya dini bali kwa sababu ya dhulma zitazofanyika
 
Sasa kwanini mkamuachia gaidi Mbowe wakati gaidi Sabaya mnamuacha analia mahakamani?
Sii mbowe tu magaidi na wauaji wengi wamepata msamaha, na haijaanza jana Wala juzi Ni utaratibu upo miaka mingi.

Sabaya nae muda ukifika atapata msamaha
 
Hizohizo mahakama mbona mmeenda kuwashtaki akina mdee?

Huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani, akina Mdee ndio wameenda kuishtaki CDM ili wasifuvuliwe ubunge wa mchongo. Nitajie popote CDM walipoenda mahakamani baada ya uchaguzi wa kihayawani wa 2020.
 
Hii sheria kikwete aliishtukia, akakataa kuikubali na kuisaini, magu nae aligoma kuisaini, le munakubali kirahisi hivi?
Unajua waislamu wanaenda kunyanyasika sana na hii sheria?
Na matokeo yake ndio mutazalisha sasa magaidi sio kwa ajili ya dini bali kwa sababu ya dhulma zitazofanyika
Kumbe unajua magaidi yanatokea wapi..sasa jiandaeni..vyema.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nikiangalia video hii iliyopigwa mwaka 1999, halafu nikiingia mtaa naona kuna utofauti mkubwa sana.



Nini kimewabadilisha waTanzania na kujihesabu kwanza wao ni wa imani fulani badala ya wao kujivunia utanzania na umatumbi wao.


Je badiliko la waTanzania kuishi katika nchi ya kufikirika iliyochagizwa na imani zao za kidini imetoka wapi.


Utaifa kufa, nini chanzo chake? na mikakati zaidi mbalimbali zaidi ya hii ya kulazimisha sheria kutumika ni ipi ili kusawazisha hali hii ya kujibainisha na imani za kuja kwa manowari na majahazi.


Ipo haja ya kujitambua sisi na wale wao waliokuja kututawala kifikra na kitamaduni bila kusahau utumwa, ukoloni mkongwe na ukoloni mamboleo


Source : d'jarell messa
 
Inchi iliyoshindwa kupambana na panya road, inataka ipambane na magaidi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Waulize ndugu zako walio taka kujifanya mwamba hapo rufiji na ikwiriri wako wapi sasa.

Panya road ni inshu nyingine na magaidi ni inshu nyingine kila mmoja ana namna ya kupambana naye.

#MaendeleoHayanaChama
 
Samora Machel : Ukoloni wa kiFikra



Katika hotuba yake motomoto kuhusu kutawaliwa, alihoji vipi mwafrika aliyetawaliwa na mfaransa akajiona bora kuliko mwingine kwa kuwa Ufaransa wana tamaduni bora zaidi ya uandishi wa mistari ya mashairi ya mapendo kwa umahiri wa kisomi.


Samoro Machel anazidi kuwaza hata wale waliotawaliwa na muingereza wajiona wao ni bora kwa vile Uingereza ilitawala nchi nyingi zaidi na inasemekana ni wazungu 'wastaarabu' zaidi.

Samora Machel anatuasa ingawa Portugal ni nchi masikini zaidi ktk ulaya lakini ni nchi iliyoendekeza ukoloni kama Ufaransa, Uingereza na Ureno / Portugal na sifa za nchi zote hizo za ulaya ni kuwa ziliendekeza ukoloni.

Samora Machel anapigia mstari neno ukoloni na kuwa ukoloni ni unyama hauna utu hivyo kujisifia wewe ni zao la ukoloni huu au ule wenye hadhi ya juu ni kukosa fikra sahihi.

Hivyo maneno ya Samora Machel anasisitiza tuamke na kuwa mapambano lazima yaendelee (2022) dhidi ya ukabila, ujinga, maradhi, njaa, ushirikina na mawazo potofu ya kukumbatia ukoloni wa aina yoyote.

Anamalizia kuwa ukoloni wowote hauna usafi wa kujivunia kwani ni Ukoloni unaogandamiza jamii zingine na kuzigawanisha.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani Eng. Masauni Yusuph Masauni ameitaja mikoa hiyo kuwa imekuwa na matukio ya kukamatwa kwa watuhumiwa waliokimbia baada ya kufanya vitendo vya ugaidi katika nchi jirani.

Pia, kuna dalili ya kuenea kwa itikadi za msimamo mkali zinazopelekea watu kuhamasika na kujiunga na vikundi vya kigaidi nje ya nchi hali inayoweza kusababisha vitendo vya kigaidi nchini.

Leo Septemba 19, 2022 Bunge limeridhia na kupitisha Itifaki ya mkataba wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Ugaidi wa Mwaka 2004, mkataba huo umecheleweshwa kutekelezwa nchini kwa miaka 18.
Hawa watu wa ajabu kweli. Mbona hawajaorodhesha Kilimanjaro, Dar es salaam na Dodoma ambapo Mbowe anakuwepo mara kwa mara? Si walisema mh. Mbowe ni gaidi!
 
Waulize ndugu zako walio taka kujifanya mwamba hapo rufiji na ikwiriri wako wapi sasa.

Panya road ni inshu nyingine na magaidi ni inshu nyingine kila mmoja ana namna ya kupambana naye.

#MaendeleoHayanaChama
Kama ulikua hujui ransom inatoka mtindo mmoja usione watu wametulia bure,
Wanatulizwa jombaa
Achana na hizo habari kabisa, nyie endeleeni kupambana na panya tu,
Hao jamaa ni next level achana nao na wala usiombee watuingilie hapa tutatafutana
 
Back
Top Bottom