Serikali na Wasafi TV mlitakiwa muwe mmeshakuchukua hatua za kinidhamu kwa Makonda na Oscar. Ukimya wenu unamaanisha mmebariki udhalilishaji huo?

Kum
Inapotokea mfanyakazi wa taasisi fulani amefanya kosa mbele za umma na akaonywa mbele za umma pia, tunatarajia taasisi anayofanyia kazi kuwajibika, kwanza kwa kukubali kuwa kosa limefanywa, kuomba radhi kwa umma, na kuchukua hatua za kinidhamu kama kanuni za maadili zinavyowaelekeza kulingana na taasisi hiyo.

Kilichofanywa na Oscar Oscar pamoja na Makonda ni udhalilishaji na uvunjivu wa haki za binadamu, Wasafi na Serikali kwanza walitakiwa kukubali kwanza kilichofanyika sio sawa na Serikali kama mtetezi mkuu wa haki za binadamu pamoda na Wasafi kama wadau wanaotetea haki za binadamu ilibidi watoe neno na kumtaka aliyefanya ukiukaji huu aombe radhi kwa umma pamoja na kuwachukulia hatua za kinidhamu.

Lakini inashangaza Oscar Oscar hajatoa neno kuomba radhi na taasisi inayomsimamia nayo imekaa kimya wala haijajigusa. Vivyo hivyo kwa Makonda, amedhalilisha mtu afu anakuja kujitapa hawa wananipiga kelele tu nizidi kusonga mbele na kuwashughulikia wajinga. Hakuna mtu anayekubali uzembe, rushwa wala ubadhilifu, lakini unatakiwa kutumia njia sahihi kufanya hivyo.

Ni aibu, huzuni inatia hasira na kinyaa kwamba mpaka sasa serikali haijatoa tamko lolote kumkanya Makonda na kuomba radhi kwa jambo alilofanya. Mnajenga viongozi wa namna gani? Leo Makonda kafanya hili limenyamaziwa kesho litafanyanika kubwa zaidi, ndio mnataka hii iwe norm? Kwakuwa mtu ana mamlaka basi afanye atakavyo?

Mnakuja na hoja za kijinga na kipumbavu kabisa, eti mbona kuna matukio yalitokea nyuma hayakupigiwa kelele, kwahiyo hilo linafanya jambo alilofanya Makonda kuwa sawa? Kwahivyo kila mtu akidhalilishwa hii ndio itakuwa escape goat (upenyo wa kuchomokea) na kuhalalisha kosa ulilofanya?

Embu tuweni serious basi, serikali msituangushe tukazidi kupoteza imani na nyie zaidi ya hapa tulipofikia, mnatengeneza bomu ambalo hamtaweza kulitegua mbeleni.

====

Pia soma:
- LHRC yamuonya Makonda kwa kumdhalilisha Mtumishi wa Kike mbele ya Umati wa Wananchi
- Makonda ashtakiwe kwa udhalilishaji alioufanya kwa mwanakamati huyu
Kumwambia mwanamke mm Nina mke mzuri ni kosa? Kwahiyo akimsifu mke wake mbele ya kadamnasi ww kinakuuma sio?
Acha upumbavu Kuna matukio mengi ya kikatili wanafanyiwa wanawake wenzako na mabinti ila hujawahi kutoka mbele kulaani kama sio unafiki ni nini?
 
Acha kutoa maoni kama hauna kichwa Mkuu, kila taasisi ina utaratibu wake wa kufuata ikiwa mfanyakazi wao ame misbehave
Mkuu sio kwa ubaya ila wewe ni jinsia gani? hiyo kauli yako ya mwanzo ni ngumu sana kutolewa na jinsia ya KE.
 
Sawa sina kichwa,tambua hakuna hatua itachukuliwa,na kuwadhalilisha kutaendelea hadi mtakapobadilika,kama unasubiri hilo tambua imekula kwako
Kwahiyo ukirefer hivyo kama mimi ndio hao watumishi umejihisi vizuri mwenyewe?:KEKWlaugh::KEKWlaugh: Nyie ndio mnaochangia ujinga kama huu kuendelea nchini. Haijalishi anaongea na nani kuna taratibu za kufanya kila kitu bila hivyo tutatengeneza mfumo mbaya ambao hata mtu akiuliwa tutaona sawa tu.

Hutakiwi kukemea jambo baya mpaka pale tu mtu wako wa karibu akiguswa, leo ametokea kwake, kesho inaweza kuwa kwako na ikawa mbaya zaidi, penye uonevu tuseme, an anapostahili pongezi pia apewe maua yake. Ukiingia ndani usiwe unaacha ubongo nje, unauhitaji kufanya maamuzi sahihi!
 
Hv mnajua ninyi ni wajinga na wapumbavu!? Kumradhi.

Nchi hii ina mambo mangapi yakushughulikiwa !? Upigaji upo kila mahali nchi hii mpo kimya tu CAG Kule Billions of Tsh zinapigwa mmekalisha makalio tu hamjawahi lolote leo kitu cha ajabu kama hki cha Paul Makonda ety manongeaaa 😅😅 mbona hamna akili!? Nlichogundua Chuki ndio inaendesha haka kanchi.
 
Na mimi nakuuliza, wao kukaa kimya wakati 'mama' yao anatendewa hivyo inahalalisha hili alilotendewa yule dada au upuuzi anaofanya oscar. Kwakuwa kesi fulani ya ubakaji haikufanywa vyema basi watu waendelee kubaka?
Two wrongs don't make a right

Hivi unafananisha matusi ya nguoni mpaka mtu kuitwa unajihusisha na masuala ya jinsia moja

Na kuambiwa eti nina mke mzuri??

Duh achen ufamba basi
 
Hv mnajua ninyi ni wajinga na wapumbavu!? Kumradhi.

Nchi hii ina mambo mangapi yakushughulikiwa !? Upigaji upo kila mahali nchi hii mpo kimya tu CAG Kule Billions of Tsh zinapigwa mmekalisha makalio tu hamjawahi lolote leo kitu cha ajabu kama hki cha Paul Makonda ety manongeaaa 😅😅 mbona hamna akili!? Nlichogundua Chuki ndio inaendesha haka kanchi.
Unasema nyie akina nani? Tatizo tanzania hii umeona ni ripoti ya CAG tu? Wewe umesema nini kwenye wizi huo? Sio laizima kila mtu aongelee kile unataka kusikia, nisiposema mimi anaweza ongelea mwingine, unaweza ongelea hata wewe. Fungua hiyo akili, upeo wako usiishie hapo kwenye pua tu
 
Mlikuwa wapi kusimama dhidi ya hao waliofanya ubaya kwa wananchi?? Ama pesa zinazoliwa na hawa watumishi wa serikali si uvunjifu wa haki za kibinadamu?? Kuna mambo ya kuingia kwenye Human Rights breach na mengine ukiyaweka unaonekana zuzu. Hakuna alichodhalilishwa hapo huyo dada ila aliambiwa ukweli,huwezi kuwa mbele ya halaiki na unajibu tuhuma ujibu kwa kurembua as if uko na danga lako😆😆😆Na kama alikwambia kadhalilishwa mshauri aende Mahakamani ili afungue kesi kisha Paul na Oscar waitwe kujibu mashitaka yao ila tofauti na hivyo mimi nasema Makonda achape kazi na azidi kuwanyoosha wazembe,wezi na wajinga wasioweza kutimiza wajibu wao walioaminiwa na serikali yao na wananchi
 
Inapotokea mfanyakazi wa taasisi fulani amefanya kosa mbele za umma na akaonywa mbele za umma pia, tunatarajia taasisi anayofanyia kazi kuwajibika, kwanza kwa kukubali kuwa kosa limefanywa, kuomba radhi kwa umma, na kuchukua hatua za kinidhamu kama kanuni za maadili zinavyowaelekeza kulingana na taasisi hiyo.

Kilichofanywa na Oscar Oscar pamoja na Makonda ni udhalilishaji na uvunjivu wa haki za binadamu, Wasafi na Serikali kwanza walitakiwa kukubali kwanza kilichofanyika sio sawa na Serikali kama mtetezi mkuu wa haki za binadamu pamoda na Wasafi kama wadau wanaotetea haki za binadamu ilibidi watoe neno na kumtaka aliyefanya ukiukaji huu aombe radhi kwa umma pamoja na kuwachukulia hatua za kinidhamu.

Lakini inashangaza Oscar Oscar hajatoa neno kuomba radhi na taasisi inayomsimamia nayo imekaa kimya wala haijajigusa. Vivyo hivyo kwa Makonda, amedhalilisha mtu afu anakuja kujitapa hawa wananipiga kelele tu nizidi kusonga mbele na kuwashughulikia wajinga. Hakuna mtu anayekubali uzembe, rushwa wala ubadhilifu, lakini unatakiwa kutumia njia sahihi kufanya hivyo.

Ni aibu, huzuni inatia hasira na kinyaa kwamba mpaka sasa serikali haijatoa tamko lolote kumkanya Makonda na kuomba radhi kwa jambo alilofanya. Mnajenga viongozi wa namna gani? Leo Makonda kafanya hili limenyamaziwa kesho litafanyanika kubwa zaidi, ndio mnataka hii iwe norm? Kwakuwa mtu ana mamlaka basi afanye atakavyo?

Mnakuja na hoja za kijinga na kipumbavu kabisa, eti mbona kuna matukio yalitokea nyuma hayakupigiwa kelele, kwahiyo hilo linafanya jambo alilofanya Makonda kuwa sawa? Kwahivyo kila mtu akidhalilishwa hii ndio itakuwa scapegoat (upenyo wa kuchomokea) na kuhalalisha kosa ulilofanya?

Embu tuweni serious basi, serikali msituangushe tukazidi kupoteza imani na nyie zaidi ya hapa tulipofikia, mnatengeneza bomu ambalo hamtaweza kulitegua mbeleni.

====

Pia soma:
-
LHRC yamuonya Makonda kwa kumdhalilisha Mtumishi wa Kike mbele ya Umati wa Wananchi
- Makonda ashtakiwe kwa udhalilishaji alioufanya kwa mwanakamati huyu
Ujinga huu
 
Chadema hamnaga kazi ya kufanya mkiamka mnapayuka payuka mpaka jua lizame. Hivi hoja kama hizi zinawaongezeaje kura?
Kila anayepinga ujinga unaofanya na baadhi ya viongozi CCM ni CHADEMA? Unajiona umetoa bonge la point mwenyewe! Kuna wengine hatuna vyama kokote wanapoboronga tunasema
 
Mlikuwa wapi kusimama dhidi ya hao waliofanya ubaya kwa wananchi?? Ama pesa zinazoliwa na hawa watumishi wa serikali si uvunjifu wa haki za kibinadamu?? Kuna mambo ya kuingia kwenye Human Rights breach na mengine ukiyaweka unaonekana zuzu. Hakuna alichodhalilishwa hapo huyo dada ila aliambiwa ukweli,huwezi kuwa mbele ya halaiki na unajibu tuhuma ujibu kwa kurembua as if uko na danga lako😆😆😆Na kama alikwambia kadhalilishwa mshauri aende Mahakamani ili afungue kesi kisha Paul na Oscar waitwe kujibu mashitaka yao ila tofauti na hivyo mimi nasema Makonda achape kazi na azidi kuwanyoosha wazembe,wezi na wajinga wasioweza kutimiza wajibu wao walioaminiwa na serikali yao na wananchi
Acha kufata mkumbo, kwakuwa makelele hayakusikika sehemu nyingine haimaanishi hili ni sawa, kama angekuwa mama yako naamini usingejihisi vizuri, vivyo hivyo iwe kwa watu wengine hata kama huwajui wala huna ukaribu nao
 
Kila anayepinga ujinga unaofanya na baadhi ya viongozi CCM ni CHADEMA? Unajiona umetoa bonge la point mwenyewe! Kuna wengine hatuna vyama kokote wanapoboronga tunasema
Ila katika hili ninyi ndiyo mmeborongaaaa, kuna harakati zingine unqzifanya mpaka yule unayemfanyia anakushangaa sana,kwa hiyo watu wasiambiwe ubaya wao kisa watavunjiwa haki zao?? Kwani kudhalilishwa anakuwa yeye wa kwanza?? Je! Kwa kutotimiza wajibu wake kazini amewavunjia haki zao watu wangapi??? Ama kwa kuwa wao hawasema hadharani basi hawqna haki
 
Ndio uwezo wako wa kufikiri ulipoishia? Kazi kweli kweli🤦‍♀️🤦‍♀️🤦‍♀️
We go along on the other thread, we quarrel on the other, by the way I live you. ❤️
 
Back
Top Bottom