DOKEZO Serikali tusaidieni wananchi, magari yanayouzwa kwenye yard za Wapakistan mitaa ya Morocco na Victoria ni mabovu sana

DOKEZO Serikali tusaidieni wananchi, magari yanayouzwa kwenye yard za Wapakistan mitaa ya Morocco na Victoria ni mabovu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Serikali itupie macho uhuni unaofanywa na hawa wafanyabiashara wa magari wenye asili ya Pakistan.

Jana mida ya saa sita mchana tulienda na rafiki yangu kwenye moja ya maduka (yard) ya kuuzia magari. Rafiki yangu alikuwa anataka Toyota Probox kwa ajili ya kubebea mizigo yake Kariakoo na kwenye godown yake.

Tukafika hiyo saa sita tukakuta magari ndiyo yanapangwa. Walivyomaliza tukaomba kukagua gari moja. Kijana akaitwa akaja mbio na funguo za gari zikiwa mkononi kwake.

Nikakaa kwenye usukani na rafiki yangu pembeni. Nilipoiweka gari switch on nikakuta odometer inasoma gari imetembea kilometa 219,551. Bei milioni 16

Tukashauriana tukasema hapana hili gari halifai. Tukaendelea duka jingine na jingine na jingine.

By saa tisa tukafudi tena kwenye ile Probox, tukakuta ishachezewa odometer, sasa inaonekana imetembea kilometa 46,755.

Nilikuwa nimeoiga picha chasis namba mlangoni na dashboard. Nikipowauliza mbona hii gari mmeichezea kilometa, nikawaonyesha na picha wakakasirika sana wakapora simu yangu. Nikawaambia kaeni nayo, leo mtalala polisi.

Nikawa naondoka kulekea kwenye gari tuliyokuja nayo hapo yard, ndipo mmoja ya wafanyabiashara wale akaja mbio huku akinibembeleza nifute zile picha watatupa million moja.

Hela tamu, tukakubali kufuta picha, tukabeba milioni yetu. Tukaondoka.

Lakini backyard ya hizo yard zote kuna mafundi wako busy wanayaweka sawa mamikweche hayo.

Kingine tulichogundua ni kwamba kwenye minada ya magari, magari ya nauzwa kwa classes. Hawa wanachagua class duni kabisa, yakifika hapa wanaongea vizuri na wakaguzi, wanatolewa bandarini.

Kwa somo hili tulilojifunza jana rafiki yangu amekata tamaa kabisa na magari haya. Sasa kaona bora aagize kutoka Japan 🗾 asubiri siku 45 abebe mwana wake wa uhakika
Wewe ni sehemu ya tatizo.

Hizo picha ulitakiwa kwenda nazo moja kwa moja polisi na TAKUKURU kuzipeleka kama vielelezo.

Badala yake umechukua milioni moja ya rushwa, kisha unaitaka serikali ichukue hatua.

Serikali inatakiwa kuanza kuchukua hatua kwako wewe kwa kula rushwa iliyoharibu ushahidi.
 
Ukienda kwenye yard kununa gari wewe nenda na fundi wako unayemuamini aangalie engine, gear box na body kama vipo vizuri . Ukienda na fundi janja janja mpenda pesa atakuchomesha atachukua pesa kwako na kwa hao wauza magari kwani kuna ishara atapewa arudi baadae kuja kuchukua mzigo wake. Hiyo habari ya km achana nayo kabisa utapotea. Unakuta gari ya mwaka 1995 imeletwa hapa kwetu 2022 halafu eti imetembea km 10,000 si maajabu hayo.
 
TBS wapo busy kukimbizana na akina mama walala hoi pale Kasumulu border, wanaohangaika na vibiscuits!,hii nchi ni shida kila kona!,pls my IGP chukua hawa police wako peleka Botswana,even for a 14days waone wenzao wanavyofanya kazi ,Tanzania bila RUSHWA INAWEZEKANA, why Gaborone wamefanikiwa kwa hili?,Zambia wanasogea nao kuwa wasafi sisi tumekwama wapi
 
Wewe ni sehemu ya tatizo.

Hizo picha ulitakiwa kwenda nazo moja kwa moja polisi na TAKUKURU kuzipeleka kama vielelezo.

Badala yake umechukua milioni moja ya rushwa, kisha unaitaka serikali ichukue hatua.

Serikali inatakiwa kuanza kuchukua hatua kwako wewe kwa kula rushwa iliyoharibu ushahidi.
Whistle blower nimesha fanya kazi yangu na wao serikali wafanye kazi yao
 
TBS wapo busy kukimbizana na akina mama walala hoi pale Kasumulu border, wanaohangaika na vibiscuits!,hii nchi ni shida kila kona!,pls my IGP chukua hawa police wako peleka Botswana,even for a 14days waone wenzao wanavyofanya kazi ,Tanzania bila RUSHWA INAWEZEKANA, why Gaborone wamefanikiwa kwa hili?,Zambia wanasogea nao kuwa wasafi sisi tumekwama wapi
Mchawi wetu utawala wa CCM. CCM ina urafiki mkubwa sana na rushwa
 
Whistle blower nimesha fanya kazi yangu na wao serikali wafanye kazi yao
Wewe si whistle blower, wewe ni selfish and greedy Tanzanian.

Whistle blower angepeleka ushahidi polisi na TAKUKURU.

Wewe ni mmoja ya walioshiriki kuwawezesha hao watu kufanya biashara yao chafu.

Tena sasa hivi watafanya kwa umakini zaidi, kwa sababu umeshawastua. Umefanya iwe vigumu zaidi kuwakamata.

Umewauza wenzako kwa vipande vya fedha.

Wewe ni mla rushwa na msaliti.
 
Kwani yale maduka yamefunguliwa jana? Si yapo miaka nenda rudi? Mbona hawajawahi kamatwa?
 
Back
Top Bottom