Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba, amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, kulifungulia Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, ambalo lilikuwa limekumbwa na changamoto za kiuendeshaji.
“Limetokea tukio kubwa hapa, naye ametoa msamaha. Na sasa ametoa msamaha pia kwa taasisi za kidini ambazo nazo zilikuwa na changamoto ndogondogo.
Waziri wa Mambo ya Ndani, natambua upo hapa baada ya hapa fuatilia utaratibu mzuri. Ziandikie upya taasisi za kidini kuhusu masharti yao na mipaka ya uendeshaji.
Na zile ambazo zilikuwa na shida wape uangalizi wa miezi sita. Natambua hii ya Ufufuo na Uzima, kaifungulie, wape masharti, na uangalizi wa miezi sita,” amesema Dk Mwigulu.
Ameongeza kuwa kukosea kwa taasisi moja hakupaswi kupelekea kufungiwa kwa taasisi zote, akisisitiza kuwa ibada ni uhusiano kati ya mtu na Mungu wake, hivyo vitendo vya viongozi havipaswi kuwanyima waumini haki ya kuabudu.
Dk Mwigulu ametoa kauli hiyo leo, Jumatatu Novemba 24, 2025, wakati akizungumza na wananchi wa Ubungo, eneo la Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kukagua uharibifu wa vituo vya mabasi uliosababishwa na vurugu za Oktoba 29, 2025.
Kanisa hilo lilifutiwa usajili, Juni 2, mwaka huu kutoka na kile kilichoelezwa katika barua ya Msajili kuwa, limekiuka masharti na sheria kwa kuhusisha siasa katika membari ya kanisa hilo.
Hatua hiyo, iliibua sintofahamu iliyosababisha kufunguliwa kwa kesi na waumini wa kanisa hilo.
==========
Habari ya mjini ndio hiyo, hali imekuwa ngumu mpaka kupelekea wasalimu amri.
Pia wamejitenga na viongozi wa dini wanaotetea dhuluma.