Lowasa ana busara sana. Nasimama na mtazamo wake kuhusu hili suala. Inasemekana hata JPM alitaka kulegeza msimamo na kuwalipa kidogo ila akapumzika.
Raisi ni mlezi wa raia wote, na raia wanafanya makosa. Raisi anategemewa na wafanyakazi, wafungwa, wakulima wa korosho, omba omba, matajiri, masikini.
Woote hawa wanamuhutaji raisi hata wanapokuwa na makosa. Anapoadhibu ni ubinadamu kuhakikisha kuwa adhabu inalenga kurekebisha na sio kutengeneza wategemezi wapya kwa kutoa adhabu kubwa mpaka anayeadhibiwa asiweze tena kusimama yeye na wanaomtegemea.