swala la afya ni swala nyeti lenye kushughulika kuhakikisha uhai wetu unaimarika ipasavyo, huku gender it does not matter usitumie itifaki za "ujinsia" kwenye mambo ya afya.
Unaposema kwa nini tusitumie inatakiwa uwe na sababu,kusema tusitumie itifaki za jinsia bila sababu hiyo haiwi hoja,hoja ni kwa nini tusitumie.
lakini katiba hiyo hiyo imempa immunity raisi kwamba hatakiwi kushtakiwa kivyovyote vile na hata akitoka madarakani hupaswi kumshtaki kwa makosa aliyoyafanya akiwa raisi
Hii nayo pia inalalamikiwa na watu wengi tu kwamba imempa raisi mamlaka makubwa,sasa huwezi kuitumia hii hoja ambayo pia ina malalamiko ati ukaifanya hoja ya juu ya jambo lingine lenye malalamiko pia.
Yaani unatumia hoja yenye mgongano kumaliza mgongano,ilitakiwa uweke hoja ambayo haina malalamiko kama hii uliyoitumia.
sasa upolisi unafikiri unahitaji taaluma yeyote ya kibailojia?
Sasa kama huko kupekua hakuhitaji taaluma kwa nini hata polisi wa kiume asimpekue polisi wa kike ?
Wakati yule anaepekuliwa pengine anatuhumiwa kinyume na mgonjwa ambaye hana tuhuma yeyote,hapo ilikuwa huyu anaepekuliwa apekuliwe na polisi yeyote yule,lakini mpaka katika mas'ala haya ya uhalifu bado wakaona kuna thamani ya jinsia lazima ilindwe,why isilindwe thamani ya jinsia katika mas'ala ya afya ambayo hayo ni mas'ala salama kabisa ?
kwani kuna polisi maalumu kutoka kitengo cha kupekua ambaye amekua trained special kwa kazi hiyo au ni gender tu ndiyo kigezo?
Kigezo ni gender,kwa nini hiki kigezo cha gender hakizingatiwi katika fani hii ya afya ?
Kwa sababu daktari wa kiume utakuta anakataa kumzalisha mama yake ili ampate mdogo wake,hii maana yake kama gender na ule utu ungekua haupo basi hili lisingepatikana kabisa ingekuwa rahisi daktari kumzalisha mama yake.
.lakini hayo yote yanafanywa na pengine daktari hawezi kupangiwa kwao kuepuka hili jambo.
hivi unafikiri huyo mpekuzi akiwa huko mafunzoni anafundishwa namna ya kuwapekua watu wenye jinsia kama yake?
Ndio wanafundishwa kupekua kwa kupewa mifano wao kwa wao wanawake wapekuane,hachukuliwi mwanaume akatolewa mfano.hili niliwahi kulisikiia kwa baadhi ya askari wanalisema hasa wale wa kike.
hospitali kuna mtu anaitwa "Obstetrician" huyu kakaa shuleni miaka zaidi ya miaka zaidi ya minne akis mfumo mzima wa uzazi wa mwanamke kuanzia mimba, mpaka kuzalisha. huyu amegraduate kwenye medical school kashapata ujuzi na anaenda hosipali kulipwa mshahara kwa kazi hiyo hiyo tofauti na mwela mshika kirungu ambaye mostly ni form four failures
Mbona haina shida hiyo,kwa sababu watakuja watu wa jinsia yake atawahudumia vizuri,hiyo haina shida.shida ni kuja mtu wa jinsia tofauti na yeye.
Kwa nini pasiwe na obstetrician wa jinsia zote,inashindikana nini ?
ikiwa wanafunzi wa jinsia hiyo ambao wanapaswa kushugulika na wagonjwa wa kike hawaja-qualify kupata huo ujuzi utawalazimisha waingie kwenye majukumu ambayo hawana uwezo wa kuyamudu?
Nani kalazimisha mkuu ?
Hao wanafunzi ambao hawajaqualify inatakiwa waqualify sasa ili wamudu hayo mambo kwa sababu ni wanafunzi basi wanatakiwa wa qualify na kuanza kufanya kszi hizo.
Hakuna aliyesema kuwa ati wafanye hivyyo hivyo labda iwe hukunielewa tokea mwanzo.
wengi wanakua ni nurse assistant, yani kama fundi msaidizi wa ujenzi ambaye hufanya kile anachoagizwa na fundi mkuu wake kutokana na kutokua na taaluma ya ujenzi.
Nakubali wanawake wengi ni nurse assistant,lakini solution yangu iko pale pale kuwa serikali izalishe madaktari wengi wa kike ili waje kupunguza au kuondoa hili wimbi,
sote tunakubaliana hapa kuwa kweli madaktari wa kike hawatoshi na ndio maana nikaanzisha uzi,sasa solution basi swrikali iqeke mikakati ya kuzalisha madaktari wengi wa kike kwa ajili ya kutibu hili janga.
ishu sio kuwepo, ishu ni ujuzi wa taaluma husika. kwa mfano imetokea kaja mgonjwa anatakiwa afanyiwe operation ya na titi ukicheki around kuna ma-nurse ambao kimsingi hawana taaluma halafu kukawa na daktari wa kiume mwenye ujuzi wa hilo tatizo je utalazimika kurudi na mgonjwa nyumbani ?
Unarudi kule kule kuwa madaktari wa kike ni wachache,solution ni kuweka mikakati itakayosaidia kuzalisha madaktari wengi wa kike ambao hata hao wakufanya operation watakuepo wa kutosha,na sidhani kama unaweza kuniambia kuwa wanawake hawawezi kumaster hizo kazi,sidhani.
kwa mfano imetokea kaja mgonjwa anatakiwa afanyiwe operation ya na titi ukicheki around kuna ma-nurse ambao kimsingi hawana taaluma halafu kukawa na daktari wa kiume mwenye ujuzi wa hilo tatizo je utalazimika kurudi na mgonjwa nyumbani ?
Ama nikijibu swali lako hapa huwezi kurudi na mgonjwa,atatibiwa na mwaume huyo huyo kwa sababu daktari mtaalamu wa kike hayupo.
Na sikusema popote kwenye uzi wangu kuwa wanawake wasitibiwe na madaktari wa kiume,nilichosema madaktari wa kike wawe wengi.alafu pia serikali yenyewe itilie mkazo suala hili,na wala sikuja na personal conclusion kwamba ati wasitibiwe NO NO.
na hiyo ita conclude kua gender doesn't matter on health services, kwahiyo utajikuta point nzima ya kulalamikia madaktari kuhudumia wagonjwa wenye jinsia tofauti na yao ni
Pale iliconclude kwamba ishu sio gender bali ishu ni uadimu wa daktari wa kike mzee.
Kitendo cha mimi kusema "
Ikiwa ugonjwa huo anaeweza kutibu ni dokta wa jinsia tofauti na mgonjwa basi uzi wangu wala haukukataa kutibiwa.
Hii maana yake ni kuwa natanguliza maslahi ya kutibiwa na daktari wa jinsia tofauti endapo wa jisnia sawa hayupo.
Suala la jinsia kwangu litamata endapo dakatri bingwa wa jinsia ya mgonjwa atakuepo,na hiyo ndio point ya uzi wangu.
Ndio maana sikusema wasitibiwe bali nilisema serikali iongeze wataalamu,lakini nikasema pia katika sehemu ambazo kuna madaktari wa jinsia zote wataalamu wa magonjwa husika basi swrikali itilie msisitizo kuwa katika hospitaki hizo wagonjwa watibiwe na daktari wenye jinsia sawa na hao.
Kwa hiyo kwa kukufahamisha zaidi.
Mwanamke kutibiwa na mwanaume wakati ambapo daktari wa mwenzie wa kike hayupo Hili ni jambo ambalo kwangu kuna maslahi ya kuokoa maisha ya mgonjwa huyu hivyo siwezi kukataa.
Lakini mwanamke kutibiwa na dokta wa kiume wakati dokta wa kike mtaalamu pia yupo,sasa suala hili ndo serikali itilie mkazo kuwa atibiwe na mtu wa jinsia yake.
kwani serikali haisomeshi watoto wa kike? mbona ndio wanaotuongoza kwenye matokeo kitaifa kila mwaka?
Angalia katika kada ya afya hasa udakri usiangalie wanaongozaje katika mambo ama ujumla wake,hapa tunachoangalia ni jambo maalumu la udaktari,daktari wa kike ni wachache.
ishu ya udaktari ni persona interest, unaweza kuwapata maelfu ya wanawake wasomi na wenye ufaulu mzuri lakini katika hao ni wachache tu ndio wakawa attractive na udaktari. na katika hao watao chagua udaktari ukapata kundi lenye kujigawa tena wengine wakawa madaktari wa mifugo
Bado uwezekano wa kuwapata madaktari wa kike upo kama ambavyo hawa waliopo wamepatikana basi inawezekana kuwapata wengine kama hawa waliokuwepo.
Vingimevyo usema kuwa wanawake kiasili hawawezi kuwa madaktari.ila kama kuna ambao weweza basi mikakati ikifanyika pia itawezekana kuwapata wengine.
na ndio maana nimekuambia haya mambo yana base sana kwenye interest binafsi, kwa mfano hata katika shule uliyosoma kulikua na wanafunzi wangapi darasani mwenu ambao walikua science taker?
Hapa tutaingia kwenye jambo lingine.
Mfano
Darasani kwangu asilimia ya wanafunzi kubwa walitaka kuwa madaktari lakini walikataa kuchukua sayansi kwa sababu ya kuaminishwa kuwa sayansi ni ngumu.
Hawa walikuwa wanataka udaktari lakini walikwamishwa na sababu mbovu ambazo wangepewa nguvu ya ziada ya jihitaha pengine na kuhamasishwa basi wangeliweza kufikia malengo yao.
Kumbuka kuna kila sababu inayomkwamishwa mtu asifikie analolitaka.
wanawake wengi ni wasomi tena sana (mpaka wanaume) ila usomi wao asilimia kubwa ni katika masomo sanaa. na hawa pia kumbuka ni wasomi hatuwezi kuwaita sio wasomi eti kwakua hawaja chagua masomo ya sayansi wakati mfumo wa kielimu umetoa uhuru kila mwanafunzi kuchagua mchepuo autakaye.
Yes nao ni wasomi ila sio wasomi wa udaktari.
Solution ni kuweka mikakati za kuzalisha madaktari wengi wa kike ili htatizo hili liondoke.
Wanawake wengi hawajachagua sayansi kutokana na mazingira na sababu mbali mbali za kijamii na kisaikolojia lakini sababu hizi zikiangaliwa kwa upana wake na kutafutiwa ufumbuzi basi tunaweza kuzalisha madaktari wengi wa kike.
Mfano wanawake wengi huambiwa kuwa sayansi ni kwa ajili ya wanaume,wengi huambiwa sayansi ni ngumu hivyo chukua japo CBG,utakuwa saikolojia zao zinakuwa hivyo wanaamini hivyo kizazi na kizazi.
Sababu kama hizi zikipigwa vita na nyinginezo basi tunapata madaktari wengi wa kike.
na kumbuka hauwezi kuwashurutisha wasome masomo ambayo wao wameona yanawazidi uwezo eti kwakua sector fulani inahitaji watu wengi zaidi
Wanawake pia wanao uwezo wa kuwa madaktari wala sio kwamba ni jambo special kwa mwanaume tu hapana,sababu ni nyingi sana.
Kama hivi leo idadi ya manesi ni wengi sana basi inawezekana oia idadi ya madaktari ikawa nyingi pia.kwa sababu unesi na udaktari ni kada moja ila tofauti ni utaalamu kwa hiyo kama manesi wa kike wapo wa kutosha badi pia inawezekana na madaktari pia wakawepo wa kutosha wa kike ikiwa mikakati itapangwa.
wengi wa hivyo wapo ila ku-balance kwamba kila hospitali hususani hizi za hospitali kwamba iwe na madokta bingwa wa jinsia tofauti zaidi mmoja ndio kasheshe
Sasa hapo ndo inatakiwa mikakati madhubuti ambayo sio mikakati ya kyona matokeo mwaka mmoja ama miwili ijayo bali iwe mikakati ya kuanzia pengine miaka 10 mbele huko.
Ni jambo linahitaji mikakati madhubuti.
huyo mama haishii kwa wanawake tu mpaka tohara kwa watu wazima anawafanyia
Ndio kutokana na kuachiwa hili suala kwa upana wake