DOKEZO Serikali tusaidieni wananchi, magari yanayouzwa kwenye yard za Wapakistan mitaa ya Morocco na Victoria ni mabovu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kurudisha Odometer sio zoezi la saa moja. Ni zoezi la muda kidogo.

Jan Motors wao hawa gari zao utaikuta kama ilivyo na bei zao ziko chini, hivyo watu huenda kwao wananunua afu wanaenda uza tena
Jan international wao ni employees ,sio agent ni wafanyakazi wa kampuni ya huko japan kwahiyo ni ngumu kufanya modification

Wanalipwa mishahara tu


Tofauti ba agents
 
Sasa Mimi nikianza kuandika hapa jinsi tunavyo chezewa in JPM voice....

Itoshe kusema Kila mbuzi ale Kwa urefu wa kamba yake.....

Unaweza ukaonekana mnoko na mtu mwenye wivu kisa tu kutetea maslah ya Watanzania....
 
Ngoja nimumue mitambo ya kukagua magari hitilafu zake
Yaani kazi yangu ni kukagua tu
Haya ya kurudisha hata waweke haijatembea kabisa wataumbuka tu kwa ukaguzi

Na nchi yetu haitaisha laana kwa kweli
Hao hao waliokupa 1m na wakaguzi wakija wanapewa nao

Umewarahisishia kazi watu wa kodi na standards ni kwenda kujichotea tu
 
Gari yoyote used kutoka nje haikosi hitilafu mkuu
Labda mtu akanunue showroom toyota au dt dobie mapugu Road huko

Ova
 
Endelea na biashara yako ukusanye mamilioni
 
Huo mchezo ni wa siku nyingi tu. ukienda kununua gari usiangalie odometer maana zainachakachuliwa sana. Gari zee viti vimechakaa eti km50,000. Nilinunua gari jipya sasa hivi nimefikisha km 50,00 na ni kama mpya tu.
Gari zinakuja kama zina michubuko au zimegongwa tu wanaita mafundi wa kunyoosha na kupiga rangi
Kama mfuko wako mzito mtu anunue brand new car .....na nashangaa eti gari za yard wanaziita brand new car
Wakati ishatumika

Ova
 
Ya kwangu ni ya mwaka 2000, wakati naagiza Japan ilisoma km 17,000, mwaka wa sita sasa ndo ipo km 62,000.......kununua gari yenye zaidi ya km laki moja naona ni kama kujilipua.​
Wamefuta 1 au 2 yaani ilikuwa na km217,000 au km117,000. Gari wanajua ni nzuri pamoja na km hizo ila wanajua ukiona hizo km hutanunua kwahio wanafuta tu hio 1 au 2 kukuridhisha. Gari ya 2002 itakuwaje na km12,000?
 
Mawazo ya kiboya sana haya, kwani polisi wote wako hivyo? Jamaa yangu aliibiwa gari baada ya miezi 3 akaitwa polisi na kupewa gari yake, tena ikiwa haina shida yoyote, acha kukariri..
 
Hata ndani ya hayo masaa motor haiwezi rudisha km 170,000 nyuma
Kurudisha km nyuma ni kitendo cha dakika kadhaa tuu maana wanatumia computer wana command cbox kusoma millage wanazotaka wao iyo michezo nimeifanya sana ndan ya dakika 10 hata ukitaka isome 00 chap tu
 
Shida mnataka gari za km chache huku uwezo ni gari za 2000-2010 ndio maana wanaamua kucheza na km ili kuwaridhisha. Unanunua gari ya 2004 halafu unataka iwe na km 40,000 ilikuwa haitumiki mpaka wewe ulipotokea kuinunua? Haiwezekani . kitu ambacho wanahakikisha ni kuwa gari iko vizuri
 
Hapo kwa wewe kupewa mil 1 ni uongo...wewe una price tag gan? Ungekuwa na price tag kubwa usinge enda kuulizia gari low classes kama hizo. Acha uongo!
Probox kwa kubeba mizigo ndiyo kazi zake, bei zake 14 million na zaidi, wewe ulitaka anunue BMW kubebea mizigo [emoji23] [emoji23]
 
Kurudisha km nyuma ni kitendo kinafanyika chini ya dk 30
Mbona nyingi sana cpu ikisoma tu hata ndani ya dakika 2 kwa mtu sharp kwenye computer unarudisha maana ni kuandika tu unataka km ngap ukimaliza pale pale inabadili
 
Oda mita zinachezewa sana.sema uimara wa gari siyo kwenye oda mita.ila wakichezea oda mita maana yake kuna wanachoficha pia
 
Kwahiyo ukabeba milioni ukanyamaza😂😂😂 dah sipati picha ulivokunjua sura ulivoiona 1M , Tz rushwa haifi Leo aisee😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…