#COVID19 Serikali ya Tanzania yatoa Katazo la Misongamano isiyokuwa ya lazima kukabiliana na UVIKO

Serikali yapiga marufuku mikusanyiko nchi nzima​



THURSDAY JULY 22 2021​


Summary

  • Serikali imetangaza uamuzi huo wakati idadi ya waathirika wa corona ikifikia 682 ambao wanapatiwa matibabu kwenye vituo vya afya mbalimbali nchini.



By Tatu Mohamed
More by this Author

Dar es Salaam. Serikali imepiga marufuku mikusanyiko yote isiyo ya lazima nchi nzima na ile ambayo itaonekena ni lazima basi tahadhari zote zichukuliwe.


Hatua hiyo inalenga kukabiliana na hofu ya kuendelea kusambaa kwa mlipuko wa tatu wa janga la corona ambao tayari umeathiri mamia ya Watanzania.


Agizo hilo limetolewa Alhamisi ya Julai 22, 2021 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima ambaye amesisitiza utekelezaji wa agizo hilo.


Hata hivyo, agizo hilo limekuja wakati ambao tayari wakuu wa mikoa mbalimbali nchini, wakitangaza kupiga marufuku mikusanyiko isiyo ya lazima kwenye maeneo yao.


Katika agizo lake hilo, Dk Gwajima amewataka viongozi wa Serikali na wa sekta binafsi kuonyesha mfano wa namna wanavyochukua hatua kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19.


Dk Gwajima pia amesema kuwa mpaka sasa idadi ya wagonjwa wa Covid 19 imezidi kuongezeka na hadi kufikia Julai 21,2021 kulikuwa na wagonjwa 682 wanaopatiwa matibabu kwenye vituo mbalimbali.



Amesisistiza kuwa Serikali itaendelea kutoa takwimu hizo pamoja kufuatilia hali halisi ya mwenendo wa ugonjwa huo na kutangaza hatua mbalimbali za kuchukua.


“Ili kuimarisha zaidi kasi ya kuoambana na kudhibiti maambukizi ya UVIKO-19, natamka kuanzia leo tarehe 22/07/2021 nimekataza shughuli zote za misongamano yote isiyokuwa ya lazima . Nimekataza shughuli zote za misongamano na ile yenye ulazima tahadhari ya kutosha ichukuliwe bila kuathiri shughuli za kiuchumi na kitaifa.


“Naelekeza wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuwapa ushirikiano waganga wakuu wa mikoa na wilaya kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria ya Afya ya Jamii Na. 1 ya Mwaka 2009 na kuweka utaratibu mzuri kwa wale wanaoomba vibali vya shughuli zenye ulazima,”amesema Dk Gwajima.


Pia, ametoa wito kwa wananchi wote kujiandaa kupata huduma ya chanjo kama ambavyo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alivyotangaza jana.


“Leo hii wataalamu wa afya wamekutana kupata mafunzo tayari kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma ya chanjo dhidi ya UVIKO-19 kwa hiari na bila malipo,” amesema.
 
Mikusanyiko ipi ni ya LAZIMA na ipi isiyo ya lazima, be specific

Kwa hiyo Covid-19 inachagua mikusanyiko ya kushambulia siyo.
 
Wavunje mechi simba na Yanga Chigoma ndio tutaona wako serious.......
 
Ile dawa ya Madagascar imeishia wapi? Tangu mheshimiwa aliyekwenda kutuletea alipoinywa kule haijasikika tena. Hata hivyo, baadae ilibainika alikunywa sampuli, si dawa.
 
Huyu mama huwa simuelewi kabisa... Kwa nini asiwacoach watu namna ya kujifukiza kama alivyofanya enzi zile.
 
Unafiki mtupu!
Imekuwa unafiki tena? Si mlikuwa mnapiga kelele sana kwamba corona ipo Tanzania wakati ule serikali ilipokuwa inasema haipo? Sasa serikali inasema corona ipo Tanzania kuanzia Machi mwaka huu, nyie mnasema ni unafiki tupu. Wananchi wawaeleweje sasa? Akili yenu ikoje?
 
Tumesoma Tamko la Wizara ya Afya lenye kichwa: Tamko la Katazo la Misongamano isiyokuwa ya lazima" lililotolewa na kusainiwa tarehe 22 Julai 2021 na Waziri mwenye dhamana, Mheshimiwa Dkt. Dorothy Gwajima (Mb.). Kwa mtazamo wetu, maudhui ya tamko hilo kwa kiasi kikubwa yanatoa mwanya kwa watu wa makundi mbalimbali kutoa tafsiri mbalimbali kuhusu maana ya 'misongamano isiyokuwa ya lazima'. Je, ni nani mwenye mamlaka ya kuamua kama msongamano ni wa lazima au sio wa lazima? Ni Polisi, Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, Mganga Mkuu wa Wilaya au Mkoa, Mwenyekiti wa Kijiji au Kitongoji, Diwani au Mbunge, Waziri, nk?

Je, msongamano ni nini na unaanzia watu wangapi? Je, misongamano kama ni yazima lakini ni hatarishi zaidi kwa maambukuzi ya Covid 19 inaweza kuruhusiwa kwa kuwa ni ya lazima? Je, misongamano kama siyo ya lazima inaweza kuzuiliwa hata kama siyo hatarishi kwa maambukuzi ya Covid 19? Maswali ni mengi zaidi kuliko majibu.

Kwa muono wetu, sisi Askofu Mwamakula tunaona kuwa katazo hilo linatoa mwanya wa manung'uniko ndani ya jamii. Kuna uwezekano mkubwa kwa watu wenye mamlaka wakawa wanatoa tafsiri ya neno 'misongamano isiyokuwa ya lazima' kwa lengo la kulinda maslahi ya tabaka hilo. Kwa sababu hiyo, tuna hofu kuwa mazingira hayo yanaweza kuleta misuguano katika jamii hasa endapo baadhi ya makundi yataonekana kubebwa na mengine kukandamizwa! Kwa sababu hiyo, tunatoa wito kwa Wizara husika kulichakata zaidi tamko hilo, vinginevyo litaonekana kama ni 'tamko la kisiasa' lisiloweza kutekelezeka zaidi ya kutaka kudhibiti baadhi ya makundi katika jamii na kuyainua mengine!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
 
Kweli akina Samia wanajichanganya vibaya mno sijui kwanini wanakosa akili ndogo ndogo tu!
 
Tatizo la vuguvugu lolote la kuleta mabadiliko Tanzania huwa lipo mitandaoni tu not otherwise.

Tuna reference nyingi tu na juzi mzee wa escort ya balozi to Ubelgiji alitoa tamko watu wamwagike barabarani nani alithubutu?.

Kiukweli bado sana wasomi na watz kwa ujumla kuthubutu.
 
Nilitehemea watataj in za mikusanyiko hiyo, mfano harusi, mikutano ya kidini n kisiasa, sherehe mbalimbali , michezo, jumuiya za nyumba kwa nyumba, baa,.. N. K
 
Umeanza chokochoko!! Huu waraka ni kumbushio tu, hakuna kitu kigeni hapo!! Lengo kubwa hasa ni kuwapoza watu fulani waone tunatekeleza ushauri wa kidunia maana Tanzania siyo kisiwa japo kwa habari ya corona wapende wasipende, Mungu ameifanya Tanzania kuwa kisiwà!! Ndiyo maana wanaotutakia mabaya tuokote miili barabarani watasubiri sana!!
 
Najibu kutokana tu na headline kwani sijataka kupoteza muda kusoma unafiki wa serikali kudhani we the people are stupid and we can't read between the lines or rather that we can't read through them.
1)Watoto wetu wataendelea kuhudhuria masomo.
2)Kwenye mabasi ya mwendo kasi utatumika utaratibu gani.
3)Vipi kwenye mechi hasa hii 'Kariakoo derby' kule Kigoma mashabiki hawatakuwepo uwanjani?
4)Masoko kama Kariakoo yatafungwa au utatumika utaratibu gani?
5)Vipi kwenye nyumba za ibada, ibada zitasimamishwa kila mtu asalie nyumbani kwake mpaka pale tutakapoi-contain hiyo Covid19?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…