DOKEZO Serikali tusaidieni wananchi, magari yanayouzwa kwenye yard za Wapakistan mitaa ya Morocco na Victoria ni mabovu sana

DOKEZO Serikali tusaidieni wananchi, magari yanayouzwa kwenye yard za Wapakistan mitaa ya Morocco na Victoria ni mabovu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Waombe file la Gari lilio tokanalo japan,Ukiona wanakupiga janjajanja sepa.

Option nyingine,chukua VIN(Vehicle Identification Number) ya Gari i-search mtandaoni possibility kubwa Ni kuikuta Gari hio na details zake zote(maana Gari hizo zinauzwa minadani hukk Japan) then linganisha Km za hii Gari hapo Yard vs Km ikiwa huko Mnadani.

Zamani Nilikua nalipia pesa kidogo ($10) kwny website flani,nawatumia VIN then wananitumia details zote za hio Gari,Ila hii sites iko shutdown siku hizi.
Sikuhizi unatumbukiza chassis number kwenye google tu gari lazma itajitokeza ikiwa Japan kabla haijapanda meli na utaona details za kms. Wale waliotoa magari beforward huwa wanaumbuka mapema sana maana gari haijifichi.
 
Kurudisha Odometer sio zoezi la saa moja. Ni zoezi la muda kidogo.

Jan Motors wao hawa gari zao utaikuta kama ilivyo na bei zao ziko chini, hivyo watu huenda kwao wananunua afu wanaenda uza tena
Eh kwa Jan Motors bei zao zile ni rahisi mtu kununua na kuuza juu kidogo baada ya kuchezea odometer.
 
Sikuhizi unatumbukiza chassis number kwenye google tu gari lazma itajitokeza ikiwa Japan kabla haijapanda meli na utaona details za kms. Wale waliotoa magari beforward huwa wanaumbuka mapema sana maana gari haijifichi.
Kwani tofauti ya Chassis number vs VIN Ni Nini mkuu?
 
TBS wapo busy kukimbizana na akina mama walala hoi pale Kasumulu border, wanaohangaika na vibiscuits!,hii nchi ni shida kila kona!,pls my IGP chukua hawa police wako peleka Botswana,even for a 14days waone wenzao wanavyofanya kazi ,Tanzania bila RUSHWA INAWEZEKANA, why Gaborone wamefanikiwa kwa hili?,Zambia wanasogea nao kuwa wasafi sisi tumekwama wapi
Mkuu hata uwapeleke mbinguni askari wa Tanzania hawawezi kuishi bila rushwa, hii ni kutokana na mishahara yao ni midogo mno. Askari polisi wa Tanzania ukikutana nao wamevaa gwanda, ndiyo wanaonekana wa maana. Kaangalie wanapoishi, hawana tofauti na wale ombaomba wanaolala viwanja vya mnazi mmoja.
 
Noma sana, hii ya kuchezea odometer inafanywa sana, wanajua wabongo wengi wanaangalia uchache wa mileage na sio service history. Kwa hiyo wanarudisha odo nyuma ili kutupa tunachokipenda.

Hongera kwa kupata milioni 1 na bado umefichua uovu. Sasa hapo polisi nao wanakwenda kujipatia hela huko.
mtumba maanake nn?
 
Noma sana, hii ya kuchezea odometer inafanywa sana, wanajua wabongo wengi wanaangalia uchache wa mileage na sio service history. Kwa hiyo wanarudisha odo nyuma ili kutupa tunachokipenda.

Hongera kwa kupata milioni 1 na bado umefichua uovu. Sasa hapo polisi nao wanakwenda kujipatia hela huko.
Jifunzeni kununuwa gari kwa kuaangalia muonekano halisi wa gari,Mambo sijui ya km au no plate ni ya mwisho kabisa, km au no plate ukitaka unapewa to hata km 0, maana hivyo ndiyo mnavizingatia na wajanja wanapita na nyie humo humo!!!
 
Mzee alinunua land cruiser ila mpaka Sasa ashakua fundi garage[emoji1787][emoji1787] jinsi Chuma inavomsumbua ni miaka kama SITA ila bado anaishi nayo
Kuna gari nyingi tu za mda mrefu lakini hadi leo watu wanaishi nazo, kiki moja tu chuma kinanyanyuka! Dingi yako kuna mafundi tu walimuharibia gari, maana kuna mafundi anaweza tia ugonjwa gari yako hadi ukaichukiya!!!
 
Kuna gari nyingi tu za mda mrefu lakini hadi leo watu wanaishi nazo, kiki moja tu chuma kinanyanyuka! Dingi yako kuna mafundi tu walimuharibia gari, maana kuna mafundi anaweza tia ugonjwa gari yako hadi ukaichukiya!!!
Hii ilianza mauzauza first hand tu toka alipoinunua
 
Serikali itupie macho uhuni unaofanywa na hawa wafanyabiashara wa magari wenye asili ya Pakistan.

Jana mida ya saa sita mchana tulienda na rafiki yangu kwenye moja ya maduka (yard) ya kuuzia magari. Rafiki yangu alikuwa anataka Toyota Probox kwa ajili ya kubebea mizigo yake Kariakoo na kwenye godown yake.

Tukafika hiyo saa sita tukakuta magari ndiyo yanapangwa. Walivyomaliza tukaomba kukagua gari moja. Kijana akaitwa akaja mbio na funguo za gari zikiwa mkononi kwake.

Nikakaa kwenye usukani na rafiki yangu pembeni. Nilipoiweka gari switch on nikakuta odometer inasoma gari imetembea kilometa 219,551. Bei milioni 16

Tukashauriana tukasema hapana hili gari halifai. Tukaendelea duka jingine na jingine na jingine.

By saa tisa tukafudi tena kwenye ile Probox, tukakuta ishachezewa odometer, sasa inaonekana imetembea kilometa 46,755.

Nilikuwa nimeoiga picha chasis namba mlangoni na dashboard. Nikipowauliza mbona hii gari mmeichezea kilometa, nikawaonyesha na picha wakakasirika sana wakapora simu yangu. Nikawaambia kaeni nayo, leo mtalala polisi.

Nikawa naondoka kulekea kwenye gari tuliyokuja nayo hapo yard, ndipo mmoja ya wafanyabiashara wale akaja mbio huku akinibembeleza nifute zile picha watatupa million moja.

Hela tamu, tukakubali kufuta picha, tukabeba milioni yetu. Tukaondoka.

Lakini backyard ya hizo yard zote kuna mafundi wako busy wanayaweka sawa mamikweche hayo.

Kingine tulichogundua ni kwamba kwenye minada ya magari, magari ya nauzwa kwa classes. Hawa wanachagua class duni kabisa, yakifika hapa wanaongea vizuri na wakaguzi, wanatolewa bandarini.

Kwa somo hili tulilojifunza jana rafiki yangu amekata tamaa kabisa na magari haya. Sasa kaona bora aagize kutoka Japan 🗾 asubiri siku 45 abebe mwana wake wa uhakika
Bado ninajiuliza kimaadili, hiyo millioni mliipokea ni ya kazi gani!

Tusipigie kelele mambo tunayoyahusudu na kuyatenda.
 
Hawa waliwahi kunikosakosa maeneo ya Aghakan,nilipowastukia wakaniambia watanipigia simu,baada ya kuona kimya nikawapigia simu ikawa inaita bila majibu,nikaona baadaye kama walini blacklist maana ilikuwa haipatikani tena...
 
Back
Top Bottom