Serikali msijisahau katika hili la daktari kumtibia mtu wa jinsia tofauti na yeye

Serikali msijisahau katika hili la daktari kumtibia mtu wa jinsia tofauti na yeye

Wagonjwa wengi ni wanawake na madaktar wengi ni wanaume, so, hamna namna.
 
Kwa nini polisi katika upekuzi kumpekua mtuhumiwa hutumiwa wanawake,mbona hata polisi mwanaume asitumike kumpekua mhalifu wa kike ?

Unaonaje juu ya polisi wa kiume kumpekua kila sehemu mtuhumiwa wa kike ?
Ishu ya afya inahusu uhai wa mtu, it's do or die sasa ukileta mambo ya dini, aibu itakua ni kupoteza muda.
 
Hii mbona kawaida tu,japo haijazoeleka.Utakuta baba mtu mzima ana ugonjwa wa zinaa anayemtibu ni binti mdogo,wakati mwingine analishikashika dushe kulichunguza ili apate pa kuanzia kutibu. Au unampeleka mtoto wa kiume hospitalini kufanyiwa suna unakutana na daktari wa kike,anamchunguza mtoto kadushe chake ndio anaandika maelezo tayari mtoto afanyiwe suna
 
Kuwepo wa kike na kiume ni Sheria kabisa na Wala sio tatizo pia unaficha nini huko ndani kisichojulikana, na hyo ya police mbona hukagua watu hadharani wakiwa wanaona nadhani hujawahi kukutana na Hawa mapolice wetu
Sheria gani? Badala ya kuchagua hospitali mjengewe nyinyi mkachagua "jumba la dhahabu" ndo mtulie mkiwa mnatibiwa busha na Sr. Consolata!
 
Kinachouma mama mzazi anaenda hospitali anakutana na daktari ambaye ana umri kama wa mimi mwanae alafu madaktari wa kike wapo kabisa.

Kuna mama wa kipemba wakati anajifungua alitaka kuja daktari wa kiume, basi mama mpemba akamuuliza "uko radhi kuchungulia tv ya mamayo wee "?

Daktari akaenda mbio
Chukulia Dr aliyemzalisha Poshqueen, mzigo wote ule🥰😍😋
 
Unapotetea uhai unajali Mambo ya aibu?
Huu NI ujinga kabisa
Mbele ya kifo unasema naona aibu!!!!
Madaktari NI wachache kwanza lazima muelewe
K
Kigezo kinachoangaliwa pale ni ujuzi na sio jinsia.

Anaweza akawa daktari jinsia ya kiume ndio ana weledi na hiyo kazi kuliko hawa assistant nurse ambao kazi yao ni kufuata maelekezo nini wafanye kutoka kwa huyo daktari bingwa.

Sasa We utakubali kumuacha dada yako au mama yako asifanyiwe operation azae eti kwasababu ya daktari kua ni mwanaume?
Kwa uhakika madaktari wengi ambao wamesomea mambo yahusuyo akinamama (gynecologist) ni wanaume. Msisitizo uwekwe ili wanawake wasomee fani hii ili kuwatibu akinamama ambao huogopa kutibiwa na ME . Yupo mkunga mmoja ambaye ni ME amejijengea jina kwa kuwazalisha wanawake wengi na pia kwa kuwa na lugha ya upole awapo katika shughuli hiyo ngumu ya kuzalisha. Waulizeni KE kuhusu kejeli wazipatazo toka kwa baadhi ya wakunga wa jinsia yao wakati wa kujifungua.
 
Kuwepo nesi wa kike pembeni bado sio ishu.

Mbona polisi wa kike anapomkagua mtuhumiwa wa kike haitakiwi polisi wa kiume awepo bali huwa ukaguzi unafanyikwa wakiwa wawili tu ?
Sasa kumkagua mtuhumiwa ni ISHU??
usimfananishe afya na mambo ya kijinga, btw kila taaluma Ina miiko yake na taratibu zake.
 
Wakuu naomba niipongeze serikali kwa jitihada zake inazofanya katika kuhakikisha ile heshima ya jinsia zote inalindwa.

Tukiangalia katika majeshi hasa jeshi la polisi utakuta kuna askari wa kike ambao kama itatokea muhalifu ni mwanamke basi askari yule hakuajiriwa kwa bahati mbaya bali hiyo itakuwa ni kazi yake kumpekua sehemu za mwili wake.

Hali kadhaalika mwanaume atapekuliwa na askari wa kiume katika kulinda heshima.

Hata mashuleni kuna waalimu wa kike kibao ambao wao watashughulikia masuala mbali mbali ya wanafunzi wa kike.

Mbona sioni suala hili la kuheshimu jinsia na kulinda heshima ya mtu likifanyika na kusisitizwa katika kada ya afya ?

Kwa nini isiwe kosa daktari wa kumtibia mgonjwa wa jinsia tofauti na yeye ikiwa katika hospitali hiyo ama maeneo hayo kuna daktari mwenye jinsia sawa na mgonjwa ?

Kama ambavyo polisi haruhusiwi kumfanyia upekuzi wa mwili mtu wa jinsia isiyekuwa yake wakati wa jinsia yake wakiwa pale hii ni kosa,vipi isiwe kosa katika hii kada ya afya ?

Yani utakuta hospitali kuna madaktari wa jinsia nyingi lskini mwanamke anatibiwa na mwanaume au kinyume chake.

Serikali isomeshe watoto wengi wa kike ili kuja kuepusha hii aibu,ipunguze vigezo vya kusomea udaktari kwa mwanamke hasa kwa mambo ya kawaida haya ambayo hayahitaji kujitoa sana wanawake wasomeshwe waje kuzalisha wanawake wenzao.

Chumba cha kuzalisha kuna madaktari wa kike watano na wa kiume mmoja,huyu wa kiume anatafuta nini,kwa nini isiwe kosa kisheria?
unachotakiwa kujua ni kwamba, sehemu za siri za mwanaume au mwanamke hazina thamani yeyote. MIMI ni mwanaume, ningekuwa naumwa ugonjwa wa aibu singependelea nitibiwe na mwanaume mwenzangu. imagine mwanaume mwenzio anakushikashika makalio, penis, korodani, etc, bora mwanamke nitakuwa confortable. uchi hauna uzee au ukijana, ni uleule tu. ukitaka kujua kuwa ucho wako huo na wa mkeo hauna thamani, waulize wanawake ambao walishaenda leba kujifungua.

acha wivu, hakuna mwenye shida na mkeo, hata yeye anakushangaa pamoja na kwamba hawezi kukuambia hilo.
 
Wakuu naomba niipongeze serikali kwa jitihada zake inazofanya katika kuhakikisha ile heshima ya jinsia zote inalindwa.

Tukiangalia katika majeshi hasa jeshi la polisi utakuta kuna askari wa kike ambao kama itatokea muhalifu ni mwanamke basi askari yule hakuajiriwa kwa bahati mbaya bali hiyo itakuwa ni kazi yake kumpekua sehemu za mwili wake.

Hali kadhaalika mwanaume atapekuliwa na askari wa kiume katika kulinda heshima.

Hata mashuleni kuna waalimu wa kike kibao ambao wao watashughulikia masuala mbali mbali ya wanafunzi wa kike.

Mbona sioni suala hili la kuheshimu jinsia na kulinda heshima ya mtu likifanyika na kusisitizwa katika kada ya afya ?

Kwa nini isiwe kosa daktari wa kumtibia mgonjwa wa jinsia tofauti na yeye ikiwa katika hospitali hiyo ama maeneo hayo kuna daktari mwenye jinsia sawa na mgonjwa ?

Kama ambavyo polisi haruhusiwi kumfanyia upekuzi wa mwili mtu wa jinsia isiyekuwa yake wakati wa jinsia yake wakiwa pale hii ni kosa,vipi isiwe kosa katika hii kada ya afya ?

Yani utakuta hospitali kuna madaktari wa jinsia nyingi lskini mwanamke anatibiwa na mwanaume au kinyume chake.

Serikali isomeshe watoto wengi wa kike ili kuja kuepusha hii aibu,ipunguze vigezo vya kusomea udaktari kwa mwanamke hasa kwa mambo ya kawaida haya ambayo hayahitaji kujitoa sana wanawake wasomeshwe waje kuzalisha wanawake wenzao.

Chumba cha kuzalisha kuna madaktari wa kike watano na wa kiume mmoja,huyu wa kiume anatafuta nini,kwa nini isiwe kosa kisheria?
hii sio rahisi ,hakuna ubaya kuvua boxer yako kwa Dr wa kike.Cha muhimu ni matibabu.Hata kule labour ward madaktari wa kiume ndio wanaongoza kwa kufanya operation za kuzalisha na wala hakuna malalamishi.Huwezi kufika hospital na kuanza kuchagua mtu wa kukutibu .
 
Naunga mkono hoja mke wangu wakati wa kuzaa nitampeleka kwenye hospitali za private halafu nalipa na kuweka sharti la mke wangu kuhudumiwa na wanawake tu
 
Mimi nimeenda kupima vipimo na dr wa kiume pembeni yangu alikuwepo nurse mwanamke, na Hadi kwenda theatre hyo ni lazima nurse wa kike awepo na hyo ya kuchunguliwa haina mashiko
Nina wasiwasi wanawake wa hivi wakishapona, siku nyingine wakikutana na huyo dokta katika mazingira tofauti hawashindwi kumtunuku huyo dokta.
 
KILA kazi ina maadili na miiko yake,tiba haijali jinsia,unatibiwa na mtaalamu wa jinsia yeyote
 
Wakuu naomba niipongeze serikali kwa jitihada zake inazofanya katika kuhakikisha ile heshima ya jinsia zote inalindwa.

Tukiangalia katika majeshi hasa jeshi la polisi utakuta kuna askari wa kike ambao kama itatokea muhalifu ni mwanamke basi askari yule hakuajiriwa kwa bahati mbaya bali hiyo itakuwa ni kazi yake kumpekua sehemu za mwili wake.

Hali kadhaalika mwanaume atapekuliwa na askari wa kiume katika kulinda heshima.

Hata mashuleni kuna waalimu wa kike kibao ambao wao watashughulikia masuala mbali mbali ya wanafunzi wa kike.

Mbona sioni suala hili la kuheshimu jinsia na kulinda heshima ya mtu likifanyika na kusisitizwa katika kada ya afya ?

Kwa nini isiwe kosa daktari wa kumtibia mgonjwa wa jinsia tofauti na yeye ikiwa katika hospitali hiyo ama maeneo hayo kuna daktari mwenye jinsia sawa na mgonjwa ?

Kama ambavyo polisi haruhusiwi kumfanyia upekuzi wa mwili mtu wa jinsia isiyekuwa yake wakati wa jinsia yake wakiwa pale hii ni kosa,vipi isiwe kosa katika hii kada ya afya ?

Yani utakuta hospitali kuna madaktari wa jinsia nyingi lskini mwanamke anatibiwa na mwanaume au kinyume chake.

Serikali isomeshe watoto wengi wa kike ili kuja kuepusha hii aibu,ipunguze vigezo vya kusomea udaktari kwa mwanamke hasa kwa mambo ya kawaida haya ambayo hayahitaji kujitoa sana wanawake wasomeshwe waje kuzalisha wanawake wenzao.

Chumba cha kuzalisha kuna madaktari wa kike watano na wa kiume mmoja,huyu wa kiume anatafuta nini,kwa nini isiwe kosa kisheria?
Kuna dhana moja kwamba mafundi nguo wa kiume ni wajuvi sana wa mishono ya kina mama.

Lakini ni aghalabu fundi nguo wa kike kushona mavazi ya kiume.

Sasa mkuu, vipi kwa fundi nguo wa kiume kumpima mwanamke mwilini?
 
Watanzania tuna ujuaji mwingi sana, hua tunapenda kujiona tunajua kila kitu, mtu unazungumzia haki mara sio sawa, je umesoma sheria na taratibu za hospitali, je umesomea udaktari...??!!
Em kua mpole kwanza umwa uwe mahututi ndo utajua umuhim wa matibabu pasipo kujali jinsia ya daktari
 
Kaka Cha wivu.
Hili suala lipeleke kwa mbunge wako ulimchagua majuzi alipeleke bungeni itungwe Sheria. Then shemeji hawezi Tena kuhudumiwa na madaktari wa kiume. Angalizo Kama atahitajika kupimwa vipimo Kama ECHO, MRI, CT SCAN, na vingine vya kuvua nguo imekula kwako maana wataalamu wa kike bado Ni wachache.
Jingine Ni pale shemeji atakapohitaji huduma za daktari mbobezi wa magonjwa ya kina mama, wabobezi bado Ni wachache sana Tanzania halafu Hawa lazima waone na kushikashika kibuyu Cha asali Cha shemeji.
Mimi nadhani tu ungeacha wivu kwani fahari ya macho haifilisi duka.
 
Mwaka 2018 nikiwa hospital moja ya serikali hapa nchini nilikuwa zamu usiku kwenye wodi ya akina mama wanaosubir kujifungua, nikipiga kaz ya kuzalisha kama wanawake sita, kufikia mida ya saa 7 usiku ikanibid nikapumzike kidogo, japo Kuna waliokuwepo mle licha ya kulalamika uchungu njia zao bado zilikuwa haziwez kupitisha mtoto, hvyo nikawaacha waendelee kulia na uchungu ili nipumzike kdg.

Mida kama saa nane kasoro kuna mmama aliletwa kutoka home aliambatana na mume wake alivyofika mm ndio nilimpokea hakukuwa na mtu mwingine, yule mume wake akaniuliza ww ndio utamzalisha mke wangu? Nikamjib ndio ni mm( kimuonekano naonekana ni mdogo)

Akasema mke wangu nampenda sana sitaki mwanaume yeyote amuone tofauti na mwanamke, mwenzie , Nikamwambie mkeo hatakufa muonekano wa hilo Tumbo (hakuniruhusu hata nilishike) inaonesha mtoto kakaa vbaya, jamaa akakaza nikaona isiwe tabu , nikamwambia aende hospitali nyingine asije kuniletea case eti nimeshindwa kumtib mgonjwa kafia mikononi mwangu..

Yule mke wake uchungu ulikolea mpka akawa anamtukana mme wake, Unataka nife?? bac uje unizalishe ww? na nikifa nakulaani? unataka umuue mwanangu na mm piah! ww mwanaume ni shetani.

Baada ya jamaa kuona vile ikabid aniruhusu nimzalishe mke wake akanipa na masharti juu eti na yy aingie kushuhudia nikakataa taaluma yetu airuhusu, ww subir hapo.oooh mke wangu ni mzuri , unaweza ukambaka, mara usiwe na unamshika Sana.( Yule jamaa ni mtu mzima lkn kama mtoto vile) ikanibid niite walinzi wamtoe ili niweze kuokoa maisha ya mke wake.

Kiukwel yule mwanamke alikuwa ni mzuri lkn sikuwa na interest nae.nafikir mume wake alikuwa anahis nitamfanyia kitu kibaya!!

Ushauri+++ Kuna haki za mgonjwa, Kuna haki za daktari tafadhar hiz kaz ziheshimiwe.Ukihisi labda Kuna vitendo vya unyanyasaji vinafanyika unaenda kuripoti kwenye mamlaka husika ili haki itendeke.Watu wachache wasituharibie taaluma yetu.daktari wa kike na daktari wa kiume wote wana haki ya kutibu mgonjwa yeyote yule kwa sababu wote tumesomea magonjwa yote
 
Kuna dr mmoja wa kike alinichoma sindano za makalio, nilijisikia vibaya sana kama mwanaume.
 
Sheria inaruhusu kupata huduma kwa mtoa huduma unayemtaka, kwa hiyo ukiona anayekupa huduma ni jinsia usiyeitaka kataa ili uende kwa hiyo jinsia unayotaka ikupe huduma,..na kama utakuwa kwenye hali ya dharura,kuokoa maisha na umekataa itabidi uandike ili ukifa mtoa huduma awe safe.
 
Back
Top Bottom