Nyabutoro
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 1,342
- 1,596
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtu akiwa na cheti feki ukweli ni kwamba inabatilisha hata ajira aliyoipata kwa kutumia vyeti hivyo. Katika jambo hili nasimama na JPM.
Mambo ya kugushi nyaraka ni kinyume cha sheria. Kwa hiyo basi ile kutokushtakiwa na kuhukumiwa ilikuwa ni huruma tosha kutoka serikalini. Sasa suala la kuwalipa waliogushi vyeti linatoka wapi wakati ajira zao zilikuwa batili!?
Katika baadhi ya mambo nilimuelewa sana JPM. Alikuwa jasiri, mwenye uthubutu wa kuchukua hatua na kufichua uozo. Sasa msimamo wa serikali umeshabadilika na kutaka kuwapa shavu wakosaji!?
RIP Magufuli.
Boss, Jambo lolote likifanyika kisiasa linatulizwa kisiasa na ndicho kilichofanyika.Mkuu muhalifu hastahili kulipwa chochote, kitugani ambacho huelewi hapo.
Labda kama tulidanganywa kwamba watu walighushi vyeti na imejulikana waliingia kihalali.
Kwa namna yoyote kama nikweli walighushi vyeti kuwalipa makato sijui mafao vyovyote, kuwalipa niwadekeza wahalifu.
Hapo watanzania watakwelewa kidogo. Hapa bwana hatakama serikali ilikosa pesa waliliendea kwa nguvu na kusababisha taharuki katika familia na kuwachonganisha na marafiki, ndugu, na jamii. Hili tatizo lilikuwa la kitaifa. Wangetafuta namna ya kupata hela ili wasisumbue familia za watu.Boss, Jambo lolote likifanyika kisiasa linatulizwa kisiasa na ndicho kilichofanyika.
Nchi tulizidiwa, tukafikiria shortcut ya kubana matumizi tukaja na drs la saba na vyeti feki. Hawa vyeti feki ni watu ambao tupo nao muda na wengi tuliwaajiri wakiwa drs la 7 na kuwalazimisha kujiendeleza wakiwa watu wazima ndipo wengi wakafanya ujanja ujanja na tuliendelea nao sababu tuliwahitaji sio kwamba hawakufahamika.(Serikali kutoa maagizo kwa mtu mwenye miaka 45 akasome elimu ya form four ilijua kuna watakaolazimisha na baada ya kulazimisha ilinyamaza, haikusitisha mkataba sababu utendaji haukuwa mbaya, uzoefu uliwabeba)
Sababu kuu ya kuwaondoa ilikuwa tunahitaji fedha na hatukua na tatizo na vyeti vyao sababu walifahamika.
Kilichokuwa kinaendelea ilikuwa ni kusubiri wastaafu na kuajiri kwa vigezo vipya vya elimu kuanzia form four tofauti na zamani ilivyokuwa drs la saba ila sasa tuna marejesho ya mikopo ya biashara, tuna miradi mikubwa tunafanyaje ili kuwa na fedha?
Tukaamua bana hawa wafanyakazi waondolewe, drs la saba wote na waliofoji vyeti ili tupate pesa. Ila yale maeneo nyeti yasiguswe sababu hatutaweza kupata mbadala, haya maeneo mengine wacha yabaki na mapengo tukiwa na fedha tutaajiri. Tangazo likatoka watu wakafukuzwa.
Sasa ukifukuza watu kisiasa kwa kuacha wengine kuna madhara yake na usipoyatibu lazima yatakutafuna. Yataibuka kila mwaka na utalazimika tu kuyatatua sababu uliadhibu bila usawa.
JPM akaanza, akarekebisha kwa kurudisha drs la saba na inasemekana alikuwa na mpango wa kuwarekebishia wa vyeti feki ila MUNGU hakumpa huo muda akamwita. Samia akamaliza kwa kuwapa 5% na huu mjadala utaisha.
Mkuu tuna changamoto ya mifumo ya usahili hivyo mambo haya yanapotokea inakuwa ni kama kengele.Hapo watanzania watakwelewa kidogo. Hapa bwana hatakama serikali ilikosa pesa waliliendea kwa nguvu na kusababisha taharuki katika familia na kuwachonganisha na marafiki, ndugu, na jamii. Hili tatizo lilikuwa la kitaifa. Wangetafuta namna ya kupata hela ili wasisumbue familia za watu.
Kwa kweli huu unyama na ukatili ni laana hata mungu hakuachi.
Mfano Familia ambayo imekumbana na vyeti feki hapo hapo wakaambiwa nyumba inavyunjwa, Happ hapo mtoto kafukuzwa chuo alama zake hazistahili asome hapo ukiwa ni mzazi, kaka, Dada, mjomba, shangazi, rafiki utajisikia je? Ukiwa na ubinadamu lazima umwonee huruma huyu mtu.
Sio kuwafokea mweleweshe akwelewe. Wapigaji serikali wapo wengi kuliko wanavyojua. Tena walioiandaa hiki kituko wanaweza kuwa ndio wezi wakubwa. Walifanyaoazi wakawa wanalipwa kuandaa uhakiki was kuwashusha wenzao kaburini.
Chochote walichokuwa wakilipwa au kukatwa katika mishahara yao kilikuwa ni batili, kwa kuwa hata mikataba yao ya kazi ilikuwa pia ni batili, "null and void ab initio"Hawalipwi mafao, wanapewa makato ile 5% ya mshahara waliyokuwa wanakatwa kwenye mshahara. Serikali imekuwa na msimamo tofauti na hili hitimisho lako.
Ukiamua kuadhibu wahalifu ndani ya serikali siasa weka pembeni na sio jambo jepesi. Samia yupo sahihi, hili suala linakwenda kuisha.Chochote walichokuwa wakilipwa au kukatwa katika mishahara yao kilikuwa ni batili, kwa kuwa hata mikataba yao ya kazi ilikuwa pia ni batili, "null and void ab initio"
Kwa hiyo hata hiyo unayosema ni makato ya 5% bado ni batili. Hawa washukuru huruma ya serikali kwa kutowafungulia mashtaka ya kugushi nyaraka na kijipatia kipato kwa njia ambayo si halali. Hili kundi la wahalifu kama wengine ambao walipaswa kushitakiwa na jamuhuri.
Rais Samia ni mtu siyo sawa na yule mwingine 👇Watumishi wa Serikali katika Kada mbalimbali ambao waliondolewa kazini kutokana na tuhuma za kuwa na vyeti feki vya taaluma. Serikali imeagiza mchakato wa kuwalipa mafao yao uanze mara moja.
Siku ya leo Mawaziri wawili watafanya mkutano na waandishi wa habari Kuhusu michango ya pensheni waliyokatwa Watumishi waliondolewa kazini baada ya zoezi maalumu la Uhakiki wa vyeti .
Mkutano huo utaongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menijementi ya Umma na Utawala Bora. Mhe.Jenista Mhagama
Pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako.
Mkutano utaanza saa tatu kamili asubuhi katika ukumbi wa PSSSF Tower ghorofa ya Nne Dodoma.
Watumishi wa Serikali katika Kada mbalimbali ambao waliondolewa kazini kutokana na tuhuma za kuwa na vyeti feki vya taaluma. Serikali imeagiza mchakato wa kuwalipa mafao yao uanze mara moja.
Na kwanini walifanya sabotage? Kutumia vyeti ambavyo sio halali
Kwa makusudi kabisa, Serikali inaamua kuwachafua wananchi klwake walioitumikia serikali kwa kuwaita WATUMISHI WA VYETI FEKI. Mwaka 2017 wapo walioondolewa kazini kwa sababu ya kuwa na vyeti vya kughushi na waapo walioondolewa kazini kwa kuambiwa kuwa walikuwa na elimu ya darasa la saba (elimu chini ya KIDATO CHA NNE). Idadi ya walioondoshwa kwa kuwa na elimu chini ya kidato cha 4 ni wengi kuliko walioghushi vyeti, ila sasa wote wanawekwa kapu moja, VYETI BANDIA, ni uonevu aisee.Badala ya kuhakikisha vijana wanajiajiri kwa kuwapa mitaji unaenda kutupa mamilioni ya fedha kwa watu waliogushi vyeti! Stupid!
Ni siasa tu, ahadi kama vile kampeni.WATALIPWA LINI ? MAANA HII POROJO NI YA MUDA MREFU SANA , mnawadanganya watu wanajipa matumaini huku mkijua kumbe ni uongo mtupu !
Wengine walionewa kabisa , mfano ;kuna mtu cheti cha O level kina jina Aisha Juma Mandamo halafu A level na shahada kina jina Asha Juma Mandamo halafu anaambiwa amegushi cheti ni halali hiyo ?Kati ya Serikali na wao nani mwizi hapo??
Hawajaiibia tu Serikali pia wamesababisha watu wenye sifa kukosa hizo nafasi.
Hawa hawakustahili kulipwa, walipaswa washtakiwe kwa ulaghai au kughushi nyalaka ( wataalamu wa sheria wanaweza kufafanua zaidi)
Samia Ni chaguo la Mungu, magufuli aliwasibu wengi na hakuwa na utu kabisaWatumishi wa Serikali katika Kada mbalimbali ambao waliondolewa kazini kutokana na tuhuma za kuwa na vyeti feki vya taaluma. Serikali imeagiza mchakato wa kuwalipa mafao yao uanze mara moja.
Siku ya leo Mawaziri wawili watafanya mkutano na waandishi wa habari Kuhusu michango ya pensheni waliyokatwa Watumishi waliondolewa kazini baada ya zoezi maalumu la Uhakiki wa vyeti .
Mkutano huo utaongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menijementi ya Umma na Utawala Bora. Mhe.Jenista Mhagama
Pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako.
Mkutano utaanza saa tatu kamili asubuhi katika ukumbi wa PSSSF Tower ghorofa ya Nne Dodoma.
Jiwe alikuwa shetani kabisa,huwezi kudhulumu jasho la mtuHivi kweli unaandika kusapot. Wezi? Nchi hii ya Ajabu sana. Tena Magufuli aliwaonea huruma hawa majizi.
Tunasomesha Watoto wetu kwa gharama kubwa wanakosa Ajira. Kwa sababu kuna watu wanafanyakazi kwa kutumia vyeti feki.
Siungi mkono hoja ya SERIKALI kuwalipa wezi fedha tena ilitakiwa warudishe fedha zote za walipa kodi walizolipwa kwa miaka yote.