Serikali ya awamu ya tano ilikusanya kodi Trilioni 1.3 kwa mwezi, leo awamu ya sita yakopa fedha hizohizo kutoka IMF kwa matumizi yaleyale

Ilikuwa propaganda, waulize watu wa TRA. Mbilikimo alikuwa anakusanya nusu ya hayo mapato

Mbilikimo alipika takwimu nyingi to compensate for his inferiority complex baada ya kuharibu uchumi imara ulioachwa na Mkwere.
Wewe utakuwa lijinga na pimbi mkubwa. Baada ya kuwa mmemuua Dkt Magufuli mnatengeneza propaganda za kumchafua kwa kutunga uongo. Suala la kodi inajulikana, kodi kweli ilikusanywa na ushahidi upo! Ila wewe muuaji wa rais wetu Mzalendo Dkt Magufuli unalazimisha uongo ila watanzania ni werevu wanajua nia yenu ovu mlivyojipanga na ndiyo maana kila mnalokuja nalao mnachekwa na kuumbuka. Niambie Tanzania ni nchi masikini??????? Je ni sahihi kukopa hicho kiasi??????? Dkt Magufuli kaacha nchi na reserve ya miezi sita, je hayo makusanyo yangekuwa uongo ingewezekana???? Hivyo ujue wewe pimbi na ujinga wenu tunaujua, just the matter of time. Badala ya kushughulikia na maendeleo ya watanzania mnakaa kila kukicha mnatunga uongo juu ya Dkt Magufuli. Na kibaya uongo wenu hakuna mtanzania anayeukubali. 2025 mtajua Dkt Magufuli ni nani.
 
Wakati huo mwendakuzimu si bado alikuwa hai au?

Chukua hii fact, Mbilikimo alikuwa anakusanya mapato kidogo kuliko Mkwere baada ya kuvuruga uchumi.

TRA katika historia yake haijawahi kukusanya 2 trillion au karibia na hicho kiasi.
Unaweza ukawa na chuki binafsi, lakini namba hazidanganyi, Kama angekua anakusanya nusu ya alichokua anakusanya mkwere jiulize haya;

Jk kwa mwezi alikua anakusanya takribani bil. 700, kwa maana hiyo JPM alikua anakusanya nusu yake yaani bil. 350

Mishahara peke yake inafikia ni takribani bil. 650, sasa JPM alikua anapata wapi fedha ya kulipa mshahara tena kwa wakati tarehe 22 kila mtumishi wa umma mzigo umeingia. Wakati JK watu walikua wanalipwa mshahara mpaka tarehe 35 tena kwa kukopa kwenye mabenki.

Miradi mikubwa yote aliitekelezaje? SGR, Ndege zimenunuliwa cash, barabara mpaka mitaani, vituo vya Afya, Madaraja na Vivuko, Elimu Bure, Mikopo ya Wanafunzi. Vyote hivi JK aliekua anakusanya fedha nyingi alishindwa kuvifanya.

Ndugu yangu huoni aibu?

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
ila siasa ni mbaya sn au mm sielewi tumekatwa tozo tujenge vituo vya afya na madarasa leo tena tunakopa kwaajili ya vitu hivyohivyo tena

kama tumetozwa kwa mwezi tumepata madarasa na vituo vya afya vingi inamaanisha kwa mwaka tutapata vingi saidi na vivaa na watumishi pia kulikuwa nahaja gani yakuchukua huu mkopo pia kuna kipindi hp nyuma nilimsikia waziri mkuu akisema tutapata mkopo kutoka WB kwaajili ya elimu na kujenga madarasa
naona kama mikopo inakua mingi tu

ila inaonekana hawa jamaa niwajanja sn wanatupa mikopo wanajua hela zinarudi kwao kwakununua chanjo na vifaa tiba kwahy hawana hasara wanapiga kotekote

nakumbuka kauli ya maguful alisema kuliko watupe hela za mkopo nafuu kama msaada bora watusamehe baazi ya madeni wanayo tudai

nashauri mama aombe msamaha wa madeni kuliko kukopa ili hela tunazo kusanya zitusaidie kweny hili janga

kuliko kupiga hatua tano mbele nakupiga hatua kumi nyuma hatuta fika.
 
Aliwezaje kujenga miradi yote hiyo bila makusanyo ya TRA? Kwa hiyo ile kauli ya kupora pesa za wafanyabiashara imekufa tena??!!

Jpm hata mmesemeje Legacy yake itaishi milele, ameacha alama zinazoishi, kila ukiona Kati ya hivi lazima umkumbuke (SGR, Bwawa la umeme Rufiji, Ubungo flyover, Salender bridge, Busisi Bridge n.k)
Mikopo yenye riba za juu

Hakuna mradi wowote uliogharamiwa kwa pesa za ndani
 
Unaweza ukawa na chuki binafsi, lakini namba hazidanganyi, Kama angekua anakusanya nusu ya alichokua anakusanya mkwere jiulize haya;

Jk kwa mwezi alikua anakusanya takribani bil. 700, kwa maana hiyo JPM alikua anakusanya nusu yake yaani bil. 350

Mishahara peke yake inafikia ni takribani bil. 650, sasa JPM alikua anapata wapi fedha ya kulipa mshahara tena kwa wakati tarehe 22 kila mtumishi wa umma mzigo umeingia. Wakati JK watu walikua wanalipwa mshahara mpaka tarehe 35 tena kwa kukopa kwenye mabenki.

Miradi mikubwa yote aliitekelezaje? SGR, Ndege zimenunuliwa cash, barabara mpaka mitaani, vituo vya Afya, Madaraja na Vivuko, Elimu Bure, Mikopo ya Wanafunzi. Vyote hivi JK aliekua anakusanya fedha nyingi alishindwa kuvifanya.

Ndugu yangu huoni aibu?

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
Hujanielewa, alikuwa hakusanyi nusu ya mkwere, alikuwa anakusanya nusu ya mapato aliokuwa akiyatangaza na hiyo miradi mikubwa yote ni mikopo 100%
 
Katika kile serikali inachoamini kufufua uchumi ulokwamishwa na janga la UVIKO-19, mapema mwezi ulopita wa August iliandika barua ya kuomba mkopo IMF.

Katika barua hiyo ambayo iliandikwa na waziri wa fedha Mwigulu Nchemba na Gavana wa BOT Florens Luoga, serikali imeahidi matumizi mazuri ya mkopo huo na kuainisha maeneo kama elimu, afya, utalii na mfuko wa TASAF.

Serikali ya Tanzania imekuja na mpango uitwao TCRP yaani Tanzania Covid-19 Social Economic and Response Plan ambapo uwingi wa wanafunzi madarasani na ujenzi wa majengo mapya ya madarasa yatapewa kipaumbele, kuboresha huduma za afya, kuongeza huduma za chanjo au vituo vya kutolea chanjo hizo na kuhakikisha dawa za chanjo zinakuwepo kwa wingi pamoja na vifaa vyote vya kusaidia kutibu wagonjwa wa UVIKO-19.

Kwa mujibu wa Bloomberg IMF wamefurahishwa sana na mkakati huo wa Tanzania kurudisha afya ya uchumi wake wa kati iloupata mwezi Julai mwaka 2020.

Tanzania iliingia uchumi wa kati baada ya uchumi wake kukua kwa asilimia 5.8 ambapo makadirio yalikuwa ni asilimia 6.6

Ikiwa ni moja ya nchi ziloathirika kiuchumi Tanzania iliathirika kwenye sekta za utalii na uwezekaji wa moja kwa moja au FDI kutokana na baadhi ya sera zake kubadilika khasa katika sekta ya madini.

Serikali imekuja na mipango thabiti ya kujikoa kutoka kwenye janga hilo la UVIKO-19 kwa kuweka tozo mbalimbali je, tozo hizo hazitoshi kwa matumizi ya angalau maeneo mawili kwa kuanzia?

Lakini kitendo hicho cha kuomba fedha huku na kule ilhali kwa miaka mitano ilopita tuliweza kukusanya kodi ya kwango hichohicho cha mkopo yaani dola milioni 600 ni uthibitisho kuwa watanzania tuna matatizo makubwa.

Je, twashindwa kusema tunatumia kila baada ya miezi kadha kununua dawa za chanjo kutoka kiwandani kwenyewe.

Je, vipi kama leo serikali ikisema italipa shilingi milioni 500 kununua dawa za chanjo kwa wanohitaji na kutuma ndege kuchukua dawa hizo iwe ni Ujerumani au wapi twashindwa kweli?

je, twashindwa kupanga bajeti ya kulipia wanafunzi kwenye mpango wa elimu bure, ujenzi wa madarasa na miundombinu yote muhimu?

Leo eti watu waketi chini kuandika barua ya kuomba mkopo IMF mkopo ambao ni sawa na makusanyo ya kodi kwa mwezi na zaidi!

Hivi tuko vipi?

Ama kweli, nchi hii ni ngumu.
Una hangaika Sana mkuu,matumizi Yale yale ndio nini?

Baada ya kukusanya pesa mlipeleka wapi?
 
Ilikuwa propaganda, waulize watu wa TRA. Mbilikimo alikuwa anakusanya nusu ya hayo mapato

Mbilikimo alipika takwimu nyingi to compensate for his inferiority complex baada ya kuharibu uchumi imara ulioachwa na Mkwere.
Kama wangekuwa wanakusanya hizo pesa ilikuaje wakashindwa kukamilisha mradi hata mmja miaka yote hiyo?
 
Kama wangekuwa wanakusanya hayo mapato SGR ingekamilika 2019 kama ilivyopangwa.

Halafu eti wanatuambia SGR inachelewa miaka miwili kwasababu ya mvua za msimu 🤣🤣🤣
 
Katika kile serikali inachoamini kufufua uchumi ulokwamishwa na janga la UVIKO-19, mapema mwezi ulopita wa August iliandika barua ya kuomba mkopo IMF.

Katika barua hiyo ambayo iliandikwa na waziri wa fedha Mwigulu Nchemba na Gavana wa BOT Florens Luoga, serikali imeahidi matumizi mazuri ya mkopo huo na kuainisha maeneo kama elimu, afya, utalii na mfuko wa TASAF.

Serikali ya Tanzania imekuja na mpango uitwao TCRP yaani Tanzania Covid-19 Social Economic and Response Plan ambapo uwingi wa wanafunzi madarasani na ujenzi wa majengo mapya ya madarasa yatapewa kipaumbele, kuboresha huduma za afya, kuongeza huduma za chanjo au vituo vya kutolea chanjo hizo na kuhakikisha dawa za chanjo zinakuwepo kwa wingi pamoja na vifaa vyote vya kusaidia kutibu wagonjwa wa UVIKO-19.

Kwa mujibu wa Bloomberg IMF wamefurahishwa sana na mkakati huo wa Tanzania kurudisha afya ya uchumi wake wa kati iloupata mwezi Julai mwaka 2020.

Tanzania iliingia uchumi wa kati baada ya uchumi wake kukua kwa asilimia 5.8 ambapo makadirio yalikuwa ni asilimia 6.6

Ikiwa ni moja ya nchi ziloathirika kiuchumi Tanzania iliathirika kwenye sekta za utalii na uwezekaji wa moja kwa moja au FDI kutokana na baadhi ya sera zake kubadilika khasa katika sekta ya madini.

Serikali imekuja na mipango thabiti ya kujikoa kutoka kwenye janga hilo la UVIKO-19 kwa kuweka tozo mbalimbali je, tozo hizo hazitoshi kwa matumizi ya angalau maeneo mawili kwa kuanzia?

Lakini kitendo hicho cha kuomba fedha huku na kule ilhali kwa miaka mitano ilopita tuliweza kukusanya kodi ya kwango hichohicho cha mkopo yaani dola milioni 600 ni uthibitisho kuwa watanzania tuna matatizo makubwa.

Je, twashindwa kusema tunatumia kila baada ya miezi kadha kununua dawa za chanjo kutoka kiwandani kwenyewe.

Je, vipi kama leo serikali ikisema italipa shilingi milioni 500 kununua dawa za chanjo kwa wanohitaji na kutuma ndege kuchukua dawa hizo iwe ni Ujerumani au wapi twashindwa kweli?

je, twashindwa kupanga bajeti ya kulipia wanafunzi kwenye mpango wa elimu bure, ujenzi wa madarasa na miundombinu yote muhimu?

Leo eti watu waketi chini kuandika barua ya kuomba mkopo IMF mkopo ambao ni sawa na makusanyo ya kodi kwa mwezi na zaidi!

Hivi tuko vipi?

Ama kweli, nchi hii ni ngumu.
Mpuuzi kama mjombako mwendazake.

Mwendazake hakuokota kodi bali kuiba hela ktk account za watu.

Mungu na amtupe motoni
 
*WENYE AKILI TUNAFAHAMU TULIENDESHWA KIPROPAGANDA ZAIDI NA SIO KIUHALISIA,
MF;*alikuwa anazindua mradi fulani huku mnaona bango kabisa limeandikwa mfadhili,yeye hapo hapo anatamka tunajenga wenyewe what was this?
Katika hiyohiyo unodai propaganda walimu na watumishi walilipwa mishahara kwa wakati tarehe 22.

Wanafunzi wote si waliendelea na masomo kwa mpango wa elimu bure?

Hizi fedha si zilitokana ni hiyohiyo kodi?
 
Mpuuzi kama mjombako mwendazake.

Mwendazake hakuokota kodi bali kuiba hela ktk account za watu.

Mungu na amtupe motoni
Mpuuzi ni weye unaeamini hela ziliibwa kutoka kwenye akaunti za watu kwa miaka mitano mfululizo.

Hao watu walikuwa na kiasi gani benki?

Kama kweli mna ushahidi kuwa aliiba kwanini mumuue badala ya kumwajibisha?

Mnaogopa nini?
 
Ilikuwa propaganda, waulize watu wa TRA. Mbilikimo alikuwa anakusanya nusu ya hayo mapato

Mbilikimo alipika takwimu nyingi to compensate for his inferiority complex baada ya kuharibu uchumi imara ulioachwa na Mkwere.
Ndio mama TISS wakamdunga sindano
 
Haya mambo yalikuwepo ata awamu zilizopita. Usiaminishe kwamba kipindi cha Mwendazake watu hawakukwepa kodi.

Kipindi hiki wenye maduka Kariakoo si ndio kwa uwingi walikuwa wanawapa Machinga mizigo yao jioni wanaletewa hesabu, alafu kwenye mauzo ya EFD NIL.
[emoji122][emoji122][emoji122]

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Halafu wewe Richard siku hizi ni kama umechanganyikiwa (kumradhi), hujui kama serikali iliyopita iliendeshwa kwa propaganda?

Mfano hai nilionao mezani hapa ni report iliyoandaliwa na watu walio finance uchaguzi mkuu wa 2020, kuanzia kuwatrain mawakala na process zingine zote na pesa zilizotumika, wakati tuliambiwa tunafanya uchaguzi kwa pesa za ndani!!!
 
Mie sijachanganyikiwa ondoa shaka, nipo safi kabisa.

Najaribu kuainisha yanoendelea nchini mwetu.

Ni watu wepi wali finance uchaguzi wa 2020?

Taarifa zilizokuwepo wakati ule ni kwamba JPM alikataa fedha za nchi wafadhili zilokuwa na masharti (na ambazo walizoea kuzitoa) na kuamua kutumia fedha za ndani.

Na kama report unayo kwanini umeibana hadi leo?

Hiyo yamaanisha kwamba ulinyamazia hizo propaganda?

Tufafanulie kidogo.
 
Mleta mada naona upeo wako ni mdogo sana! Nchi haiongozwi kishamba kama unavyofikiri wewe! Huwezi kuchukua mapato yote ya mwezi dola milioni 500 eti unaenda kununu dozi za COVID-19,maeneo mengine utayaendeshaje!? Jielimishe acha kukimbilia chuki za kijinga! Rais Magufuli alishakufa kubali hilo na kazi iendelee!
vitu vingine ni logic tu wanashindwa kufikiria vizuri kilakitu wamekaa kupingapinga na kuzodoa zodoa hii nchi ngumu sana hasa ukiwa kiongozi hela unapata ila na presha, kisukari unavipata pia..
 
Mnyonge mnyongeni lakininukweli ninkwamba jpm alikusanya mapato mengi huo ndo ukweli.
 
Back
Top Bottom