Serikali mnataka tufanye kazi gani?

Ukiingia mtaani kuiba, kukaba na kufanya mambo ya ovyo sawa, ila omba wananchi unaowaibia, kuwakaba na kuwafanyia mambo ya ovyo wasikubananishe. Ila mimi naomba sana wakubananishe tena wakiwa na mafuta ya petroli na kiberiti! Ahahahahaha!!!
Siibii wananchi wenzangu maskini walala hoi ... Na deal na hao hao big fishes
 
Pole yako katika maumivu hayo.

Lakini kuna machache ambayo bado ninakudharau kabisa kwa kuyasema hapa. Inaonyesha katika kuchanganyikiwa kwako kwa akili, bado hujajifunza lolote maishani mwako; hata baada ya mkasa ulio kukumba.

Kwanza:
Sasa nauliza hivi tukiingia mtaani na kuanza kuiba , kukaba au kufanya mambo ya hovyo mtatufanya nini...
Hao utakao wakaba, ndio watakao kusaidia na kuondoa ujinga wako ulio kuwa nao na hao CCM kabla hawaja kuvuruga?
Pili: unavyo jieleza hapa ni wazi kabisa, kesho bwana 'Abdul' akimtuma mtumishi wake kukutembelea hapo ulipo; wewe ni mtu wa kununuliwa na kusahau kila jambo baya ulilo tendewa. Watu wa aina yako ndio wanao likwamisha sana taifa hili.

Tatu: pamoja na lawama hizo unazo watupia hao walio kulea na kuwapenda kabla hayajakufika; wewe mwenyewe uliona wapi watu wajifanyie tu shughuli zao bila ya taratibu za kufanya shughuli hizo. Wewe ulitaka tu, wakuache undelee kujifanyia utakavyo mwenyewe? Pamoja na ubovu wao, lakini hili, hata kama wamelifanya kipuuzi, walikuwa na haki ya kukufuata ili nawe uchangie maendeleo ya nchi hii.

Nashindwa kabisa kumhurumia mtu kama wewe.
 
tukiingia mtaani na kuanza kuiba , kukaba au kufanya mambo ya hovyo mtatufanya nini...

Suluhu ni kuingia mtaa kufanya maandamano ya kupinga hali ngumu ya kiuchumi, gharama za maisha, kodi na kugandamizwa kisiasa kwa kutopewa nafasi mchague viongozi mfano Uchafuzi wa uchaguzi 2024 n.k kiasi mnaumia bila kusikilizwa, huku serikali ya chama dola kongwe tawala inasema ni serikali sikivu

Hakuna sababu ya kuingia mtaani tuanze kukaba masikini wenzetu, wakati tunajua uzi huu lawama zote ni sera mbovu za serikali ya CCM

Tukabiliane na serikali hii moja kwa moja badala ya kutumia njia za kuzunguka kuibiana sisi wenyewe tulio wengi kuliko watawala wachache walafi walioshindwa kuongoza nchi.
 
Watu wana iba pesa ambazo hadi zina wazidia wanakosa pa kuweka na bado wanaendelea kuiba.. leo nme ona Kariakoo watu wana bebewa bidhaa zao zinarushwa kwenye lorry seriously
 
Sawa
 
Na hivyo VIBALI ukiamua ufuatilie, utapigishwa kwata nenda rudi kibao,...kila ukienda watu wapo ofisini wanajadili mpira na wanakujibu njoo kesho kitu fulani hakipo,...hawajali kama umetumia nauli,.....mi biashara yangu nilifungua bila reseni kisa huu UJINGA....
 
Nakubaliana na wewe mkuu
 
Its too sad mkuu
 
Sikutaka na wala sifurahishwi na hali iliyo kupata; lakini naomba tu ujitafakari mwenyewe. Na wala siyo rahisi kwangu kukuandikia maneno kama hayo. Hali ni ngumu sana kwa kila mmoja wetu, labda kasoro ya hao walio kufanyia hayo.
Nashukuru mkuu kwa ushauri wako...
Pia nimejifunza hapa shukrani sana.
 
Ndo maana wanapigwa
 
Wanyime watu elimu,wanyang'anye kipato,UTAWATAWALA MILELE NA MILELE KWANI WEWE NDIYE UTAKUWA MMILIKI WA KILA HITAJI LAO,WATALAZIMIKA KUKUIMBA NA KUKUSIFU WEWE TU ILI WAPATE KITU KIDOGO.
Maisha ya chawa hayo
nina gunia zaid ya elfu3 za alizeti, mahindi, maharagwe, ufuta na mbaazi gentleman
Unauzia katika masoko gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…