Serikali wekeni sheria mtu asiingie airport bila VISA na Tiketi ya kusafiria

Serikali wekeni sheria mtu asiingie airport bila VISA na Tiketi ya kusafiria

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Kumezuka wimbi la watanzania ambao wamekua wakijiingilia aiport utadhani ni stendi ya basi.

Hili limekua ni tatizo kubwa muda mwingine linapunguza hata usalama.

Sasa tufanye yafuatayo ili kutokomeza tatizo hilo.

1. Mtu anayeenda kumpokea mgeni wake awe na kopi ya visa, tiketi ya kusafiria na passport ya huyo mtu anayekwenda kumpokea.

2. Mtu anayesafiri asiruhusiwe kuingia airport bila visa, tiketi na passport.

Airport za wenzetu huwezi kuingia kienyeji kienyeji bila hizo documents nilizotaja.
 
Nchi zipi hizo unaongelea? Kama hujawahi kwenda hizo nchi pitia Youtube uone utaratibu wa kupokea/ kuingiza wageni mwisho ni wapi.

Pili Ticket ya ndege inayo reference number ukimtumia mtu aka cancel trip yako au aka edit siku/ saa yako ya safari utamlaumu nani? Watanzania tunahitaji EXPOSURE sana jinsi ulimwengu unaenda.
 
Mbona utaratibu ni mzuri sana pale Airport. Terminal 2 wasindikizaji wanaishia pale nje. Terminal 3 wanaingia ndani ya lile jengo lakini hawafiki sehemu ya kupandia. Terminal 1 nilipanda zamani kidogo hata sikumbuki utaratibu lakini siyo ishu sana mana ni vile vindege vidogo vya coastal aviation. Kimsingi hakuna tatizo kabisa
 
Kumezuka wimbi la watanzania ambao wamekua wakijiingilia aiport utadhani ni stendi ya basi.

Hili limekua ni tatizo kubwa muda mwingine linapunguza hata usalama.

Sasa tufanye yafuatayo ili kutokomeza tatizo hilo.

1. Mtu anayeenda kumpokea mgeni wake awe na kopi ya visa, tiketi ya kusafiria na passport ya huyo mtu anayekwenda kumpokea.

2. Mtu anayesafiri asiruhusiwe kuingia airport bila visa, tiketi na passport.

Airport za wenzetu huwezi kuingia kienyeji kienyeji bila hizo documents nilizotaja.
Hiko kitu uliona airport gani. Wenzetu wapo busy hawawezi kwenda tu airport wakati wanamajukumu mengine
 
Tutajie angalau viwanja vitatu ambavyo wasindikizaji wanishia nje. Hata Dubai yenyewe nadhani hujawahi fika. Kiwanja kimoja tu ambacho wasindikizaji walikuwa wanapata shida nayo ni Terminal 2 basi shida ni kuwa ndani panyewe ni padogo. Terminal 3 at leaset sasa watu wanapumua.
 
Back
Top Bottom