#COVID19 Serikali ya Tanzania yatoa Katazo la Misongamano isiyokuwa ya lazima kukabiliana na UVIKO

mikusanyiko isiyo ya lazima, elewa hiyo lugha chief....
Kwahiyo watu kujazana kwenye madaladala hadi tunashindwa kupata hewa safi nako ni mkusanyiko wa lazima?

Ndo maana watu wanasema lengo la serikali ni kuzuia makongamano ya kudai katiba mpya sio kuzuia maambukizi maana kama serikali ingekuwa serious na maisha ya Watanzania basi ingezuia rasmi mikusanyiko yoyote au kuweka masharti makali kwenye mikusanyiko.
 

Tunalazimishwa kucheza mdundo ambao hata hatuusikii asee...
 
Naomba nimwulize mheshimiwa Dorothy Gwajima: Hivi barakoa kama inamkinga mtu na virusi vya corona kwa nini isimkinge na ukimwi au gonoria au kaswende!! Maana yangu ni kwamba kama mtu akijishonea kondomu kwa kutumia vitambaa wanavyotumia kutengeneza barakoa, halafu akaiwekea elastic kwenye mdomo ili mtu akivaa ibane vizuri, je itazuia virusi vya ukimwi au itazuia bacteria waletao gonoria kwenye tendo la ngono! Msinicheke, nina maana yangu! Maana yangu ni kwamba tunavalishwa barakoa isiyokuwa na ulinzi wowote dhidi ya virusi!! Vaa kondomu ya material ya barakoa halafu uende kwa changudoa mwenye gonoria uone kama kesho yake kama hautatoa usaha mbeleni!! Virusi vya corona ni vidogo zaidi ya bacteria wa gonoria! Kama bacteria wanaweza kupenya kwenye kitambaa cha barakoa, virusi vya corona vitapenya kwa urahisi zaidi. Huu ni ukweli lakini watu wa adanganywa wajikinge kwa barakoa wakati barakoa haiwezi kumkinga mvaaji wake!! Ndiyo maana watumishi wa afya wameambukizwa sana corona duniani kote wakati ni waaminifu kuvaa barakoa!! Barakoa ni biashara, siyo kinga mathubuti!! Vinginevyo watengeneze pia kondomu kwa material ya barakoa!! Mh Gwajima karibu ujibu!
 
Nategemea mbio za mwenge zimeshasitishwa.
 
Mh waziri, umewahi kutembelea shule za bweni za serikali na kujionea watoto wanalala wawili kila kitanda, na double decker zikitenganishwa umbali wa futi 2? Unaiona (ukichungulia dirishani tokea V8 lako) mibanano ya abiria kwenye magari ya usafiri wa umma dar? Mikoani umeongelea lolote kuhusu minada na magulio? Vipi umati wa watu kwenye barabara za mijini zilizo fungwa kuruhusu wamachinga? Tangazo lako ni shinikizo kuhalarisha kukamatwa kwa Mbowe. Serikali haina uchungu na raia wake na ndio maana wizara yako inajivua kuwajibika kwa madhara ya chanjo za Corona.
 
Kwa hivyo vibali vitakuwa na kinga ya virus? Kwa nini pasiwe na standard guidelines? Eg misiba watazika ndugu wasiozidi kadhaa, harusi ukumbi uzidi waalikwa kadhaa, mikutano ya kisiasa ya nje stop, ya ndani umbali uwe kadhaa, nk nk. Mnaingiza siasa kwenye utaalamu, matokeo mnadharaulika.
 
Vuguvugu la katiba limewatoa uvunguni...haya tukutane Kigoma!! CCM lazima mkae safari hii.

Korona ipo sehemu Mh.Mbowe anakanyaga - tutaheshimiana tu.
Una maanisha mahabusu?
 
Katazo hili ni la hila na lina lengo la kukomoa kikundi cha wanaotaka katiba mpya. Vipi mikusanyiko ya michezo, ibada, sherehe, ziara za rais na viongozi wa serikali na CCM? Je kuna mikusanyiko isiyo ya lazima?
 
Tupo kwenye mwenge hatuna habari, sijui kwa nini wemeruhusu Mwenge,kwani una ulazima gani
 
Corona hii mpya yenyewe inashambukia wana kongamano la katiba tu...mambo ya mpira Covid-19 haisogei... mashabiki jazeni uwanja.

Hiii ndiyo Tanzania na hii ndiyo CCM yetu...hutaki HAMIA Burundi [emoji1060]

Na mwenge pia haisogei
 
Imetoa behewa za kupereka mashabiki wa mpira kwenda kusamba UVIKO19 Mkoani Kigoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…