Serikali: Sasa ni ruksa kusafirisha wanyama nje ya nchi

Serikali: Sasa ni ruksa kusafirisha wanyama nje ya nchi

Hahahaha wacha weee kwakuwa tunapata hela nyingi tuuze tuu urithi wetu hakika Mama ana upiga mwingi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Urithi kwa namna gani? Wanyama wanazaliana kila mwaka.

Mimi nimekuwa positive kwasababu unless kufanyike utafiti utakaotoa majibu negative, sioni ubaya wa kuuza na kutengeneza fedha za kuboresha huduma kwa jamii.
 
Hawauzwi wanyama waliopo kwenye hifadhi za taifa au mamlaka ya hifadhi (Ngorongoro) ila wanauzwa wanyama wa kwenye vitalu.

Sasa wakwenye vitalu hao wazungu walikuja nao? Kuuza ni kuuza tuu! Kwanini wasichukue nyama wanapeleka walio wazima?
 
Acha ujinga, akitokea mtu akafanya hujuma kuibawanyama kwenye hifadhi utawatofautisha vipi???.
Wanyama wote wanaowindwa au kuuzwa kwenye lazima uwe na kibali, hao wa hifadhini hawaruhusiwi kuguswa.

Kama mtu kawinda au kukamata mnyama lazima awe na kibali,kama hana huyo ni jangili na sheria itachukua mkondo wake.
 
Wanyama waliopo hifadhini ni marufuku kuwindwa au kuuzwa

.....ila wa kwenye vitalu inaruhusiwa kwa kibali.

Ukisha ruhusu kusafirisha wanyama lazima ushuhudie ujangili wa kupindukia kwa visingizio vya kuwa walikuwepo kwenye vitalu...biashara ya kusafirisha wanyama kama ingelukuwa ina faida nyingi basi tungekuwa matajiri sana lakini kwakuwa kuna ujangili mkubwa basi
 
Sasa wakwenye vitalu hao wazungu walikuja nao? Kuuza ni kuuza tuu! Kwanini wasichukue nyama wanapeleka walio wazima?
Nyama wanachukua na waliopo hai wanachukua vile vile ndiyo biashara hiyo.

Isitoshe uwindaji na uuzaji wa wanyama ni chanzo kimojawapo cha kuingiza fedha nyingi za kigeni na kuongeza akiba za fedha hizo.
 
Bora tuu serikali ingetoa fursa wawindaji wa ndani wakawinde then wawapelekee kitoweo watoto wao
Maana tushaambiwa njaa ipo karibu sasa si bora wenyeji tukatafute kitoweo kwenye mbuga zetu kuliko kuwapeleka ughaibuni?
 
Ukisha ruhusu kusafirisha wanyama lazima ushuhudie ujangili wa kupindukia kwa visingizio vya kuwa walikuwepo kwenye vitalu...biashara ya kusafirisha wanyama kama ingelukuwa ina faida nyingi basi tungekuwa matajiri sana lakini kwakuwa kuna ujangili mkubwa basi
Boss kama wanyama wa kwenye vitalu wamezaliana Sana kiasi cha kusumbua wananchi Kuna ubaya gani kuwavuna kwa faida ?

Na wanavunwa kwa kibali sio kiholela
 
Wengi wanapinga kwa kigezo cha utalii bila kufanya utafiti wowote. Watalii huku lazima waje kwao kunapokuwa majira ya baridi au joto kali (middle east)

Inaweza kufanyika cost benefit analysis kuona kama ina athari zozote.

Kama kuuza kunaleta fedha za maana hakuna tatizo kama wanyama wapo wengi.
Usiwaze karibu,waza miaka mingi ijayo itakuaje?
 
Back
Top Bottom