Serikali yaamriwa kufanya maamuzi haraka kesi ya Lissu

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Serikali imeamriwa kutoa uamuzi haraka katika kesi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu.
Wakati wa kutajwa kwa kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam, ilisema kuna haja ya uamuzi wa haraka kufanywa kama kuna ushahidi wa kutosha kumshtaki Lissu au kama hakuna basi aachiliwe.
Mawakili wa upande wa Serikali waliiarifu Mahakama kuwa jalada la kesi hiyo limeshasomwa na kutolewa maoni ya kisheria na sasa lipo tayari kutolewa uamuzi, na wanaomba tarehe nyingine ili uamuzi utolewe.
Wakati wa kesi hiyo Tundu Lissu alitoa maombi mawili.
‘’Mheshimiwa Hakimu, kama upande wa Mashtaka wanao ushahidi wa kutosha, basi wasajili taarifa muhimu Mahakama Kuu ili kesi hii iweze kuhamishiwa huko, au kama hawana ushahidi wa kutosha basi DPP aite Nolle Prosequis kusitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa,’’ Lissu alisema.
Kesi ya Lissu, mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, Chadema anashitakiwa kwa kosa la uhaini ambalo halina dhamana na lenye adhabu ya kunyongwa mpaka kufa, imeahirishwa hadi Julai 15, 2025
 
Inawezekana uamuzi wackumuachilia huru Mh TAL ulikuwa ufanyike Jana,ila kwasababu taarifa ilivuja kabla wakaona wavunge.
 
Swali.

Ikiwa DPP ataamua kuitupilia mbali kesi, je, walioifunguwa hawapaswi kufunguliwa kesi ya usumbufu na kudhulmu haki ya mshitakiwa?
 
Kemeeni ushoga, na sio kuhalalisha ushoga.
Pelekeni muswada bungeni ili mashoga wachukuliwe hatua kali za kisheria tofauti na hapo acheni kutupigia kelele huku katiba inakataza kuingilia uhulu wa faragha
 
Hivi umewah kusikia mashoga wamekamatwa au kuchukuliwa hatua yoyote tangu Samia awe rais? ya kwamba hamna mashoga au

Kama wengi wenu mmechagua upande wa mayahudi na wamagharibi ambao ushoga kwao ni halali, munategemea nini sasa, mkionyesha kupinga hilo basi hata serikali italichukulia serious
 
Back
Top Bottom