Serikali: Sasa ni ruksa kusafirisha wanyama nje ya nchi

Serikali: Sasa ni ruksa kusafirisha wanyama nje ya nchi

Kuwepo mipaka katika uuzaji wa rasilimali hizi kutegemeana na hatari ya kundi la wanyama waliopo, mfano mamba walizidi mto fulani wavuliwe wauzwe ili kupunguza madhara hatarishi ya wanyama hao the same to others, wanaozidi na kuhatarisha usalama,
>Na sio kuuza tu kama wendawazimu....!
 
Viongozi dhaifu, wasio na maono wanaliletea taifa fadhaa kubwa.
 
Kurejea kwa baadhi ya vinara pale CCM ilionesha dhahiri kurejea kwa biashara mbovu kama hizi!

A few wanaofaidika na hizo biashara wamefanikiwa kupenyeza rupia ili walio karibu na maza wamdanganye akubali kirahisi!!
 
Serikali imeruhusu wanyama pori walionunuliwa kusafirishwa
 

Attachments

  • 20220604_194745.jpg
    20220604_194745.jpg
    141.4 KB · Views: 12
Hali iko hivyo, tunaelekea kule kule tulipotoka, sasa ni rasmi twiga wetu wataanza kupandishwa ndege tena kwenda Ughaibuni.

_______________


Wafanyabishara sasa huru kusafirisha wanyama Pori kutoka Tanzania

Marufuku hiyo imeondolewa kwa muda wa miezi sita ambapo wafanyabiashara watakuwa huru kusafirisha nje wanyama pori kuanzia Juni 6 hadi Desemba 5

Tanzania imeondowa kwa muda marufuku ya usafirishaji wanyama pori iliyokuwa imewekwa miaka sita iliyopita kwa lengo la kuwalinda wanyama pamoja na ndege katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Uamuazi wa kuondolewa marufuku hiyo kwa kipindi cha miezi sita kumewaibua watetezi wa mazingira na wanyama pori kutowa mwito kuwepo michakato ya ufuatiliaji kuwalinda wanyama dhidi ya ujangili ambao umepunguwa kwa kiasi.

Mamlaka ya wanyama pori nchini Tanzania ijumaa ilitowa taarifa ikisema serikali imekuwa ikitathmini biashara ya usafirishaji wanyama pori hai tangu ilipowekwa marufuku hiyo na hivi sasa imeamua kuondowa marufuku hiyo.

Taarifa hiyo imebaini kwamba wafanyabiashara watakuwa na kipindi cha miezi sita kuanzia Juni 6 hadi Desemba 5 kumaliza kuuza wanyama waliokuwa wamebakisha walioshindwa kuwauza wakati marufuku hiyo ilipokuwa ikitekelezwa.

Tanzania iliweka marufuku ya kusafirisha wanyama pori mnamo mwaka 2016 chini ya utawala uliopita uliokuwa ukiongozwa na hayati rais John Pombe Magufuli ambaye namna yake ya uongozi ilimfanya apachikwe jina la ''Bulldozer''.

Wakati huo serikali ilihalalisha marufuku hiyo kwasababu ya dosari zilizokuweko kwenye biashara,ikiwemo usafirishaji nje wa wanyama wanaolindwa.

Rais wa sasa wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ameamua kujitenga na baadhi ya sera zilizokuwa zikifuatwa na mtangulizi wake,tangu alipoingia madarakani mwaka jana kufuatia kifo cha ghafla cha Magufuli.

WWF: Uamuzi huo usifute mafanikio yaliofikiwa

Shirika la kutetea mazingira na wanyama pori la WWF limetahadharisha kwamba kuondolewa kwa marufuku hiyo hakupaswi kuyaondowa mafanikio yaliyopatikana katika kuwalinda wanyama pori,na kuchochea kurudi hatua kama ujangili ambao umeonekana kupungua.

Amani Ngasuru ambaye ni mkurugenzi wa WWF nchini Tanzania ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mifumo ya uhakika ya ufuatiliaji inahitajika pamoja na data kuenda sambamba na maamuzi kama yaliyofanyika.

Tanzania inafahamika kwa fukwe zake za kuvutia katika visiwa vya Zanzibar,lakini pia matembezi ya safari ya kutazama wanyama pori pamoja na mlima mrefu barani Afrika,Kilimanjaro,yote hayo yakiwa vivutio vikubwa kwa watalii.

Mnamo mwaka 2010 kiasi wanyama 116 pamoja na ndege 16 baadhi wakiwa ni wanyama wanaotakiwa kulindwa walisafirishwa kutoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro,huko kaskazini mwa nchi hiyo kwa ndege ya shirika la ndege la Qatar.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani ya Tanzania, miongoni mwa wanyama hao walikuwemo twiga wanne, aina chungunzima ya paa,na ndege aina ya Tai.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri:Hawa Bihoga

View attachment 2250506
Usikute ndio masharti nafuu ya mikopo.
 
Duh, namkubali mama kwa mambo mengi ila hili lakuuza wanyama wetu nje hapana kwa kweli, huu ni urithi wetu tunatakiwa kuulinda kwa hali na mali,!!

Wazungu wakitaka kuona wanyama wa asili fulani ijulikane wapo Tanzania na sii vinginevyo!!

Hii sijaelewa kwa nn wameamua kufanya hivyo, ila siyo sahihi hata kidogo!! They should re think about it again!!
Na bado!
.
Taratibu mtaelewa tu. Hamna rais mle
 
Hawauzwi wanyama waliopo kwenye hifadhi za taifa au mamlaka ya hifadhi (Ngorongoro) ila wanauzwa wanyama wa kwenye vitalu.
Una akili hiyo ya kufuatilia kama ni wa kwenye vitalu?
 
Naamimi kabisa nchi hii mapinduzi yatakuja kuanzia hapa JF. Maxence Melo Max uendelee kutiwa nguvu bro. Sana sana bro.

Hii nchi haiji kuendelea bila wewe. Ni hiyari yetu tu kuamua.

Mimi nilishamua. Even with a thousand cuts I'll die for my mother country.
Waanzilishi wa hayo mapunduzi ni wapi? Hawa kina sexless?
 
Back
Top Bottom