PostGE2025 Serikali ya Tanzania yajibu matamko EU, Marekani na mashirika ya kimataifa

PostGE2025 Serikali ya Tanzania yajibu matamko EU, Marekani na mashirika ya kimataifa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Mbona haijaandikwa kwa mipasho?
11-03-2025-11-20-36-am-4114517.jpg
 
Mabalozi wanafuatilia kwa karibu sana kinachoendelea nchini wala hawategemei taarifa za Waziri wa mambo ya nje pekee.

Hiyo tume haiaminiki toka siku wajumbe wanateuliwa na tukaona inapangiwa cha kufanya siku ya uzinduzi wake.
Mabalozi wa wenzetu ni makachero waliobobea sio teuzi za kupongezana na zawadi
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea na kuzingatia matamshi na matamshi yaliyotolewa kwa nyakati tofauti wiki iliyopita na washirika wa maendeleo na serikali kuhusu Tanzania na matukio ya tarehe 29 Oktoba 2025. Hizi ni pamoja na Ubelgiji, Canada, Denmark, Ujumbe wa Umoja wa Ulaya, Finland, Ufaransa, Ghana, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Poland, Slovakia, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Mataifa, Uswidi, Uswidi wa Amerika, na Wakfu wa Thabo Mbeki.

Tanzania imebainisha kwa kusikitishwa na yaliyomo katika taarifa hizo, licha ya mazungumzo ya wazi kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na wajumbe wa Kikosi cha Wanadiplomasia kilichoidhinishwa kuwa Tanzania, uliofanyika tarehe 28 Novemba 2025. Pamoja na kutambua nafasi ya jumuiya ya kimataifa katika kukuza demokrasia na maendeleo ya kijamii na kisiasa nchini, lakini pia inatambua umuhimu wa Tume ya Uwekezaji katika kuwekeza kwa usawa. vurugu za baada ya uchaguzi na kutoa ripoti.

Matokeo ya ripoti yataleta uelewa wa matukio ya bahati mbaya yaliyotokea na kuunda msingi wa ushirikiano wa kujenga siku zijazo. Tanzania bado ina nia ya dhati ya kujenga ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya amani na maendeleo na inatoa wito kwa wadau wote kuruhusu mifumo ya kitaifa ya kutekeleza hatua na hatua zinazochukuliwa na serikali.

Zaidi ya hayo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapenda kuihakikishia jumuiya ya kimataifa na washirika wa maendeleo utayari wake na dhamira yake ya kuendelea kushirikiana katika masuala yote yenye maslahi kwa pande zote, kama washirika sawa.

Imetolewa na

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
mbona hawajasema wataturudishia lini maiti zetu naona kama barua ya mshenga kuposa mchumba tu
 
Ilibidi wajibu hata kwa hii broken english maana Sweden wametangaza kuvunja ushirikiano. Wanajua anayefuata ni Denmark, Holland, Norway na Finland.
Baadaye ufaransa na uingereza. Wamescruti wakakumbuka wataagiza whisky kutoka wapi?
Halafu barua haikua na sinye ya Grishone.
 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika taarifa kwa vyombo vya habari imesema Serikali imepokea taarifa na matamko kwa umma yaliyotolewa kwa nyakati tofauti na washirika wa maendeleo na Serikali za mataifa mbalimbali kuhusu matukio ya Oktoba 29, 2025.

Wakati na baada ya uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025 yalifanyika maandamano yaliyozaa vurugu katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Dar es Salaam, Mwanza, Mara, Mbeya, Geita, Dodoma, Songwe na Arusha.

Vurugu hizo zilisababisha vifo, majeruhi, uharibifu wa mali za umma na binafsi. Miongoni mwa mali zilizoathirika zaidi ni kuchomwa moto vituo vya polisi, ofisi za serikali za mitaa, vituo vya mafuta na mabasi yaendayo haraka na nyumba za watu kadhaa.

Taarifa iliyotolewa leo Desemba 5, 2025 na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha wizara hiyo imesema taarifa na matamko hayo yanajumuisha yaliyotolewa na Ubelgiji, Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Ufaransa, Ghana, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Poland, Slovakia, Hispania, Sweden, Uswisi, Uingereza, Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Marekani na Taasisi ya Thabo Mbeki.

Wizara imesema Tanzania imeguswa hususani na maudhui ya matamko hayo, licha ya mazungumzo ya wazi kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Balozi Mahmoud Thabit Kombo) na wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania, yaliyofanyika Novemba 28, 2025.

Taarifa imesema ingawa inatambua mchango wa jumuiya ya kimataifa katika kukuza demokrasia na maendeleo ya kijamii na kisiasa nchini, ni muhimu pia kutambua kuanzishwa kwa Tume ya Uchunguzi ambayo itachunguza ghasia za baada ya uchaguzi na kuwasilisha ripoti.

Wizara imesema matokeo ya ripoti hiyo yataleta uelewa wa matukio yasiyofurahisha yaliyotokea na kuwa msingi wa ushirikiano wa kujenga katika siku za usoni.

“Tanzania itaendelea kuwa na dhamira ya ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya amani na maendeleo. Inatoa wito kwa wadau wote kuruhusu mifumo ya kitaifa kutekeleza hatua na mikakati iliyochukuliwa na Serikali,” imesema taarifa hiyo.

Majibu mepesi na ya hovyo. Waondoke. Hili ndilo jibu.
 
Back
Top Bottom