Serikali yaagiza zile nyumba ambazo ukuta umepita mbele ya geti, moja ivunjwe ndani ya siku 7

Serikali yaagiza zile nyumba ambazo ukuta umepita mbele ya geti, moja ivunjwe ndani ya siku 7

Sasa mwenye geti badala ya kutumia diplomacy nadhani analeta ubabe wa huyo waziri. mahakamani atawashinda labda kwa vile mahakama zetu ni compromised

Sasa tabu yote ya nini mpaka kuanza kupelekana mahakamani kwa ishu ndogo hiyo? Hivi hata ukishinda kesi, unaishije na huyo jirani? Kumbuka kuna maisha baada ya huo ukuta.. kuna majanga kama moto nk unaweza kujikuta unaenda kuomba hifadhi kwa huyo huyo jirani..
 
Ubaya ubaya. Tupunguze tamaa. Kiwanja kidogo unajenga bonge la nyumba, hapohapo kauli nzuri huna kwa majirani kisa umeweka vioo nyumba. Mm mwenyewe nakunyoosha
 
Huyo mwenye geti inabidi anunue kiwanja kilchojengwa ukuta kwa gharama, maana hapo
 
Additional information hii hapa kutoka kwa mmoja wa mmilki wa awali ili tuone kama aliejenga ukuta ana roho mbaya au la

Boss, ukiwa na kiwanja chako fanya kashughuli ili jamii isitengeneze njia hapo. Ardhi yote ni mali ya serikali boss, ss raia tunakodisha tu ila serikali ina maamuzi ya mwisho.
SIDHANI KAMA ULIVYOSEMA NI SAWA!
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Na Mimi Kuna jirani yangu nataka nimfanyie roho mbaya maana jeuri,Tulivyonunua kiwanja tuliambiwa tuache njia yeye kajenga watu wanapita kwenye eneo langu bado sijabahatika kujenga.
Hufananii roho mbaya,mwite mzungumze kabla hujaanza ujenzi
 
si rahisi kwani hana ndugu mpaka aombe kwa mbaya wake? hapana
Mkuu unataka kuniambia wewe hapo unapoishi ndugu zako wamekuzunguka kiasi kwamba ukipata tatizo wao ndio watakua karibu? Unless uwe unaishi vijijini, kwa mjini mtu wa karibu ni jirani.
 
Mkuu unataka kuniambia wewe hapo unapoishi ndugu zako wamekuzunguka kiasi kwamba ukipata tatizo wao ndio watakua karibu? Unless uwe unaishi vijijini, kwa mjini mtu wa karibu ni jirani.
umesema anaweza akakupa malazi, kwani mjini hatuna ndugu wa tumbo moja, baba mdogo, shangazi, mjomba, rafiki , dada kaka, etc etc
 
umesema anaweza akakupa malazi, kwani mjini hatuna ndugu wa tumbo moja, baba mdogo, shangazi, mjomba, rafiki , dada kaka, etc etc
Sasa kama wewe ndugu zako wapo karibu unadhani na kila mtu ni hivyo hivyo? Mfano: mimi hapa ninapoishi, ndugu yangu wa karibu yupo kilometa 40 kutoka hapa. Kwahiyo unaniambia nikipandisha presha usiku nimpigie yeye mpaka aje kufika si nimeshakufa? Au nyumba ikishika moto, ntatoa vitu nikahifadhi kwa huyo ndugu yangu aliepo km 40 wakati nna majirani tumepakana..
 
Back
Top Bottom