Serikali: Sasa ni ruksa kusafirisha wanyama nje ya nchi

Mbona tumeshakwambia wanaouzwa ni wale waliozidi? Halafu Bahamas hakuna wanyama na watu wanaenda.

Hospitality industry sio suala la maliasili, ni suala la ubunifu wa kiakili.

Acha kupotosha wameruhusu kuuza wale wanao milikiwa kwenye vitalu lakini kuuza nje wanyama ni biashara kichaa kabisa maana ni vigumu kabisa kudhibiti biashara ya ujangili wakati umesha ruhusu wanyama kuuzwa kwa vyovyote hata hao wanao wamiliki waliwanunua humu humu na wapo nao kwenye mazoo! Wanakwenda nje kufanya nini kama sio utalii? Sasa royal tour yanini wakati tunauza vivutio kwa kisingizio viko kwenye vitalu? Serikali imechanganyikiwa kabisa!
 
 

Yani huu ni wehu kabisa!
 
Safi mnajazana na tembo zinakula mazao ya wananchi ni upuuzi mtupu bora kuuza kupata fedha za kigeni
 
napita tu wadau, salamu.
lakini kwa uzalendo tu,
VUNJA BEI: KUANDAA HESABU ZA KODI za makampuni; USAJILI WA MAKAMPUNI dakika za mwisho hizi..!!
0788104228
 
Hao wanyama wanaofugwa na kulishwa kwenye 'zoo' (Kama kuku wa kisasa ) hawawezi kuwa kivutio kikubwa cha kuzuia watalii kuja hifadhini kuona maisha ya wanyama mwituni.
Chimbuko la hao wanyama ni wapi?au wametoka ulaya kuja kufungwa hapa Tz.
Tatizo sisi atuthamini vyetu
 
Hivi ndivyo tunavyotaka, Sukuma gang walituchelewesha sana.

Mama upige mwingi usiyumbishwe na maneno ya sukuma gang, ongeza tozo, safirisha wanyama, pandisha bei ya mafuta, ongeza nauli, fukuza wamachinga wote mijini, ondoa nidhamu kwa watumishi wa uma, acha tuvimbiane sasa hivi rudisha zile "unanijua mimi ni nani wewe"!

Hiyo ndiyo demokrasia tunayoitaka....
 
Wenye connection naomba na mimi nisafirishwe kuelekea Qatar
 
Utalii ni hospitality na sio wanyama au vivutio. Hizi mindset ndio zinafanya utalii wetu haukui.

Mauritius hapo hakuna mbuga wala wanyama na wanavutia watalii kuliko sisi.
 
Utalii ni hospitality na sio wanyama au vivutio. Hizi mindset ndio zinafanya utalii wetu haukui.

Mauritius hapo hakuna mbuga wala wanyama na wanavutia watalii kuliko sisi.

Kwa hiyo tunawauza na kuwasafirisha nje ili kutengeneza hospitality?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kuuza wanyama nje na kusafirisha ni biashara kichaa hii! Sasa kwanini tuliharibu pesa kwenye royal tour?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…