Serikali yaagiza zile nyumba ambazo ukuta umepita mbele ya geti, moja ivunjwe ndani ya siku 7

Serikali yaagiza zile nyumba ambazo ukuta umepita mbele ya geti, moja ivunjwe ndani ya siku 7

Aliejenga ukuta hana kosa, huyo alie elekeza geti kwenye barabara bila kuuliza hiyo barabara ni halali au lah ndio aliekosea.

Haya umeelekeza geti kwenye kiwanja cha mtu kisa una hela umejenga chap chap umemaliza,mwenyewe karudi unaongeleshwa unajibu nyodo.

acha watu wapandishe tofali tu,unaleta u faru wako kwenye maeneo ya watu!
 
Na Mimi Kuna jirani yangu nataka nimfanyie roho mbaya maana jeuri,Tulivyonunua kiwanja tuliambiwa tuache njia yeye kajenga watu wanapita kwenye eneo langu bado sijabahatika kujenga.
 
Kuna kipindi hadi Jiwe alikuwa anatatua migogoro ya ardhi!
Wizara ya ardhi na ndio kisheria yana mamlaka ya kutatua migogoro ya ardhi na kutoa maamuzi.

Sio Waziri.
 
Kuna watu wakimiliki kaardhi wanahis kama wamemiliki dunia

Nilijionea nilipofanya kazi kwenye maroli ya mchanga, kuna sehemu mtu anapanga mawe makusudi tu njiani ili msipite.
Jambo hili kinanikera kweli kweli. Hajui kwamba humo anamopita yeye yalikuwa ni maeneo ya watu wamejitolea ili watu waweze kupita!
 
Mimi ningekuwa ni huyo mwenye ukuta, bila kujali kama mwenye geti aliuziwa bila njia au la, ningemuachia hatua 4 - 5 bure kabisa afanye njia. Na nina uhakika nisingepungukiwa chochote. Lakini huyo ni mimi, wewe unaweza kuwa tofauti.
Na huo ndiyo uungwana
 
Mkuu usikimbilie kulaumu upande mmoja,

Binadamu wana hulka ya dharau na kiburi.
Usikiue huyo mwenye ukuta kafanya jitihada za kuonana na mwenye nyumba, akamfungia tinted.
Basi naye akaamua kumuonesha jeuri yake. Usikute hakuwa hata na mpango wa kujenga huo ukuta ni basi tu ili kuiridhisha ego yake.


Usi
Inawezekana pia
 
Kwa nilivyoiona habari japo hawakwenda kwa undani, inaonekana eneo ni lake ila wananchi walikuwa wanapita (it seem like alikuwa bado hajajenga) na ndio maana wanataka kumfidia kwa maslahi ya wananchi walio wengi.
[emoji848][emoji2958][emoji57][emoji19][emoji58][emoji849]
 
Issue kama hii iliwahi mkuta mdg yangu wakati anajenga kwenye eneo lake pale jijini Dar, katikati ya eneo lake ndipo majirani walikuwa wakipita.

Siku anaziba lile eneo na njia majirani wakaja juu mpaka mjumbe alikuja nao, kilichofanyika huyo ndg yangu akaingia ndani akatoka na panga, waliwatimua mbio akiwemo mjumbe, hadi leo kimya.

Kuna wakati binadamu wanakuwa wadudu kama si wanyama kwenye mali za watu!.
 
Ni busara na utu watu kupendana,hata huyo mwenye kujenga ukuta,ili afike kwenye kiwanja chake amepita kwenye Viwanja vya wenzake , lakini busara na utu,wameamua kuacha njia au barabara ya kupita watu na vipando vyao.
Ikiwa kila mtu ataamua kuziba njia au barabara, Watu watafikaje makwao?
 
20220907_234821.jpg

Acha tuonyeshane makali kwanza
 
Huyo jamaa aliyejenga ukuta, ana roho mbaya na alifanya hivyo kwa nia ovu, wivu na husda.
Ajilaani mwenyewe kabla hatujamlaani.
Hapana bali huyo aliyejenga huku akijua kiwanja chake ni kidogo akataka aachiwe hatua kadhaa. Watu wa hivyo ni wakorofi sana.
 
Back
Top Bottom