Serikali: Wahanga vyeti feki kulipwa mafao yao

Serikali: Wahanga vyeti feki kulipwa mafao yao

Kati ya Serikali na wao nani mwizi hapo??

Hawajaiibia tu Serikali pia wamesababisha watu wenye sifa kukosa hizo nafasi.

Hawa hawakustahili kulipwa, walipaswa washtakiwe kwa ulaghai au kughushi nyalaka ( wataalamu wa sheria wanaweza kufafanua zaidi)
Tatizo liko kwa nani? Walitumia kigezo gani kuingia makazini? Nani aliwapokea? Au ajira zilikuwa zinauzwa Kama sokoni? Kosa nila mwajiri au aliyedanganya?
 
Tatizo liko kwa nani? Walitumia kigezo gani kuingia makazini? Nani aliwapokea? Au ajira zilikuwa zinauzwa Kama sokoni? Kosa nila mwajiri au aliyedanganya?
Kuna pande mbili;

Aliyedanganya na aliyedanganywa (serikali)

Aliyedanganya alikusudia kufanya hivyo kwa kuambatanisha nyalaka ambazo anajua si sahihi.

Aliyedanganywa hakukusudia kumuajiri mtu aliyeghushi nyalaka, ilitokea kwa sababu hakuwa na mfumo na miundombinu rafiki kulibaini hilo. ( hii haifuti kosa la aliyedanganya)
 
Mifumo ya elimu ya zamani ilikuwa siyo tafiki.

Unakuta mkoa mzima una private secondary school moja. Darasa zima wanaenda secondary school wanafunzi wawili. Kurudia darasa la 7 ni marufuku. Mtu anaenda mahali pengine, anarudia darasa kwa kutumia jina la mtu mwingine. Au aliyepata nafasi ya kuendelea sekondari za serikali ameamua kutokwenda, anaenda seminary school, anampa nafasi ndugu yake.

Hao watumishi walionewa kwa sababu ya nafasi zao. Mbona akina Bashite, Madelu, Bagalile (wachache tunaowafahamu), hawakufukuzwa.
Lakini Unakuta kijana ana miaka 35 au 36 then ameliwa kichwa kwa vyeti hiyo unaisemaje Mkuu?

Serikali ingewaangilia watu waliobakisha miaka michache tu kustaafu na sio vinginevyo
 
Tatizo liko kwa nani? Walitumia kigezo gani kuingia makazini? Nani aliwapokea? Au ajira zilikuwa zinauzwa Kama sokoni? Kosa nila mwajiri au aliyedanganya?
Wizi ni wizi tu usitake kuupaka mafuta! Kitendo cha kuchukua vyeti si vyako kwenda navyo chuo au sehemu ya kazi ukavitumia isivyo halali ni uharifu! Huu uzuzu upo hapa kwetu tu nchi za watu wenye akili huwezi kukuta upumbavu kama huu!

Ushawahi kujiuliza vijana wangapi waliohitimu vyuo wapo mtaani kwa miaka mingi bila ajira? Unachukuaje hela ya walipa kodi kwenda kumlipa mtu mwizi wakati kipindi chote alichokuwa anafanya kazi na vyeti vyake feki alikuwa anapokea mshahara isivyo halali! Au ndio wale mnaoendeshwa na mihemko na busara za kipumbavu?
 
Watapewa michango yao tu, sio ya mwajiri wala sio pension.

Wengi wameliwa vichwa wakiwa na mshahara chini ya m1 na wakiwa kazini pungufu ya miaka 15 na ikumbukwe walianza kazi na mishara midogo sana pungufu ya laki.

Watapata hela pungufu ya milion 6
Ikumbukwe kuwa laana za vijana walioondolewa mavyuoni Joyce Kuna siku atajuta. Wale vijana Kama wazazi wait walikuwa hawana uwezo ni Kama serikali iliuwa ndoto zao. Ni afadhali lingefanyika marekebisho hata Kama nikuanzisha vyuo vya ufundi wangepelekwa huko Kama kifungoni wakitoka huko wakiingia mitaani wajiajiri.
 
Lakini Unakuta kijana ana miaka 35 au 36 then ameliwa kichwa kwa vyeti hiyo unaisemaje Mkuu?

Serikali ingewaangilia watu waliobakisha miaka michache tu kustaafu na sio vinginevyo
Hawa wote hawatakiwi kupewa chochote! Kwani wasipopewa maisha hayataenda? Mbona watu kibao wapo mtaani wanapambana huku wanadgree na diploma zao halali kwenye makabati huko! Hawa ni wakuwatema wakafie mbele wezi hao!
 
Kuna pande mbili;

Aliyedanganya na aliyedanganywa (serikali)

Aliyedanganya alikusudia kufanya hivyo kwa kuambatanisha nyalaka ambazo anajua si sahihi.

Aliyedanganywa hakukusudia kumuajiri mtu aliyeghushi nyalaka, ilitokea kwa sababu hakuwa na mfumo na miundombinu rafiki kulibaini hilo. ( hii haifuti kosa la aliyedanganya)
Sasa wewe unamlaumu vipi? Mrekebishe basi afanyekazi kwa sababu kazi anaitaka. Serikali baada ya kupata miundo fafiki ingeanzia Happ bila kusumbua familia za watu.
 
Kati ya Serikali na wao nani mwizi hapo??

Hawajaiibia tu Serikali pia wamesababisha watu wenye sifa kukosa hizo nafasi.

Hawa hawakustahili kulipwa, walipaswa washtakiwe kwa ulaghai au kughushi nyalaka ( wataalamu wa sheria wanaweza kufafanua zaidi)
Tangu waondolewe hao wenye vyeti feki Serikali imeajiri wangapi kuchukua nafasi zao, jiwe ali tuhadaa kwa Mengi sana ambayo mpaka leo tunashindwa kuyapatia ufumbuzi ikiwemo ya Madaraja ya utumishi
 
Watumishi wa Serikali katika Kada mbalimbali ambao waliondolewa kazini kutokana na tuhuma za kuwa na vyeti feki vya taaluma. Serikali imeagiza mchakato wa kuwalipa mafao yao uanze mara moja.

Siku ya leo Mawaziri wawili watafanya mkutano na waandishi wa habari Kuhusu michango ya pensheni waliyokatwa Watumishi waliondolewa kazini baada ya zoezi maalumu la Uhakiki wa vyeti .

Mkutano huo utaongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menijementi ya Umma na Utawala Bora. Mhe.Jenista Mhagama

Pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako.

Mkutano utaanza saa tatu kamili asubuhi katika ukumbi wa PSSSF Tower ghorofa ya Nne Dodoma.
Wanastahiki kulipwa walilitendea kazi taifa
 
Sasa wewe unamlaumu vipi? Mrekebishe basi afanyekazi kwa sababu kazi anaitaka. Serikali baada ya kupata miundo fafiki ingeanzia Happ bila kusumbua familia za watu.
Miundombinu rafiki imeisaidia kujua hao wahalifu na ikawaondoa. (Tena walifanya uhalifu kwa kukusudia)

Ni busara tu zinataka kutumika tena busara zenyewe zimelenga kuwalipa na kuwatumia kisiasa. Tofauti na hapo hawana sifa za kulipwa chochote namaanisha CHOCHOTE.
 
Mtu akiwa na cheti feki ukweli ni kwamba inabatilisha hata ajira aliyoipata kwa kutumia vyeti hivyo. Katika jambo hili nasimama na JPM.

Mambo ya kugushi nyaraka ni kinyume cha sheria. Kwa hiyo basi ile kutokushtakiwa na kuhukumiwa ilikuwa ni huruma tosha kutoka serikalini. Sasa suala la kuwalipa waliogushi vyeti linatoka wapi wakati ajira zao zilikuwa batili!?

Katika baadhi ya mambo nilimuelewa sana JPM. Alikuwa jasiri, mwenye uthubutu wa kuchukua hatua na kufichua uozo. Sasa msimamo wa serikali umeshabadilika na kutaka kuwapa shavu wakosaji!?

RIP Magufuli.
Lowasa ana busara sana. Nasimama na mtazamo wake kuhusu hili suala. Inasemekana hata JPM alitaka kulegeza msimamo na kuwalipa kidogo ila akapumzika.

Raisi ni mlezi wa raia wote, na raia wanafanya makosa. Raisi anategemewa na wafanyakazi, wafungwa, wakulima wa korosho, omba omba, matajiri, masikini.

Woote hawa wanamuhutaji raisi hata wanapokuwa na makosa. Anapoadhibu ni ubinadamu kuhakikisha kuwa adhabu inalenga kurekebisha na sio kutengeneza wategemezi wapya kwa kutoa adhabu kubwa mpaka anayeadhibiwa asiweze tena kusimama yeye na wanaomtegemea.
 
wanastahiki kulipwa walilitendea kazi taifa
Nakwambia walishavuna walichoiba hawastahiki chechote! Taifa la wajinga na wapumbavu linaweza kufanya huo uzuzu! Mtu mwizi wa kuku anapigwa na kuuliwa mtaani lamini mwizi wa vyeti anabembelezwa alipwe na mafao yatokanayo na kazi yake ya wizi kwa kutumia nyaraka feki!

Huu upumbavu uko kwetu na kamwe kwakuleana hutaa uione nchi hii imepiga hatua maana inaendesha bila kuwa na misimo dhabiti kwa waharifu kama hawa wa vyeti feki!

Pia kinachowapomza wabongo wengi ni kuhurumiana lakini akitokea mwizi wa kuku mtaani hawawezi kumhurumia ila mwizi wa kutumia karamu kila mtu anamtetea!
Tunaishi enzi za ujima licha ya kujinasibu kuwa wasomi!

Ushawahi kujiuliza watu wangapi walipaswa kupata hizo ajira lakini walizikosa kwa sababu watu waovu walizichukua kwa kutumia vyeti feki!
Tafakarini msijitoe ufahamu taifa hili la kwetu sote!!!
 
Wanastahili kulipwa maana serikali pia ilifanya uzembe na kuajiri watu wasio na vigezo.
 
Nakwambia walishavuna walichoiba hawastahiki chechote! Taifa la wajinga na wapumbavu linaweza kufanya huo uzuzu! Mtu mwizi wa kuku anapigwa na kuuliwa mtaani lamini mwizi wa vyeti anabembelezwa alipwe na mafao yatokanayo na kazi yake ya wizi kwa kutumia nyaraka feki! Huu upumbavu uko kwetu na kamwe kwakuleana hutaa uione nchi hii imepiga hatua maana inaendesha bila kuwa na misimo dhabiti kwa waharifu kama hawa wa vyeti feki!
Pia kinachowapomza wabongo wengi ni kuhurumiana lakini akitokea mwizi wa kuku mtaani hawawezi kumhurumia ila mwizi wa kutumia karamu kila mtu anamtetea!
Tunaishi enzi za ujima licha ya kujinasibu kuwa wasomi!
Ushawahi kujiuliza watu wangapi walipaswa kupata hizo ajira lakini walizikosa kwa sababu watu waovu walizichukua kwa kutumia vyeti feki!
Tafakarini msijitoe ufahamu taifa hili la kwetu sote!!!
ayo maneno yako yangekuwa mazur sana kama ungeweza kubeba uhalisia wa jamaa ..yani kwa mfano wewe ndo ungekuwa wao.
 
Ningeshauri serikali pamoja na kuwalipa pesa zaa iwape hata room tatu za kulala. Kama atakuwa Hana nyumba hiyo hell haitoshi. Wapigiwe mahesabu ya vyumba vitatu na choo serikali iwasaidie pamoja na pesa zao. Maisha ni magumu mno.
 
ayo maneno yako yangekuwa mazur sana kama ungeweza kubeba uhalisia wa jamaa ..yani kwa mfano wewe ndo ungekuwa wao.
Kila binadamu anaubinafsi! Ila ukweli utabaki kuwa ukweli hawa ni wezi hata kama walitumikia taifa ila njia yao ya kuingia kwenye kazi zilikuwa haramu!
Mfano ushawahi kujiuliza watu wangapi wali pata madhara kutokana na huduma za hawa watu wasio na vyeti halali? Daktari asiye na vyeti anamhudumia mgonjwa kwa kutumia uzoefu huu ni uharifu wa hali ya juu!
Wapigwe chini tena hili lisijitudie!
 
Ningeshauri serikali pamoja na kuwalipa pesa zaa iwape hata room tatu za kulala. Kama atakuwa Hana nyumba hiyo hell haitoshi. Wapigiwe mahesabu ya vyumba vitatu na choo serikali iwasaidie pamoja na pesa zao. Maisha ni magumu mno.
Taifa la majuha lolote linawezekana!
 
Back
Top Bottom