Serikali ya Burundi yatangaza kifo cha Rais Pierre Nkurunziza

Serikali ya Burundi yatangaza kifo cha Rais Pierre Nkurunziza

Status
Not open for further replies.
Mkewe yuko huku Kenya tunamtibu corona, poleni RIP in peace ila nakumbuka alikua mkaidi kwenye suala la corona, isiwe ndio imemlamba.
Nae angekuja Kenya kutibiwa sijui alikuwa hataki?
 
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza aaga dunia.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza (55) amefariki dunia. Taarifa ya serikali imeeleza kuwa alikuwa hospitali akisumbuliwa na tatizo la moyo.

Serikali ya Burundi imetangaza kifo cha Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza (55). Mshtuko wa moyo umetajwa kuwa chanzo cha kifo chake.

Rais Nkurunziza alizaliwa Desemba 18, 1964 na ameongoza nchi hiyo kuanzia mwaka 2005 hadi mauti ilipomfika.


Hivi ni vile vifo vya ghafla ghafla ambavyo nguvu kubwa sana hapa kwetu imekuwa ikitumika kulazimisha kuwa havikusababishwa na Corona.

Ila ni wazi kuwa habari za mkewe kukutwa Corona, yeye mwenyewe kuwa na Corona na walinzi wake kuwa na Corona ndani ya wiki takribani mbili zilizopita hazikuwa ngeni.

Burundi first lady in Kenya for COVID-19 treatment

Tetesi: - Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza pia apatikana Corona

Ikumbukwe pia kuwa Nkurunziza alikuwa amekataa kuchukua hatua zozote thabiti kuhusiana na Corona akidai kuwa Mungu aliipenda sana Burundi kwa Corona kuwafikia.

Pia alikaidi miito yote kuahirisha shughuli za uchaguzi mkuu mwezi jana na mwezi huu ili kuidhibiti mikusanyiko ya watu. Pia alikaidi kusimamisha mikusanyiko ya makanisani na misikitini.

Maisha nchini kwake yaliachwa kuendelea kama yanavyoendelea hapa kwetu.

Yale yale ya wale wabunge wetu, wakuu wa wilaya, ma OCD na ma OCS yule bwana wa TABOA na wengi wengine. Vifo vya ghafla!

Tangulia kwa amani bwana Pierre kwa hakika umetuachia somo. Hadi litakapoeleweka si muda mrefu utakuwa mwenyeji wetu tu.

Nyuma yako mbele yetu. Twaja mkuu!
 
Kumbuka kuwa wiki iliyopita mkewe alisafirishwa kwenda Nairobi kwa matibabu ya corona na haikuwa siri
Mimi naona huwenda attack attack ikawa imesababishwa na kuwekewa sumu...

Kumbuka huyu bwana hakuwa kipenzi cha warundi wengi kitendo cha yeye ku step down from power ikawa ndio nafasi ya kummaliza kimyakimya...
 
Nasikia tunataka kutangaziwa kuwa hapa kwetu hakuna tena corona imekimbia maombi
Kwasababu mapafu yanaposhindwa kusafirisha oxygen ya kutosha mwilini moyo unaongeza mapigo ili hiyo oxygen kidogo isambae.
 
Naam, hakika Mwenyezi Mungu hajaribiwi, RIP Nkurunzinza,
 
Mimi naona huwenda attack attack ikawa imesababishwa na kuwekewa sumu...

Kumbuka huyu bwana hakuwa kipenzi cha warundi wengi kitendo cha yeye ku step down from power ikawa ndio nafasi ya kummaliza kimyakimya...
Madikteta wote ni lzm wawe na heart attack check hata kiduku wa Korea, sababu wamejaza sumu,visasi,choyo,PhD za roho mbaya,mioyoni mwao sababu ya kumtumia shetani badala ya Mungu.Mawazoni mwao wamejaza full negative jinsi ya kuuwa upinzani,ngono,uchawi na ushirikina,hofu na mashaka,kutojiamini, extremely inner selfness yanatamani Kodi za wananchi zote ziwe zao.Yana kila kitu lkn yamekosa amani ya moyo.
Sehemu yao sahihi ni kuzimu ili wamsaidie shetani kazi ya kuchochea kuni Mungu utukosea Sana kutuletea duniani nusu binadamu nusu jini.
 
Nini hiki? Mungu Fundi, Bora umefariki umeachia nchi kwenye taharuki ndogo tofauti ungefia madarakani.

Binadamu siku zetu ni chache Sana hapa duniani na hazina idadi maalumu.
RIP Nkurunzinza, poleni wana Burundi wote.

Nkurunzinza aliidharau sana covid 19 akaona ni ugonjws wa kawaida.Katikati ya corona aliruhusu kampeni za uchaguzi mkuu huku ligi za mpira zikiendelea, hakuruhusu vipimo vya corona nchini mwake kwahiyo hakutangaza walio ambukizwa wala vifo nk

Wiki jana wanafamilia wake akiwemo mkewe walikimbizwa Nairobi kwa ajili ya matibabu ya covid 19, leo hii naye kaondoka .

Ni ujumbe tosha kwamba haya magonjwa yakiingia si ya kuchukulia powa,tahadhari muhimu lazima zichukuliwe,na hasa ukiwa kiongozi mkuu wa nchi lazima kuhamasisha matumizi ya tahadhar badala ya dharau kama kwamba hakuna kinacho endelea.
Tuchukue tahadhar Corona ipo na inaua na hadi sasa haina dawa wala kinga
 
Halafu madikteta wote wamesoma au wamewahi ishi Tanzania,M7,pk,nkuru,kabila,mnanga,Ina maana tz ni chuo cha udikteta? Only Kenya tu ndo awajawahi ishi au soma tz.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom