PostGE2025 Serikali ya Tanzania yajibu matamko EU, Marekani na mashirika ya kimataifa

PostGE2025 Serikali ya Tanzania yajibu matamko EU, Marekani na mashirika ya kimataifa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Mlizika watu wanahema, yaani mshayakanyaga tena ya moto moto. Mlizima Internet ili mfanye yenu mkidhani wazungu kujua information za Dunia hii wanatumia hivi vi fibre vyenu ya Voda na Tigo - ha ha ha ha

Pambaneni....
 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika taarifa kwa vyombo vya habari imesema Serikali imepokea taarifa na matamko kwa umma yaliyotolewa kwa nyakati tofauti na washirika wa maendeleo na Serikali za mataifa mbalimbali kuhusu matukio ya Oktoba 29, 2025.

Wakati na baada ya uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025 yalifanyika maandamano yaliyozaa vurugu katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Dar es Salaam, Mwanza, Mara, Mbeya, Geita, Dodoma, Songwe na Arusha.

Vurugu hizo zilisababisha vifo, majeruhi, uharibifu wa mali za umma na binafsi. Miongoni mwa mali zilizoathirika zaidi ni kuchomwa moto vituo vya polisi, ofisi za serikali za mitaa, vituo vya mafuta na mabasi yaendayo haraka na nyumba za watu kadhaa.

Taarifa iliyotolewa leo Desemba 5, 2025 na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha wizara hiyo imesema taarifa na matamko hayo yanajumuisha yaliyotolewa na Ubelgiji, Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Ufaransa, Ghana, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Poland, Slovakia, Hispania, Sweden, Uswisi, Uingereza, Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Marekani na Taasisi ya Thabo Mbeki.

Wizara imesema Tanzania imeguswa hususani na maudhui ya matamko hayo, licha ya mazungumzo ya wazi kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Balozi Mahmoud Thabit Kombo) na wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania, yaliyofanyika Novemba 28, 2025.

Taarifa imesema ingawa inatambua mchango wa jumuiya ya kimataifa katika kukuza demokrasia na maendeleo ya kijamii na kisiasa nchini, ni muhimu pia kutambua kuanzishwa kwa Tume ya Uchunguzi ambayo itachunguza ghasia za baada ya uchaguzi na kuwasilisha ripoti.

Wizara imesema matokeo ya ripoti hiyo yataleta uelewa wa matukio yasiyofurahisha yaliyotokea na kuwa msingi wa ushirikiano wa kujenga katika siku za usoni.

“Tanzania itaendelea kuwa na dhamira ya ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya amani na maendeleo. Inatoa wito kwa wadau wote kuruhusu mifumo ya kitaifa kutekeleza hatua na mikakati iliyochukuliwa na Serikali,” imesema taarifa hiyo.

Wamekua wapole ghafla, dadeeeeki a
 
Mlizika watu wanahema, yaani mshayakanyaga tena ya moto moto. Mlizima Internet ili mfanye yenu mkidhani wazungu kujua information za Dunia hii wanatumia hivi vi fibre vyenu ya Voda na Tigo - ha ha ha ha

Pambaneni....
Hahaa walidhani wanategemea vifurushi vya voda Nipige tafu.
 
Tatizo Gen Z kama tumehama au tumedhibitiwa sasa. Mbona inshu ya 9D imefifia??

Wengine tumeshajisogeza tupo mjini tunasubiri siku tu.
Wakati wengine wanaikimbia Dar, sisi wengine tumekuja kuungana na wapambanaji wenzetu.
Wanangu wa Dar msiniangushe
 
Tatizo Gen Z kama tumehama au tumedhibitiwa sasa. Mbona inshu ya 9D imefifia??

Wengine tumeshajisogeza tupo mjini tunasubiri siku tu.
Wakati wengine wanaikimbia Dar, sisi wengine tumekuja kuungana na wapambanaji wenzetu.
Wanangu wa Dar msiniangushe
Kwani haya mabarua yamesababishwa na nani kama sio GenZ.
 
Haya kiko wapi na kubana pua 'who are you' hahhahaaa
Kufurahisha vizee vya watu vyenye njaa!
Nimecheka mpaka nimepaliwa na maji, sijui kwanini kabla ya kusoma hii moment sikumeza maji, eti kifurahisha vizee vyenye njaa. Mbaya zaidi vilikuwa vinapigwa makofi kama havijui madhala yaliyotokea🤣🤣
 
Kwahiyo Ile Who are you wameshaifuta au mkubwa hakosei?
 
Serikali walitakiwa wajitathmini pakubwa sana.

Kitendo cha kujibu Kila mara Kila dakika matamko kutoka sehemu mbalimbali duniani means Kuna kitu hakipo sawa na kinatakiwa kifanyiwe kazi ili nchi irudi kwenye default mode.

Ila kwa jeuri na kiburi serikali umekuwa kama inaona sifa kujibu badala ya kushughlikia haya matatizo ambayo hata mtu wa kawaida tu anaona Tz hii siyo ile tuliyoizoea.

Kesho tunaweza kukuta taarifa nyingine "tunamshikilia padre kitima kwa matamko yake dhidi ya serikali na tanesco".

Ni mwendo wa ubabe na matamko tu!!

Nchi inaongozwa na watu wenye viburi na ego.
Hivi kuna kipi cha maana watanganyika walikitarajia Kwa kumkabidhi mamlaka mama wa kiswahili toka pemba? mwenye elimu ya hapa na pale?
 
S100 alifikiri wakisikia WHO ARE YOU? watalegeza msimamo!
WHO ARE YOU shenzema.....
G7WTiheXYAAJPyd.jpg
 
Back
Top Bottom