Kwa kila mtu anayeifuatilia Kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti Mbowe na wenzake 3 huko kwenye Mahakama Kuu, atagundua kuwa hii Kesi ni ya kubambika, kwa maana ya kuwa Majaji wake wanaopangwa ni wa michongo, mawakili wake walioko upande wa Jamhuri, walio upande wa mashitaka nao ni wa michongo hata mashahidi wao waliopangwa kushuhudia "uongo" dhidi ya Mwenyekiti Mbowe, nao ni wa michongo!
Kitu kingine ambacho kimekuwa ni kibaya zaidi na kimeleta taswira mbaya zaidi kwa Taifa letu kwa Jumuiya ya kimataifa, nao wamebaini kuwa Kesi hiyo ni ya kisiasa.
Kulithibitisha hilo ni namna mabalozi wa nchi za Magharibi wanavyoifuatilia kwa ukaribu mno kesi hiyo na hawapendi kukosa hata "session" moja ya Kesi hiyo.
Hii Kesi pia imepata "coverage" kubwa Sana kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, kuvitaja vichache tu Kati ya vyombo hivyo ni BBC World, Al jazeera na CNN.
Imefikia hatua Kesi hiyo imepiga hodi hadi kwenye viunga vya Bunge la Ulaya na imejadiliwa kwa kina, kuwa Kesi hiyo ni ya kisiasa na Bunge hilo limemtaka Rais Samia, aifute Kesi hiyo bila masharti yoyote yale, ama sivyo nchi yetu iwe Katika "risk" ya kibano cha kukosa misaada mikubwa inayotoka kwenye Jumuiya hiyo ya Ulaya.
Kutokana na Hali hiyo tete, serikali ya Rais Samia, imekuwa ikifikiria namna itakavyoondokana na fedheha hiyo kubwa na ikifikiria namna bora zaidi ya kuifuta Kesi hiyo bila kupata aibu kubwa kutoka kwa watanzania na Jumuiya ya kimataifa.
Ndiyo wamekuja na "Plan A" ya kupanga kikao cha Baraza la vyama vya siasa na msajili wa vyama vya siasa pamoja na Jeshi la Polisi, kujadili kile walichokiita namna bora zaidi ya kuendesha shughuli za kisiasa nchini, huku wakipanga kumwalika Rais Samia kuwa mgeni rasmi wa kukifungua kikao hicho.
Kitu kingine ambacho "kilipangwa" ni kumteua mwanasiasa Zitto Kabwe, awe ndiyo msemaji mkuu wa kambi ya upinzani nchini na kumomba Rais Samia Ili aweze kuwa na huruma na kumuachia huru.
Hivi kwa Mwenyekiti Mbowe kutekeleza wajibu wake kama kiongozi mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema, kuwashawishi wananchi Ili kuishinikiza serikali ikubali kuwa na Katiba mpya ya nchi, nalo ni kosa hadi abambikiwe Kesi ya ugaidi?
Hivi kwa walomsikiliza Rais Samia akijibu hoja hiyo ya Zitto, kuwa Mbowe alivunja sheria na anapaswa kuwa mtii kwa mamlaka iliyopo madarakani, hivi hayo majibu yana busara kweli??
Rais Samia kujifanyia kama hayajui majukumu ya wapinzani nchini ndiyo kujenga ile demokrasia anyoiita "vibrant" nchini?
Sasa imefika hatua shinikizo limekuwa kubwa sana kutoka kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani na kwa wanaharakati kutoka ndani ya nchi na Jumiya ya kimataifa kuitaka serikali ya Rais Samia, iifute Kesi hiyo ya "kubambika" na serikali imelazimika kuwa haina "option" nyingine zaidi ya kusalimu amri na kufikiria kumwachia Mwenyekiti Mbowe bila masharti yoyote!