..PM kwa uchaguzi upi na nyie acheni kumpa mileage..!msamaha kwa kosa gani Gwajima alifanya? PM hawezi kufanya jambo lake hayo maelekezo ya Rais
..PM kwa uchaguzi upi na nyie acheni kumpa mileage..!msamaha kwa kosa gani Gwajima alifanya? PM hawezi kufanya jambo lake hayo maelekezo ya Rais
Kosa la Gwajima lilikuwa lipi kwani?...Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba, amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, kulifungulia Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, ambalo lilikuwa limekumbwa na changamoto za kiuendeshaji.
“Limetokea tukio kubwa hapa, naye ametoa msamaha. Na sasa ametoa msamaha pia kwa taasisi za kidini ambazo nazo zilikuwa na changamoto ndogondogo.
Waziri wa Mambo ya Ndani, natambua upo hapa baada ya hapa fuatilia utaratibu mzuri. Ziandikie upya taasisi za kidini kuhusu masharti yao na mipaka ya uendeshaji.
Na zile ambazo zilikuwa na shida wape uangalizi wa miezi sita. Natambua hii ya Ufufuo na Uzima, kaifungulie, wape masharti, na uangalizi wa miezi sita,” amesema Dk Mwigulu.
Ameongeza kuwa kukosea kwa taasisi moja hakupaswi kupelekea kufungiwa kwa taasisi zote, akisisitiza kuwa ibada ni uhusiano kati ya mtu na Mungu wake, hivyo vitendo vya viongozi havipaswi kuwanyima waumini haki ya kuabudu.
Dk Mwigulu ametoa kauli hiyo leo, Jumatatu Novemba 24, 2025, wakati akizungumza na wananchi wa Ubungo, eneo la Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kukagua uharibifu wa vituo vya mabasi uliosababishwa na vurugu za Oktoba 29, 2025.
Kanisa hilo lilifutiwa usajili, Juni 2, mwaka huu kutoka na kile kilichoelezwa katika barua ya Msajili kuwa, limekiuka masharti na sheria kwa kuhusisha siasa katika membari ya kanisa hilo.
Hatua hiyo, iliibua sintofahamu iliyosababisha kufunguliwa kwa kesi na waumini wa kanisa hilo.
==========
Habari ya mjini ndio hiyo, hali imekuwa ngumu mpaka kupelekea wasalimu amri.
Pia wamejitenga na viongozi wa dini wanaotetea dhuluma.
Yeah, ignition point ya maandamano ya 29th-Oct ulikuwa hapo kwenye kanisa la Gwaji boy.Nasikia maandamano yalianziaga hapo sijui ni kweli anyway tukutane D9 Samia lazima atoke na akitoka lazima atoke na takataka zake zote alizoziteua.
Huu ni utaratibu wa hovyo kabisa..lazima.utawala wa sheria ufuatweSababu ilikuwa chuki tu.
Wameiba sadaka
Walitaka wamteke wamemkosa wameona wafungue ili ajitokeze wamteke
Kwa hiyo Gwajima kama Hawezi kuwashinda ajiunge naoGT
Hatuwezi kuendelea kuishi.gizani mda wa manyanyaso haupo tena
Kama walifunga kanisa kwa uonevu ni hatua gani wamechukua dhidi ya waonevu.
Je na kama walifunga kihalali ni jambo gani limefanyika mpaka kanisa likafunguliwa tena. Haya mambo lazima yawekwe wazi ili watawala.wasiendelee kuwa kuwa miungu watu.
Huyo Hananja anajisikiaje huko aliko
Ya Chaula kijana aliechoma picha ya Samia yatajirudia😶😶Gwajima anatafutwa, akitokea TU, shwaaaaaaaaaa![]()
![]()
Niliona sehemu pia, ila Gwajima si mjinga hatatokea hadi nusu mlingotiKuna mtu ticktock jana alikuwa anamuonya Gwajima kuwa hapo Mikocheni alipojificha (Hii ni nyumba ya Tatu anahama kujificha) wameshaigundua achomoke haraka na kuwa Gwajima alikuwa na plani ya kukimbia Nchini imegonga mamba kwa ajili ya Hali iliyopo. Akadai hatua inayofuata watalifungua kanisa aangie mkenge wamchuke kiulaini. Hizi kauli za Serikali kuonyesha wanajali, wameumia ni baada ya Makala ya CNN.