Serikali yaagiza zile nyumba ambazo ukuta umepita mbele ya geti, moja ivunjwe ndani ya siku 7

Serikali yaagiza zile nyumba ambazo ukuta umepita mbele ya geti, moja ivunjwe ndani ya siku 7

Kwa nilivyoiona habari japo hawakwenda kwa undani, inaonekana eneo ni lake ila wananchi walikuwa wanapita (it seem like alikuwa bado hajajenga) na ndio maana wanataka kumfidia kwa maslahi ya wananchi walio wengi.
You might be perfectly right. Akiktaa huwezi kumlazimisha kuwa nitakufidia......
 
Mimi ningekuwa ni huyo mwenye ukuta, bila kujali kama mwenye geti aliuziwa bila njia au la, ningemuachia hatua 4 - 5 bure kabisa afanye njia. Na nina uhakika nisingepungukiwa chochote. Lakini huyo ni mimi, wewe unaweza kuwa tofauti.
Sasa mwenye geti badala ya kutumia diplomacy nadhani analeta ubabe wa huyo waziri. mahakamani atawashinda labda kwa vile mahakama zetu ni compromised
 
viwanja vya 15mx15m na havina njia
huyu kaamua 'kumaliza' na yule kaamua 'kumaliza'
kazi kweli kweli
 
Kwanini ajilaani ilihali amesema nyumba ndiyo ivunjwe na siyo ukuta? Au mimi ndiyo sijaelewa!!!!
....imesemwa asimamishe ujenzi...kwa hiyo ni huyo anayejenga sasa sio nyumba iliyokamilika....angalia aya ya pili
 
Anayetakiwa kuvunja hapo ni mwenye hiyo Nyumba yenye geti au aliyejenga ukuta mbele ya geti?

Ni yupi hapo aliyevunja sheria na kuziba njia?
Kuna video ya huo ujenzi iko mtandaoni, ukiiona ni kuwa usawa wa huo ukuta wa fensi wenye rangi ni sehemu ya njia inaelekea huko kushoto,ni njia ya kupita gari moja (ya mtaa) hivyo huo ukuta mpya unablock hiyo njia na kufanya iishie hapo.
 

Attachments

  • 20220903_163539.jpg
    20220903_163539.jpg
    22.7 KB · Views: 2
Sijaelewa! Nadhani sehemu hizi hazijapimwa na hivyo mtu anauziwa bila kuonyeshwa njia. Mtu anaamua kujenga ukuta kwenye eneo lake majirani ambao hawakumtaka anayewauzia atoe njia wanaanza kulalamika. Kama sehemu imepimwa, mtu hawezi kuziba njia.
Hivi unawajua maafisa ardhi wa nchi hii mkuu?
 

Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, Juma Makungu Juma, ametoa muda wa siku saba, ili kuvunjwa kwa nyumba iliopo Fuoni Migombani, kwa madai msimamizi wa nyumba hiyo, Hafidh Ahmed Mohammed, amejenga kinyume na utaratibu wa kisheria za mipango miji na vijiji.

Ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara katika eneo hilo la Fuoni Jitimai Shehia ya Migombani Wilaya ya Magharibi B na kumuagiza msimamizi kusimamisha ujenzi, ikiwa ni pamoja na kuvunja eneo ambalo alilazimika kuweka njia na badala yake kwenda kinyume na taratibu zilizopo.

Amesema serikali haina malengo ya kumdhulumu mwananchi, ila ni vyema kwa wananchi kutambua umuhimu wa kuweka njia wakati wanapofanya ujenzi, hivyo kutokana na kitendo kilichofanywa na mmiliki huyo, serikali inalazimika kuchukua hatua.

"Tunapofanya taratibu za ujenzi kwanza tunapaswa kujua, hatupaswi kuziba njia ambayo inatumiwa na jamii, kufanya hivyo ni kosa na yoyote atakayekua anakiuka taratibu za ujenzi hatua huchukuliwa dhidi yake,” amesema.

Amewataka viongozi kushirikiana pamoja katika kutatua migogoro ya ardhi nchini, ambapo mzozo huo haukupaswa kutokea, endapo viongozi waliopewa dhamana ya utoaji vibali wangetimiza wajibu wao kikamilifu.

Ameeleza kuwa kwa mujibu wa sheria anayepaswa kutoa vibali vya ujenzi, ni Kamati ya Udhibiti na Usimamizi Vibali vya Ujenzi (DCU), ambayo mwenyekiti wake ni Mkurugenzi Mipango Miji na Vijii, hivyo wananchi wanapotaka kujenga ni vyema kufika katika taasisi hiyo iliyowekwa kisheria.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji Kutoka Kamisheni ya Ardhi, Muchi Juma Ameir aliwataka wananchi wanapotaka vibali vya ujenzi kufika sehemu husika iliyowekwa kisheria, ili kuepuka athari, ambayo inaweza kutokea.


Source: Habari Leo
Hiyu waziri hajielewi, kama huyo mwenye geti alitaka njia ni kwanini hakununua kioande cha njia na kukiacha njia? Yeye kiwanja chake angeambiwa aache njia angekubali?
 
Sidhani Kama ameziba eneo la njia. Ni sehemu yake watu walikuwa wanapita tu, Sasa akiamua kujenga ukuta kwenye eneo lake utu anaukosaje
Tena kaacha niia ya mwenye heti apite kwa miguu, wala hajaziba, unajengaje geti la kuingiza gari wakati kiwanja ulichonunua hakina njia ya gari? Sasa mtu asijenge kwenye kiwanja chake kwa nini? Yaani kiwanja cha mwenzako ugeuze njia kivipi? Kama unataka njia nunua
 
Sidhani Kama ameziba eneo la njia. Ni sehemu yake watu walikuwa wanapita tu, Sasa akiamua kujenga ukuta kwenye eneo lake utu anaukosaje
Boss, ukiwa na kiwanja chako fanya kashughuli ili jamii isitengeneze njia hapo. Ardhi yote ni mali ya serikali boss, ss raia tunakodisha tu ila serikali ina maamuzi ya mwisho.
 
Back
Top Bottom